Wewe unatapatapa sana mkuu,katika mchango wangu ulionijibu hakuna sehemu nimesema CHADEMA ni chama cha kidini , nashangaa unajizogoa mwenyewe kwa vile unajua kabisa ninyi ni wadini. Halafu ujue kuwa Katiba Mpya na elimu bure hazikuwa agenda zilizoanzishwa na CHADEMA, wapo watu kama akina MTIKILA, chama cha CUF na hata wabunge wa CCM walikuwa na hoja hizo tangu hata kabla haijafahamika kama KUNA SIKU CHADEMA kitakuja kuoenakana kwenye ramani ya vyama vya siasa nchini.
Naomba na mimi nikupe mfano mmoja tu wa namna ambavyo CHADEMA wanapenda kujichomeka kwenye hoja za wengine.
Miaka yote CUF waliwatuhumu CHADEMA kuwa wanashrikiana na chama cha CONSERVATIVE cha kule uingireza, chama ambacho ni wazi kinaunga mkono USHOGA. Hoja hii ya CUF imewatesa sana CHADEMA mpaka WENJE alipokuwa na udaku wake kuwa CUF nao wanashirikiana na chama cha ushoga, basi wakalibebea bango ili mradi tu wajinasue kuwa MASHOGA, lakini ukweli utaendelea kubaki pale pale kuwa CHADEMA wanashirikiana na mashoga wa Uingereza na hata juzi JK aliulizwa kuhusu msimamo wake juu ya ushoga na jibu lake likawa ni la herufi mbili tu kubwa yaani "NO"
CHADEMA wadandiaji wa hoja na sera za vyama vingine, ndicho chama kichanga kabisa ukilinganisha na CCM, CUF na NCCR-Mageuzi, hawa ni wazuri sana wa ku-copy na ku-paste.