Chuma,
Zitto JF ni nyumbani kwake inabidi kila mara atupe mchango wake ktk hoja tofauti
Jama, napenda kuuliza, members hawa wametowekea wapi? Kuna anayejua...
--Mchongoma
--KadaMpinzani
--Pangupakavu
--AmazingFriend
--
Ila Nahisi kadi amerudi kwa jina lingine,Kuna baadhi ya maneno yanatumiwa na member mmoja hapa na ukiangalia kwa makini utajua ni kada ttu..
Ila kada tumekukumbuka
Gembe, inawezekana kabisa... ila napenda kukuhakikishia kuwa nami nimechunguza maneno fulani hivi na flow ya kada, bado nasita kujua kama mtu huyo ndiye yeye... ila speed yake ya kutype na kuwepo kwake mtandaoni kunafanana sana na kada...
ama kweli, saa nyingine hata kama mtu alikuwa ana kukera mara kadhaa, yale mazoea ya kuwepo kwake tu yakitoweka... yaani mtu una m-miss ile mbaya...
Jamani mugongomugongo je? Au kafungiwa?
Hapana, huyu yupo hapa kwa jina tofauti. Style ya mwandiko wake ndiyo ilinifanya nijue ni yeye. Mtu makini sana hivi sasa, character aliyoitumia kama mugongomugongo kaiacha, ila makali yake katika kuchambua bado yale yale.
Steve D,
Mgongowamgongo- tulimzoea bwana asibadili jina! Yeye ni kwa nini akabadili jina?
Je jina jipya ni lipi?
Katika kuheshimu sheria za JF, siwezi kumtaja hapa, nitamstahi. Hata kama hivyo kama unahamu sana ya kumjua ni nani, nina tricks nyingi za kumgundua mtu... ukihitaji nitakupa moja (naweza ku charge fee lakini 🙂!!).
By the way, kuna Mugongomugongo na kuna mgongomgongo, sasa huyo uliyemtaja kama Mgongowamgongo, mimi kwa kweli simjui, sina uhakika kama ulimaanisha yule mugongomugongo aliye mtaja Judy.
SteveD.
Kuna mmoja alikuwa Marekani kafariki mwezi huu, hizi habari nilizisoma hapa kwa kuchelewa sababu ya shughuli zangu kuwa nyingi. Mwenyezi Mungu amlaze pema, amin.
Yupi huyo?