Imagine, kuna haya mabasi
Ester Luxury
Tilisho
Happy Nation
Sauli
New Force
Arusha Express
Shabiby
Abood
Machame Express
Kapricon
Kilimanjaro Express
Dar Express
Zube
Saratoga
Mgamba
Kimbinyiko
Abc
Ally's
Saibaba
etc etc
Malori ndiyo usiseme.
Unakuta mtu ana basi 10, 20 au 60. Basi moja bei yake ni Milion 300, 400 hadi 500. Jamaa wanapata wapi hela aisee?
Binafsi nimetoka nyumbani na kuanza kutafuta maisha kwa kila hali mjini na mashambani toka mwaka 1996 ,mpaka leo nimepita kwingi sana, nimelima, nimevua samaki, nimetegeneza magari,nimechimba dhahabu na Almasi, nimeendesha magari ya mashirika, lakini mpaka leo maisha yangu ni ya kawaida sana na Kwa namna nyingine naweza kusema ni magumu tu
Kuna kazi ngumu sana kukusanya pesa kiasi cha Milion moja kabla hujapata shida ya Milion mbili, yaani pesa haikusanyiki, tunaishia kujenga nyumba ya vyumba vitatu vya kuishi na kula na huduma ndogo ndogo za kawaida
Nasema ya kwamba, pesa ina mambo makubwa mawili tu
1. PESA ya kuikuta tu labda kutoka Kwa wazazi au ndugu
2. PESA ya mtu msomi aliye bahatika kufanya kazi za mashirika ya kimataifa tena ngazi za juu zenye mishahara ya Milion 40 na kuendelea, na huyo nae afanye kazi zaidi ya miaka kumi labda
Nje na hivyo, Kuna ukwapuzi na uchawi japo huo uchawi sina hakika sana lakini nadhani wakwapuzi ndiyo wengi
Unaikusanyaje billion 1 tu katika maisha haya ya kiAfrica hususani Tanzania?
Iko Siri tusiyoijua kwa watu wenye PESA