Wamiliki wa Mabasi na Daladala, kwani Mchawi wenu ni nani, mbona mnatutusi abiria?

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Jana jioni kupitia Radio one nimemsikia Muwakilishi au Kiongozi wa Wamiliki wa Usafirishaji Dar akiongea kwa jazba sana kulalamikia nauli kutokupanda kwa namna ambavyo wangetamani.

Bwana huyu alienda mbali zaidi na kuwalaumu sana LATRA kuwa ndio wanaowaangamiza wao Wamiliki wa Vyombo vya usafiri.

Ni kana kwamba yeye angepewa Mamlaka basi angetamani nauli badala ya mia nne iwe hata elfu tano kwa town trip, kwa hasira za yule Bwana zimenipa maswali mengi sana kichwani,

Hii ikanikumbusha kauli ya kale iliyokuwa inasema "Ubepari ni unyama", kwa maneno mengine Tajiri ni Mnyama asiyemjali kabisa asiye nacho.

Mwalimu aliupigania Ujamaa ili Watu tusisahau Utu, ikawa ngumu kwa sababu Binaadamu wengi hatuko tayari kutanguliza utu dhidi ya mali..na mpaka leo wapo wanaotukana na kukejeli juhudi zile.

Hivi wao wanapolalamikia kupata zaidi vipi yule Mchoma mahindi au Kibarua Mjenzi yeye nani anamuongezea pesa ili amudu hizo nauli anazozitamani?.

Lawama alizokuwa anatoa kwa LATRA ni kama anawaambia "nyie ndio Mnawakingia kifua hawa Masikini tuacheni tuwakamue tutakavyo washenzi hawa".....kweli Bepari ni Mnyama.

Wakati mnatetea maslahi yenu msiwasahau Wananchi wenzenu, maana huwa mnadhani mnapambana na kina Bw January lakini kiuhalisia mnapamba na Wananchi wenzenu Wachovu, kina January wala hawajui Daladala ni nini.

Mnachokipigania kwa lugha kali na kejeli zote mjue mnawafanyia Mabinti walioajariwa kwa Mama lishe wanaolipwa elfu tatu au nne kwa siku, hao ndio mnawasuta na kuwaambia kuwa watumie shilingi elfu mbili kwa usafiri wa kila siku kufika na kutoka kazini kwake abakiwe na elfu moja tu ndio alipie chumba anachoishi na mahitaji yake mengine pamoja na ya Mtoto wake aliyetelekezewa na Mzazi Mwenzake?..au kwa mawazo yenu mafuta yakipanda bei na huyu Binti au yule Fundi Viatu nao wanaongeza mapato?.

Sitaki kubeza juhudi zenu kuhakikisha mnapata mapato yanayoweza kuwafanya muendeshe Biashara hiyo ya usafirishaji lakini hilo haliwatoi kwenye kuwajibika kwa Ndugu zenu kwa kisingizio chochote kile mkijifanya mnapambana na Taasisi za Kiserikali lakini ukweli ni kwamba mnapambana na Wananchi wasionacho.

Unapotoa mfano wa Kampuni za Mabasi zilizokufa kwa sababu ya nauli ndogo, hebu njoo huku kwetu nikuoneshe Watu waliofungua vibanda vya kukaanga chipsi na wakashindwa wakafunga, lakini Chipsi si bado zinachomwa na wengine?.

Unaposema ninyi huwa hamgomi bali ni Madereva ndio wanagoma, kweli haya ni maneno ya kuwaambia wenye akili timamu au uliwalenga Watoto?.

Mapambano yenu na Mamlaka yasiwasahaulishe kuwa mna dili na Wananchi wa aina gani, tumieni approach inayofaa kupambana na Mamlaka na si kuwatusi, kuwakebehi na kuwasuta Abiria...tukae upande mmoja msijitoe kutaka Mamlaka ziwajali nyie na kuwapuuza Wananchi.
 
Mkuu,

Kila kitu kimepanda bei, na wala havijasubiri hiyo tarehe 14 Mei.

Waacheni wapandishe with immediate effect, kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake.

Kazi iendelee.
 
Miliki na ww chombo cha moto harafu uone kama inatosha kuendeshea biashara hiyo
 
Jana jioni kupitia Radio one nimemsikia Muwakilishi au Kiongozi wa Wamiliki wa Usafirishaji Dar akiongea kwa jazba sana kulalamikia nauli kutokupanda kwa namna ambavyo wangetamani.

Bwana huyu alienda mbali zaidi na kuwalaumu sana LATRA kuwa ndio wanaowaangamiza wao Wamiliki wa Vyombo vya usafiri.

Ni kana kwamba yeye angepewa Mamlaka basi angetamani nauli badala ya mia nne iwe hata elfu tano kwa town trip, kwa hasira za yule Bwana zimenipa maswali mengi sana kichwani,

Hii ikanikumbusha kauli ya kale iliyokuwa inasema "Ubepari ni unyama", kwa maneno mengine Tajiri ni Mnyama asiyemjali kabisa wasio nacho.

Mwalimu aliupigania Ujamaa ili Watu tusisahau Utu, ikawa ngumu kwa sababu wengi hatuko tayari kutanguliza utu dhidi ya mali..na mpaka leo wapo wanaotukana na kukejeli juhudi zile.

Hivi wao wanapolalamikia kupata zaidi vipi yule Mchoma mahindi au Kibarua Mjenzi yeye nani anamuongezea pesa ili amudu hizo nauli anazozitamani?.

Lawama alizokuwa anatoa kwa LATRA ni kama anawaambia "nyie ndio Mnawakingia kifua hawa Masikini tuacheni tuwakamue tutakavyo washenzi hawa".....kweli Bepari ni Mnyama.

Wakati mnatetea maslahi yenu msiwasahau Wananchi wenzenu, maana mnadhani mnapambana na kina Bw January lakini kiuhalisia mnapamba na Wananchi wenzenu Wachovu maana hao kina January wala hawajui Daladala ni nini.

Mnachokipigania kwa lugha kali na kejeli zote mjue mnawafanyia Mabinti waliojariwa kwa Mama lishe wanolipwa elfu tatu au nne kwa siku, hao ndio mnawasuta na kuwaambia kuwa watumie shilingi elfu mbili kwa usafiri wa kila siku kufika na kutoka kazini kwake abakiwe na elfu moja tu ndio alipie chumba anachoishi na mahitaji yake mengine pamoja na ya Mtoto wake aliyetelekezewa na Mzazi Mwenzake?..au kwa mawazo yenu mafuta yakipanda bei na Huyu Binti au yule Fundi Viatu nae anaongeza mapato?.

Sitaki kubeza juhudi zenu kuhakikisha mnapata mapato yanayoweza kuwafanya muendeshe Biashara hiyo ya usafirishaji lakini hilo haliwatoi kwenye kuwajibika kwa Ndugu zenu kwa kisingizio chochote kile mkijifanya mnapambana na Taasisi za Kiserikali lakini ukweli ni kwamba mnapambana na Wananchi wasionacho.

Unapotoa mfano wa Kampuni za Mabasi zilizokufa kwa sababu ya nauli ndogo, hebu njoo huku kwetu nikuoneshe Watu waliofungua vibanda vya kukaanga chipsi na wakashindwa wakafunga, lakini Chipsi si bado zinachomwa na wengine?.

Unaposema ninyi huwa hamgomi bali ni Madereva ndio wanagoma, kweli haya ni maneno ya kuwaambia wenye akili timamu au uliwalenga Watoto?.

Mapambano yenu na Mamlaka yasiwasahaulishe kuwa mna dili na Wananchi wa aina gani, tumieni approach inayofaa kupambana na Mamlaka na si kuwatusi, kuwakebehi na kuwasuta Abiria...tukae upande mmoja msijitoe kutaka Mamlaka ziwajali nyie na kuwapuuza Wananchi.
Mafuta kabla hayajashushwa kwenye meli, mnakimbilia kupandisha bei, wamiliki wa vyombo vya uchukuzi wakijitutumua kidogo tu kelele zinajaa, hivi wao wanatumia maji?
 
Hao wamiliki wa vyombo vya usafiri inapaswa sisi wananchi tusafunze adabu yaani tunakaa ndani siku mbili nzima hakuna kutoka tuone kama watapanda wenyewe hayo mavyuma yao.
 
Hao wamiliki wa vyombo vya usafiri inapaswa sisi wananchi tusafunze adabu yaani tunakaa ndani siku mbili nzima hakuna kutoka tuone kama watapanda wenyewe hayo mavyuma yao.
Nadhani pia ipo haja ya kurudi kwenye matumizi ya Baiskeli na Mikokoteni ya kukokotwa na Wanyama iliyoboreshwa.

Ifike mahali kupatikane mbadala wa hivi vyombo vya kusafiria vinavyotegemea nishati zisizo na utulivu wa bei.
 
Back
Top Bottom