Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

Ulinzi wa GPS umenivutia je ni effective maeneo yote mkuu au kwa mjini tuu
Mimi natumia mkuu, inafanya kazi maeneo yote ambapo mtandao wa simu unashika. GPS Tracking zinatumia simcard, kwa hiyo ni juu yako kuchagua mtandao wenye coverage kubwa hadi vijijini. Mi natumia halotel kwa ajili ya coverage yake vijijini. Nitafute nikufungie, kwenye bajaji yako au pikpiki yako, bei ni laki na nusu hakuna malipo ya kila mwezi ni ww kununua kifurushi cha sms cha buku na kuweka salio la buku unatumia mwezi mzima. Karibu
 
Asante Jf. Nazidi kujifunza. Kiukweli Nina itamani hii biashara,na I believe ipo siku nitafanikiwa.
Mkuu usingoje sana, anza. Mimi nilianza na pikipiki moja ya mkataba baada ya kusoma uzi huu, now nina Bajaji kadhaa. Hakuna kusimama, maisha yanaendelea.
 
Uzi mzuri sana huu na mimi ni mmoja wapo wa wamiliki wa boxer tatu na bajaji moja,,
Na Kwa week kwa makubaliano yetu ni 60,000Tsh ambayo kwa siku 6 ni 10,000 afu siku moja ya dereva ila mi sina mkataba na pikipiki napiga tu ya kawaida na bajaji ni 105,000Tsh kwa week na kwa siku ni 15,000 ila kuna changamoto zake ambazo ni ;

1.matengenezo ya hapa na pale kama vifaa kuharibika sanasana ni spoketi na kubadilisha tairi ,,

2.Mvua kunyesha ambapo zikinyesha huharibu sana mahesabu yetu ya week inabidi madereva waniombe niongeze tena siku moja au mbili mbele ya kupokea hesabu,,

3.kukamatwa na polisi kwa makosa ya wrong parking na bima ambapo utatakiwa kutoa 30,000Tsh kuikomboa pikipiki yako kituoni na hii huku kwetu luguruni na mbezi mwisho hutokea ila sio mara kwa mara.

4.Na hii ni upepo wa abiria kuwa wachache pindi chuo kikifungwa ambapo sisi huku hutegemea sana wanafunzi wa chuo kwa ajili ya usafiri kwa hiyo inabidi dereva aunganishe week mbili ili akujumlishie hesabu yako yote ya week mbili.

5.Matatizo binafsi ya dereva anaweza akakwambia yeye au ndugu ama mzazi anaumwa kwamba ela katumia kwa matibabu au kalipia chumba chake cha kupanga inabidi tu uvumilie week mbili ili akuunganishie ela yako yote.

Angalizo kwa hizi changamoto usipokuwa mvumilivu kwa dereva wako mnaweza shindwana kwa kweli inahitaji uvumilivu wa hali ya juu maana matatizo yapo kwetu sote na inabidi wote tusikilizane...!!!!!!!
Umenena sawa mkuu. Usipokuwa mvumilivu kwa dereva utabadili madereva kila siku na mwisho wa siku utapata madereva watakaokuharibia chombo chako. Mimi pia huwa napata changamoto kama hizo kwenye bajaji zangu but mambo yanaenda kibishi hivohivo. Gharama za uendeshaji hizo hazikosekani mkuu, mimi kwa bajaji so far Operation Cost Ratio ina range 21%- 30%. Ningependa isizidi 25%.
 
Katika biashara ya kivivu ambayo haina faida ni boda boda....

Na ninawashangaa saana wanaofanya iyo biashara km sehemu ya kutengenezea pesa....

Mwelewa katika mambo ya pesa hawez fanya iyo boda trade...

Unanunua pikipiki 2m alafu unapata buku 7 per day... it means mpaka miezi kumi baadae ndio uanze kupata buku 7 per day km faida...

Na izo hesabu hapo haujakutana na majanga ivyo........

Then bado trafic n.k

Sasa je.... kama iyo 2m ungeiweka kwenye biashara ingine... ina maana kwa miezi kumi ungepata zaid ya iyo buku 7 ya boda....

Tatizo nyie wana boda boda munaangalia saaana kinachoingia kuliko kilichotoka...

Income-Starting package=profit
Nakubaliana nawewe lkn binafsi naona watu hata wakianza na biashara hiyo sio mbaya kwasababu ndio watu wanajifunza biashara. Wakishapata uzoefu kwenye biashara hiyo watakuwa na nafasi nzuri ya kuhamia biashara nyingine. Pia biashara zinazolipa zaidi zinahitaji menejimenti ya karibu sana, ukifeli hapo ndo umefeli business, sioni tatizo kwa mtu kuanza na biashara hii mkuu hasa kwa mtu ambaye hana muda wa kusimamia biashara.
 
Uzi mzuri sana huu na mimi ni mmoja wapo wa wamiliki wa boxer tatu na bajaji moja,,
Na Kwa week kwa makubaliano yetu ni 60,000Tsh ambayo kwa siku 6 ni 10,000 afu siku moja ya dereva ila mi sina mkataba na pikipiki napiga tu ya kawaida na bajaji ni 105,000Tsh kwa week na kwa siku ni 15,000 ila kuna changamoto zake ambazo ni ;

1.matengenezo ya hapa na pale kama vifaa kuharibika sanasana ni spoketi na kubadilisha tairi ,,

2.Mvua kunyesha ambapo zikinyesha huharibu sana mahesabu yetu ya week inabidi madereva waniombe niongeze tena siku moja au mbili mbele ya kupokea hesabu,,

3.kukamatwa na polisi kwa makosa ya wrong parking na bima ambapo utatakiwa kutoa 30,000Tsh kuikomboa pikipiki yako kituoni na hii huku kwetu luguruni na mbezi mwisho hutokea ila sio mara kwa mara.

4.Na hii ni upepo wa abiria kuwa wachache pindi chuo kikifungwa ambapo sisi huku hutegemea sana wanafunzi wa chuo kwa ajili ya usafiri kwa hiyo inabidi dereva aunganishe week mbili ili akujumlishie hesabu yako yote ya week mbili.

5.Matatizo binafsi ya dereva anaweza akakwambia yeye au ndugu ama mzazi anaumwa kwamba ela katumia kwa matibabu au kalipia chumba chake cha kupanga inabidi tu uvumilie week mbili ili akuunganishie ela yako yote.

Angalizo kwa hizi changamoto usipokuwa mvumilivu kwa dereva wako mnaweza shindwana kwa kweli inahitaji uvumilivu wa hali ya juu maana matatizo yapo kwetu sote na inabidi wote tusikilizane...!!!!!!!
Angalizo lingine:

Jaribu kuwa mkali kwa dereva wako pale siku ya kutuma ela inapowadia madereva wengine huwa wanafanya mambo ya hovyo wakijua mabosi zao hawana noma,,
Limenitokea wiki hii nimechachamaa hadi ela zikatumwa..!!!!!
 
Mkuu usingoje sana, anza. Mimi nilianza na pikipiki moja ya mkataba baada ya kusoma uzi huu, now nina Bajaji kadhaa. Hakuna kusimama, maisha yanaendelea.
Mtaji nduvu. Sijafikia kuwa na pesa ya kununua bodaboda. Kwa sasa niko na biashara zangu ndogo tu kiasi, nikiweza kutoka huko ndio nitaweza hata kununua bodaboda
 
Nilijua hujaanza biashara kabisa Mkuu. Hapo hapo kwenye biashara ndogo ndogo komaa, hata mbuyu ulianza kama mchicha. Watu wengi wanadhani mtaji ni kuwa na milioni 10 lkn ukweli ni kuwa hata laki moja ni mtaji.
 
Angalizo lingine:

Jaribu kuwa mkali kwa dereva wako pale siku ya kutuma ela inapowadia madereva wengine huwa wanafanya mambo ya hovyo wakijua mabosi zao hawana noma,,
Limenitokea wiki hii nimechachamaa hadi ela zikatumwa..!!!!!
Naam ni kweli mkuu, madereva wakati mwingine ni waongo sana. Anaweza kwambia hiki kimeharibika nikanunua kumbe mwongo tu au leo sijafanya kazi kumbe kapiga kazi sana tu. Mimi saivi nina mbinu za kuwabana madereva akiniambia kabadili kifaa namwambia nipe ulichotoa pamoja na risiti. Akisema hajafanya kazi, mi naangalia kwenye gps tracking platform mizunguko aliyofanya.
 
Nakubaliana nawewe lkn binafsi naona watu hata wakianza na biashara hiyo sio mbaya kwasababu ndio watu wanajifunza biashara. Wakishapata uzoefu kwenye biashara hiyo watakuwa na nafasi nzuri ya kuhamia biashara nyingine. Pia biashara zinazolipa zaidi zinahitaji menejimenti ya karibu sana, ukifeli hapo ndo umefeli business, sioni tatizo kwa mtu kuanza na biashara hii mkuu hasa kwa mtu ambaye hana muda wa kusimamia biashara.
True aisee..... kwa wakongwe hawawez fanya
 
Biashara ya bodaboda hailipi sana labda uwe nazo nyingi ndio utaenjoy pesa yake. Kwa mtu ambae hana muda wa usimamizi hii biashara inamfaa, Biashara nyingine zinazolipa zaidi zipo nyingi lakini zinahitaji usimamizi mkubwa sana vinginevyo hupati kitu. Mimi nilishajaribu kilimo ambacho wengi wanasifu kinalipa lkn nilitupa 2M zangu kwasababu ya usimamizi dhaifu. Nitarudia shamba nikiwa na wasaa wa usimamizi au laa labda niajiri farm manager but kwasasa sina mtaji wa kuajiri farm manager
 
Katika biashara ya kivivu ambayo haina faida ni boda boda....

Na ninawashangaa saana wanaofanya iyo biashara km sehemu ya kutengenezea pesa....

Mwelewa katika mambo ya pesa hawez fanya iyo boda trade...

Unanunua pikipiki 2m alafu unapata buku 7 per day... it means mpaka miezi kumi baadae ndio uanze kupata buku 7 per day km faida...

Na izo hesabu hapo haujakutana na majanga ivyo........

Then bado trafic n.k

Sasa je.... kama iyo 2m ungeiweka kwenye biashara ingine... ina maana kwa miezi kumi ungepata zaid ya iyo buku 7 ya boda....

Tatizo nyie wana boda boda munaangalia saaana kinachoingia kuliko kilichotoka...

Income-Starting package=profit

Mkuu biashara gani inayotaka mtaji wa milioni 2 ambayo inalipa vizuri ndani ya miezi 10.
 
Tarakilishi
Mimi nina gps tracker kunifungia utanifungia kwa tsh ngapi kwenye pikipiki? Kifaa ninacho
 
Back
Top Bottom