Nani anazipa jeuri Daladala za Moshi Mjini kutoka Kikavu Chini hadi Longoi?

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Umbali wa kutoka Moshi Mjini hadi Kikavu chini ni Kilomita 11 tu, nauli ya awali ilikuwa ni Shilingi 600 kabla ya ongezeko la hivi karibuni iliyofanya nauli ya eneo hilo kuwa ni Shilingi 700.

Pamoja na mabadiliko hayo, Daladala zinazoenda njia hiyo hazijawahi kuwatoza kiasi hicho cha nauli abiria wake kama ilitolewa maelekezo na Mamlaka ya LATRA, badala yake Daladala zinatoza Shilingi 1,500 kwa mtu mmoja na hawatoi tiketi.

Agosti 2023 tulifikisha malalamiko haya kwenye mamlaka husika, LATRA walifika na kutoza faini kwa baadhi ya magari kwa kuzidisha nauli, kutoandika kiwango cha nauli ubavuni na kuwazidishia abiria nauli pamoja na wahusika wa Daladala kutokuvaa sare.

Hata hivyo, suala hilo halijawa dawa ya kuwafanya waache kuwatoza abiria nauli kubwa tofauti na maelekezo ya LATRA.

Kinachoendelea sasa ni kilekile ambcho Wananchi wamekikataa na wamekuwa wakikipigia kelele muda mrefu, ukiwauliza sababu ya kupandisha nauli wanakwambia tutaelewana na LATRA wakija kutukagua.

Jambo hili linatusikitisha sana na kwa hakika Wananchi tunadhulumiwa, tunaomba LATRA wawe wakali na wawe na meno, kinachoendelea hapa kwa hizi Daladala ni kama vile wanatunishiana ubavu na Serikali na tunaoumia ni Wananchi wa hali ya chini.
 
Hii nchi siasa imekuwa nyingi sana. Amini nakwambia hilo unaloliona huko lipo sehemu nyingi sana nchi hii.

Wafanyakazi wa serekali wanafanya kazi kwa mazoea. Inakuwaje wenye daladala wachache waizidi nguvu serekali? Watu hawana woga yaani.

Kamata daladala chache fungia milele. Achaneni na mafaini yasiyo na tija! Wenzenu wanachukulia fine kama bei wanawanunua
 
Back
Top Bottom