Earthmover
JF-Expert Member
- Sep 28, 2012
- 23,030
- 20,522
wala haijachakachua....
Ni kitu halisi alichoongea mwenyekiti na aliwaambia waandishi wakaandike... nyie ndo mnahangaika kutaka kusema eti TBC wamekanusha ili muoneshe kwamba tunajutia kauli hiyo..
soma hiyo usipate tabu...
"Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge," alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa Nec.
Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
"Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na mwache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake," alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.
"Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi,"alisema.
haturudi nyuma kuwa na unyonge... unyonge basi
.....
....
......TAFAKARI !!!!