Wana JF, niko mbele yenu kwa unyenyekevu kuomba baraka zenu & moral support yenu jambo langu hili liwe! Mniombee Mungu asaidie, awezeshe liwe!

Nakuombea na binafsi sina kinyongo nawe kwakuwa tumeishi kwa kuheshimiana mno na kupeana sitara pale palipokuwa na mitazamo tofauti..!

Kila jambo huanzia rohoni bila kujali asili yake.. Tokeo lolote la kimwili asili yake ni rohoni..! Hili jambo utakalo kama una asili nalo BASI LITAKUWA .. Lakini kama ni 'passive' kutokana na jinsi ulivyoeleza hapo basi kuna shida kidogo.. Nachelea kusema unaweza kuangua pua

Natambua unatambua kwa hakika kwa kipindi cha 2015 mpaka sasa ama kwa kujua au kwa kutojua ulijijengea nguvu hasi kubwa sana...lakini haya si sehemu yake sasa kwakuwa umejinyenyekesha, kujishusha kabisa na kuomba radhi... Ambaye hatakusamehe ajitambulishe na kutuonesha ukamilifu wake! Kwenye hili huna mawaa tena ila kuna hiki kitu kinaitwa KARMA!

Sala na maombezi yetu vitakuwa nawe lakini vinaweza kukosa nguvu chanya ya uchaji wa kiroho kulingana na muktadha wake! Kwamba kama ni nafasi ya kisiasa basi baraka nyingi hukumbana na nguvu za kiza
Mfua vyuma katika ubora wako........
Very interested!!
 
Ulipaswa kutuonesha ulivyoweza kukabili maisha ili tukupe nafasi uwezeshe wengine sasa unatulilia jinsi ulivyoshindwa maisha ili tukupe cheo ukajitafunie maisha kweliii??
Uongozi sio kutia huruma ni kuonesha ujasiri,umahiri na uhodari katika kutafuta maendeleo endelevu binafsi nakisha kwawengine
 
Mkuu

Watu wanaomba au kuiba kwa watu wanaowajua na kuwazunguka

Culture ya uombaji ni ya kuacha kabisa...watu wajitegemee

Yeye kugombea chochote ni yeye kama yeye...angetunza fedha afanyie ugombezi wake na sio kuleta mapvumbv humu kuomba omba upumbavu

Halafu anaomba kwa lugha ya kimasikini sana utadhani ni mwanamke kumbe ni mwanaume

Ndio maana nikasema yaani laiti watoto wake ndio wasome huu upumbavu wake hawataamini kama ndio baba yao anajilegeza kiasi hiki mbele ya jamii analilia msaada kiasi hiki

Mpaka nimeshangaa kabisa.....

Kuna reason kwanini Paskali anadharaulika sana nchini....there is a reason,na inaonekana kwenye uzi wake....useless kabisa
Lakini yeye ameomba zaidi asamehewe kama aliwakwaza watu na pia aombewe Dua ili jambo lake litimie !! Hapo surely hakuna ubaya wowote alioufanya !! Ni mambo ya ya kiungwana kabisa
 
Nakuombea na binafsi sina kinyongo nawe kwakuwa tumeishi kwa kuheshimiana mno na kupeana sitara pale palipokuwa na mitazamo tofauti..!

Kila jambo huanzia rohoni bila kujali asili yake.. Tokeo lolote la kimwili asili yake ni rohoni..! Hili jambo utakalo kama una asili nalo BASI LITAKUWA .. Lakini kama ni 'passive' kutokana na jinsi ulivyoeleza hapo basi kuna shida kidogo.. Nachelea kusema unaweza kuangua pua

Natambua unatambua kwa hakika kwa kipindi cha 2015 mpaka sasa ama kwa kujua au kwa kutojua ulijijengea nguvu hasi kubwa sana...lakini haya si sehemu yake sasa kwakuwa umejinyenyekesha, kujishusha kabisa na kuomba radhi... Ambaye hatakusamehe ajitambulishe na kutuonesha ukamilifu wake! Kwenye hili huna mawaa tena ila kuna hiki kitu kinaitwa KARMA!

Sala na maombezi yetu vitakuwa nawe lakini vinaweza kukosa nguvu chanya ya uchaji wa kiroho kulingana na muktadha wake! Kwamba kama ni nafasi ya kisiasa basi baraka nyingi hukumbana na nguvu za kiza
Kuna nguvu hasi nyingine pia ambayo inaweza kuwa kigingi cha kukwamisha ndoto zako.. Nacho ni chama cha siasa utakachotumia kuombea nafasi firikirika.. Kimejaa tuhuma, ubaya na uchafu wa kila aina... Kimeumiza na kutesa wengi, kimedhulumu na kufanya kila aina ya hila ili kiwepo mahali kipo..! Baraka huwa hazikai mahali kama hapo!

Kwahiyo bro pamoja na maombi yetu ambayo utayapata kwa wingi sana lakini una hizo negative energy tatu zinazokukabilli
. Background yako hasa 2015..
.Nafasi ya kisiasa unayoomba
. Chama cha siasa utakachopitia (as per rumors)
Nguvu hasi itarudi Tu akishapata huyu. Hamna lolote.
Anyhow hata Sisi hua tuna majambo yetu mengi tunayaomba Kwa Mungu atufanikishie pamoja na kuweka jitihada of course, lkn hua hatuji jf kutaka public sympathy. Tuna waomba ndungu na jamaa zetu ktk familia zetu watuombee. Small circle if you know what I'm talking about, ambao keki ikipatikana hua tuna share wote.
Sasa mtu aje hapa jf aanze kupiga magoti as if sie ndie tunapiga hizo Kura za kumchagua.
Pathetic.
 
Mkuu, hizo nafasi zinahitaji uwe mtu wa aina flani hivi.

Yaani uwe mtoto wa kigogo.

Huko ndiko wanakofichana wenye nchi.
 
Wana JF wenzangu,
Kuna msemo usemao "Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu", "Vox Populi is Vox Dei"

Hili ni Bandiko la kukusanya sauti za wengi ili iwe ni sauti ya Mungu. Mimi mwana jf mwenzenu Pascal Mayalla, nina jambo langu ambalo mimi kama mimi peke yangu kama Pascal Mayalla peke yangu na familia yangu tuu, na ndugu zangu tuu, na jamaa zangu tuu na rafiki zangu tuu, pekee, hatuwezi, hivyo naomba kuwashirikisha wana jf ili hili jambo langu, lisiwe ni jambo langu tuu, bali liwe ni jambo letu, umoja ni nguvu, together we can.

Pasikali, sio tuu ni mwenzenu, humu jf, bali mimi ni ndugu yenu. Baadhi tuko humu pamoja toka ile 2006, jf ikiitwa Jambo Forums hivyo ni zaidi ya miaka 15 pamoja!. sasa. Kuna watu tunafahamiana kupitia jf, kuna watu tumesaidiana kupitia jf, na wengine hadi kutembeleana home na kushirikiana kwenye shida na raha na kuna misiba ya wana jf, we drive all the way hundreds of kilometers just to bid farewell to a jf member!.

Enzi zile najiunga jf nilikuwa kijana shababi, kuna mikoa ya baridi, nilikuwa nikitua tuu na kupost kitu chochote, kutoka mkoa huo, pm zitaingia kuniulizia niko nimefikia wapi na hadi blangeti la kuzuia baridi napata kutoka kwa mwana JF!, what a love!.

JF is Like Home to Me, It's More Than A Friend, It's A Family. Nalala jf, naamka jf, nashinda jf, jf is everything!, its a big family, tukianza kuji consolidate na kutumia a consolidated powers ya nguvu yetu ya ushawishi as a pressure group, we can do wonders!. Hii togetherness yetu lets start using it as one, Kwanza Kwa kusahau tofauti zetu za kisiasa na vyama vyetu, tuka supportiana as one, tuka stand together as one kwa jambo letu, ile powers ya pamoja ndio the magic behind!,tutatusua!.

Msione watu wanakusanya the multitude of people nje kwao for a whole day na jioni baada tuu ya kuzama jua, kuwagawia Ten Ten,kuwalisha au kuwafuturisha!.

Au matajiri wanashindana kudhamini timu za mpira za Simba na Yanga, spending billions!. Go find out wafanyakazi wa viwandani kwa matajiri hao wanalipwa shilingi ngapi!, unaweza usiamini, it's not for nothing, the will power is everything!. Hivyo kitu ninachokiomba kwenye bandiko hili kutoka kwako ni kimoja tuu, your will!.

Hivyo kwenye hili jambo langu,
, nawaomba tusimame pamoja kwa kunigawia will zenu!.
  1. Kuna wakati nilipataga ajali mbaya ya Piki Piki, watu wa kwanza to break the news ni JF, hivyo nikasaidiwa nikaokolewa. Thanks JF to save my life, Thanks God for JF.
  2. Nikapelekwa South Africa kutibiwa, Hospital ya Milpark, Wana JF wa Joburg walinifariji Sana. Thanks for all JF brotherhood na Sisterhood
  3. Gharama za Treatment ya South Africa zikawa kubwa kuliko family affordability, hivyo tukatafuta cheaper option, tukapata India, Apollo Hospital, New Delhi. Wana JF wa Dheli walinifariji Sana. Nilichangiwa gharama za matibabu na Wana JF dunia nzima!. Thanks Wana JF for support.
  4. Nikiwa India, kuna tangazo la kazi lilipostiwa humu jf kwenye nafasi za kazi, FCO ya Uingereza, nikaomba na nikapata, nikaajiriwa na FCO na kupostiwa DAR es Salaam. Thanks for JF Kunipatia kazi.
  5. From there JF ndio kama ndugu zangu wa kwanza. Nilikuja kupata matatizo ya kuitwa Dodoma baada ya gazeti la Raia Mwema kuichapisha makala yangu ya jf as their lead story.
  6. Kufuatia matatizo hayo wife akaimaind Sana jf na kunishauri nichague moja ama jf ama yeye!. Huwezi amini, ili kulinda familia niliamua kuachana na if.
  7. Huwezi amini, nilijikuta nimeshindwa ndipo nikajua kumbe jf ni very addictive. Kwanza nikawa naingia Kwa siri, usiku mkubwa akiwa amelala, alipogundua akanikumbusha kuchagua moja, nilichagua jf. Thanks for her understanding. Bado yupo.
  8. Enzi niko fit kiuchumi, enzi zile za harambee, mimi ni miongoni mwa wana JF tuliochangia jf 6 figures!.
  9. Kauli huumba!. Baada ya kuitwa njaa, kiukweli kauli ile iliniumbia njaa kwani, tenders zangu zote za publicty zilifutwa na njaa ya kweli ikanitembelea kweli!. Ukijumlisha na Corona, licha ya kuwa na ndugu, jamaa na marafiki wenye uwezo, ni mwana JF mmoja fulani alijitokeza to my rescue to save me!. Thanks kwa mwana JF huyu!
  10. Sasa leo ninakuja tena kwenu wana JF, nina jambo langu.
  11. Kabla sijalitaja Jambo lenyewe, naomba kwanza kwa unyenyekevu kabisa, kuwaeleza Wana JF wenzangu, kuwa mimi ni binadamu tuu na sio malaika, hivyo kuna watu humu tumepishana kauli, tumekwazana, tumekosana, tumetukanana, nimewakosea, nawaomba msamaha kwa yote niliowakosea na wote walionikosea nimewasamehe, ignore list yangu nime unignore, samahanini Sana!.
  12. Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana!. Naomba msamaha mnisamehe kwa yote kwasababu sisi binadamu wote ni viumbe dhaifu, kukosa ni ubinaadamu na hakuna mkamilifu!. Please forgive me for everything and I apologize for whatever I did wrong to whoever niliye mkosea, samahani sana naomba mnisamehe!.
  13. Jambo langu ni baada ya kujaribu Kawe na kuambulia kura moja!, sasa kumejitokeza fursa nyingine. Hivyo kitu cha kwanza nilichofanya ni kuwashirikisha nyinyi Wana jf, ninacho kiomba kwenu ni kitu kimoja tuu, naomba baraka zenu na support yenu, ya will ili, kuniwezesha kutupa karata yangu tena kwenye hili jambo langu.
  14. Naomba kwa sasa nisilitaje hilo jambo, na nakuomba na wewe hata kama utalihisi, nakuomba usitaje, please!. Kuna sababu.
  15. Baada ya hiyo fursa kutangazwa, mimi nimejipima uwezo wangu, ability yangu na capabilities nilizo nazo, nikakuona ninaweza, nina uwezo nalo in terms of ability, na capabilities niko capable ninachohitaji ni just moral support.
  16. Ninachohitaji kwenu ni kitu kimoja tuu, moral support Kwa kuniunga mkono kwa sala zenu, kupitia a collective bargaining "powers of will" za wana jf wote collectively kuniwezesha by goodwill zenu. Just wish me good, hiyo will power yako ina nguvu kuliko kitu kingine chochote!. Naombeni tutumie powers of positivism na affirmative kuniwezesha niweze.
  17. Wale msio nikubali au kukubaliana na mimi, naowamba sana sana sana, na niko chini ya miguu yenu, mnisamehe kwa yote ya nyuma na kunisaidia kwa kutochangia negative kwenye uzi huu, kama mmeshindwa kabisa kunisamehe, basi please just ignore me kwa kutochangia chochote kwenye bandiko hili ili msilete negative powers nikaja kuambulia kura moja tena!. Please nihurumieni!.
  18. Baada ya kujipima na kujiona nina uwezo, ability na capabilities, lakini natakiwa kujengewa uwezo zaidi in terms of capacity, niwe capacited ili niwe capable, niwezeshwe niweze, hata nikihitajika kunyoosha mkono mahali popote parefu, niwe na uwezo wa kuunyoosha huo mkono, urefuke na kufika popote. Hivyo nawaombeni mniunge mkono kwa hili kupitia moral support yenu
  19. Ewe Mwana jf mwenzangu, tusahau tofauti zetu, nakuomba uniunge mkono kwenye hili, together we can!.
  20. Naamini nitayaweza yote katika YEYE anitiaye nguvu!. Mungu Nisaidie!. Sema Amen!. Hiyo Amen yako is all that I need!. Natanguliza shukrani na ubarikiwe sana!
Paskali.
HUFAI KABSAAA
 
Nakuombea na binafsi sina kinyongo nawe kwakuwa tumeishi kwa kuheshimiana mno na kupeana sitara pale palipokuwa na mitazamo tofauti..!

Kila jambo huanzia rohoni bila kujali asili yake.. Tokeo lolote la kimwili asili yake ni rohoni..! Hili jambo utakalo kama una asili nalo BASI LITAKUWA .. Lakini kama ni 'passive' kutokana na jinsi ulivyoeleza hapo basi kuna shida kidogo.. Nachelea kusema unaweza kuangua pua

Natambua unatambua kwa hakika kwa kipindi cha 2015 mpaka sasa ama kwa kujua au kwa kutojua ulijijengea nguvu hasi kubwa sana...lakini haya si sehemu yake sasa kwakuwa umejinyenyekesha, kujishusha kabisa na kuomba radhi... Ambaye hatakusamehe ajitambulishe na kutuonesha ukamilifu wake! Kwenye hili huna mawaa tena ila kuna hiki kitu kinaitwa KARMA!

Sala na maombezi yetu vitakuwa nawe lakini vinaweza kukosa nguvu chanya ya uchaji wa kiroho kulingana na muktadha wake! Kwamba kama ni nafasi ya kisiasa basi baraka nyingi hukumbana na nguvu za kiza
Kuna nguvu hasi nyingine pia ambayo inaweza kuwa kigingi cha kukwamisha ndoto zako.. Nacho ni chama cha siasa utakachotumia kuombea nafasi firikirika.. Kimejaa tuhuma, ubaya na uchafu wa kila aina... Kimeumiza na kutesa wengi, kimedhulumu na kufanya kila aina ya hila ili kiwepo mahali kipo..! Baraka huwa hazikai mahali kama hapo!

Kwahiyo bro pamoja na maombi yetu ambayo utayapata kwa wingi sana lakini una hizo negative energy tatu zinazokukabilli
. Background yako hasa 2015..
.Nafasi ya kisiasa unayoomba
. Chama cha siasa utakachopitia (as per rumors)
Barikiwa sana. Kitakachomtesa Paschal Mayala ni "KARMA"
 
Lakini yeye ameomba zaidi asamehewe kama aliwakwaza watu na pia aombewe Dua ili jambo lake litimie !! Hapo surely hakuna ubaya wowote alioufanya !! Ni mambo ya ya kiungwana kabisa
Kamkosea nani mzee?

Dua zimpeleke wapi?Niache kumuombea dua bibi yangu wa 105years nije nimuombee yeye jitu zima?

Yaani wanaostahili dua wamejaa tele lenyewe baba zima lenye nguvu liombewe halina mdomo?

Hii yote wala sio dua wala "kusamehewa" wala nini ni narcissism yakutaka kila kitu ki-revolve around him,just him na kutafuta huruma ya kura

Anakuja kutuomba sisi ndio wapiga kura?Wakati wapiga kura ni watu wengine kabisa...

This nigga is so obsessed with attention seeking....yaani uzi hauna uhusiano na JF members kabisa ila kaulazimisha kuletea JF members attention of his own uongozi seeking problems
 
Back
Top Bottom