Aisee na wewe ndio umemalizia kisomi namna hii,na ndio Mwenye Uelewa wa Mambo ya Pesa.
Sasa mie nimewekeza Almost 49m kwenye vyombo vya usafiri,na ingekuwa hailipi basi ningekuwa miaka Mingi nimeacha.
Kuna Mdada wa Kichanga ana Bodaboda 22,na bado anataka kuongeza.Sasa sijajua uelewa wako upoje.
Kwanza jua kabisa 2m sio pesa kivile unavyoifikiria wewe kwamba itafanya makuubwa.
Maana hata sijui hesabu unaipiga vipi.
Jua kwamba hata Nchi ikinunua Boeing au ndege ya Airbus basi jua wana miaka si chini ya Mitano ndio pesa irudi.Sasa itakuwa bodaboda?
Ila sikulaumu,maana ndio uelewa wako,sie tunaofanya biashara na tunaotumia Changamoto kuzigeuza kuwa fursa basi ndio maana tumekomaa.
Na ndio maana Miaka hii Watoto wa kike wanatumia sana fursa za kupambana kibiashara huku wakiume wakiwa wapo wapo tuu,waoga
Tuulize sie tunaofanya hii biashara kitambo,mtu unaibiwa bodaboda mpyaa,ila unapambana mpaka unaunua nyingine,sasa naona wewe ukiibiwa unakufa kabisaaa.
Kwa kukudokeza tu mkuu,Zanzibar Bodaboda zilikuwa hakuna ila zimeibuka kwa kasi ndani ya miaka hii Miwili,na nilianza kuwekeza Dar ila baada ya Zanzibar kuunga nikawekeza na huku.
Tatizo ni kwamba,mtu unataka faida kubwa na haraka wakati pesa yenye ndogo tu 2m.
Maisha sio rahisi kama unavyofikiria
Assignment ndogo tu,hembu toa biashara ambayo inafaida zaidi ya Bodaboda kwa Capital ya 2m.
Umekurupuka kujibu kama ulivyokurupuka kuisoma iyo comment....
Sio kwamba ciijui au chawahi fanya iyo biashara....
Iyo ndio biashara yangu ya tatu kujaribu.... nimeifanya nikayaona ninayokuambia.... we kama unaamini endelea kuiamin... kila mtu ana akili zake.... na mimi nimeandika ninachokijua ila cijakuamulia kuiacha au kuifanya... ni faida yako wewe na mmeo/mkeo.
Kiuchumi.... eti unafananisha boeing na boda... kwamba zote zinachelewa kurudisha mtaji.
Hivi 2m alafu ukae mwaka mmoja wenye changamoto kibao na migogoro.... ndio uanze pata faida....
Tena ni elfu 7 per day.... bado unajiira mfanya biashara mkongwe mwenye uelewa....
Umeuliza biashara gani ya 2m.
Nakupa mifano rafu tu ukitaka serious utaongea...
Ukifuga kuku wa kienyej. Utaanza pata pesa baada ya miez mitatu laki moja elf 50 kila day... baadae hadi laki.
2m inafungua vibanda vya chips vi4 vizuuri.... ni elfu 5 per day teeena kama sehemu nzuri iyo ni 10 per day.
It means vi4 ni elf 20 hadi 40 per day na no usumbufu.
Ukiamua kulima eg. Mahindi.
Iyo 2m ni heka 15 ambazo zitatoa mahindi gunia 200... ukiziuza unapata million 20 ndani ya miez 7 tu.
Ziko nyiiingi saaaana.... sema we ni mvivu wa kufikiri na muoga wa kujaribu... na ndio maaana unaamini katika biashara iliyokutoa tu hutaki kuongeza maarifa tu.
Na ndio maaana miaka mingi now bado unajongea taratibu tu...
We komaa katika mawazo yako... utakapofikia uwezo wa kuona kama mimi utabadirika tu.
Nilishafikia wakati namiliki boda 5 na bado nikaona nimezika.... pesa kwenye vyuma....
Last year nimezika kwenye ardhi baada ya kuuza boda... hapa nina stock ya gunia 300 za mahindi nawait soko likae poa nagonga 30m.
We komaa na boda jifanyd jiwe hutak kubadirika zaid ya kukosoa tu...
Muda utakupa fundisho mdugu.
Sent from "La -Vista"