Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

Angalizo jingine muhim.
Nikwamba tafuta kwanza Driver then ndio ununue chombo.
Sio kila Driver anapenda Boxer,wapo wengine wanakuambia wanata Sunlg, Tvs king,nk
Mie mwanzo nilianza na Boxers ni wakati ndio zilikuwa gumzo la jiji.Baada baadhi ya driver akaniambia yeye anataka Sunlg.

Unajua faida ya kumpa Driver pikipiki anayoipenda ni sawa na wewe kuoa mke unaempenda.Tena wengine mpaka rangi anachagua,maana miwe kwenye boxer kuna alietaka nyeusi,mwengine nyekundu.Sasa akiipata ana enjoy kweny unamuona kabisaa mwenye furaha ya ajabu sana.Ni tofauti nayule amabae unamuambia unapikipiki nayeye kwanjaa anakubali tu.
Hili sio lazima saaaana,ila ni kama ziada tu,ukiwanazo zaidi ya moja ndio unaweza ku experience hiki kitu.
 
Mie ni Mmiliki.
Naungana na mleta hoja hapo juu,hii biashara lazima uwe na akili ya kuona mbali,sio hizi za kusema akupe elfu kumi then iwe yake.So,what next,inaamana wewe kila mwaka unatakiwa kubadilisha Driver mpya?hii sio akili ya kibiashara kabisaaa,na waoga wa biashara ndio wanaitumia.
Kama unakimbia changamoto za bodaboda basi sikufichi kwenye Gari ndio usisogee kabisaa,utakuafa,nakuambia kwa uzoefu

Mie hutumia hivi:-
-Hesabu yangu mie ni kwa Wiki Tsh:50,000
-Na kila baada ya miezi sita tu nauza Chombo nanunua kingine,na huwa nanunua kwanza kisha nampa Driver halafu ndio nakiuza ili asikose kazi hata siku moja.Unless kuwe na jambo katikati.
Na kwenye kuuza huwa baada ya kuuza nampa Driver kama zawadi ya pesa kwa kutunza Chombo vizuri in percentage,so hii hufanya na wao kuwa makini na chombo
-Driver akiwa na Msiba au ugonjwa wowote katika familia au Msiba wa Driver mwenzao,basi huleta pikipiki nyumbani au mdogo wangu anaenda kuichukua,na akipona anakuja kuichukua,hii huwa siangalii muda gani,hata kama ni mwezi.Ila ukizidi mwezi huwa nakuwa na option ya kumtafuta Day worker ili apige kwa muda then akipona ndio namrejeshea chombo chake,na huyo Day worker namuomba mwenyewe amtafute.
-Akiwa na dharura ya kifamilia au maafa,au ugonjwa,basi hutoa kiasi cha pesa ili kumsaidia kama sehem ya familia,tusiangalie pesa tu.

Halafu kama unapesa ya mawazo na Bodaboda moja,basi wasiwasi ndio anakuwa rafiki yako muda woote.Ila kwa mie mwenye more than one,huwa hainipi saana presha.Na thanks Allah kwamba Drivers wangu woote ni watu safi sana.Kuanzia wa Bodaboda hadi kwenye Carry.

Hakua kazi isiyo na stresses,lazima uwe na wazo endelevu kwamba leo unamiliki bodaboda moja basi kuna siku utamiliki zaidi ya moja,na baadae utamilimiku hadi gari.Sasa akili lazima uiandae kwa changamoto na sio kuzikimbia kwa kufanyakazi kwa hofu au kubahatisha kama hao wa Mkataba eti akimaliza inakuwa yake.Kinachofuata hapo unakuwa akili yako ipo limited.

Uwezo wa kujua changamoto za biashara hii inakupa uwezo mkubwa saana wa kuelewa,na ndio maana wale wenye kutaka wepesi wengi wao wameachia kazi hizi.Kuna siku nimeenda TRA kusajili nikamkuta kuna mdada anamiliki bodaboda 21,na hesabu ya wiki na hakuna mkataba wa kusema kwamba mali ni ya Driver ndani ya mwaka.vyombo vyote ni mali yake.Na anaenda vizuri na Drivers wake,leo hii wanaume ndio wanakimbia changamoto,aiseee.Kuna siku Dar itakuwa mji fulani wa wategea maisha.

Ndoto yangu ni kuunda Kampuni ya usafiri Dar,bila kujali gari aina gani.Nasuburi itimie idadi ya gari kadhaa then ni unde Kampuni ili nile vitenda vidogo vidogo,Idea ya website tayari inafanyiwa kazi Nairobi.
Na pia Drivers wangu wawili wa Carry wote walitoka kwenye Bodaboda wakaomba kama nikileta Carry niwashift,na ndio nilivyofanya na hadi leo wanaenda vizuri.Na mmoja yupo kwene option ya Noah ndio nasubiria kuipakia Dubai ili niilete.Although pia Carry zinapoteza soko inabidi nibadilike niingie kwenye Townace au liteace Tani moja ambazo zinasoko zuri sana kibiashara na demand kwa wateja ni kubwa,hii ni kutokana na Drivers wangu.

Biashara akili,ukikimbia changamoto basi kaa pembeni usubirie siku za mwisho wa ujana wako uanze kulaumu watu.

Mtoto wa Kitaa wazo lako na Plan yako aisee nimeipenda saaana,endelea nayo na usikatishwe tamaa,biashara ni mbuni na akili ya ubunifu.Na pia hesabu hizi zinategemea maeneo gani ya Biashara ndio maana hutofautiana kidogo.
Ushauri kwako pia,katika hizi siku unazowaachia za free,basi tenga muda kama nusu saa hivi ukagua chombo chako,ili kama kunatatizo dogo basi uweze kulifix kabla halijawa kubwa.
Mkuu Zanzibar spice ki ukweli nimefuatilia mjadala huu kwa kirefu, na nimefaidika sana na mchango wako mkubwa ulioutoa hapa. mimi ni mmoja wapo ambaye nilitaka kuanzisha biashara hii lakini nikaogopa hizo changamoto lakini kwa elimu hii niliyoipa hapa, nafikiri nitaingia kwenye gemu mungu akipenda, na nitahitaji msaada zaidi kutoka kwako.
 
Asante mkuu nitakupa maelezo kwa ninavyoelewa,ila wengine watajazia,maana mie binaadam na sio mkamilifu wa kujua kila kitu,nitakapokosea watu watarekebisha.

Kwanza lazima uwe unaipenda hii biashara,sio kuona kwamba fulani anaifanya,au wengine hupenda kuitwa maboss.
Maana siku hizi ukiwa na bodabodam moja tu,basi kama Driver wako anapaki kituo fulani basi yeye anakuita boss,sasa na wenzie woote ukipita pale unasikia boss wake fulani yuleee,sasa kuna wengine wagonjwa kweli kuitwa boss wanaona rahaaa,hovyo kabisa
Sasa lazima iwe kwenye dam,na ukubali changamoto zake,ni biashara ngum sana ila nyepesi kama unajitambua.
Maduka mengi unapoenda kununua wanakusajilia pale pale kila kitu kama ukienda Mapema.Mie huwa naenda pale makao makuu ya Boxer duka lao kubwa.Na ukifika mapema wanakusajilia kila kitu an pia wanaku advise bima.So unatoka pale umekamilika,kinachofuata ni siku ya pili mwenyewe kwenda TRA ambapo ni procces fupi saana.
Unaweza haya yote ukayamaliza ndani ya siku mbili tu ukaanza kazi.
GPS system hii inategema na system ipi unatakiwa uwekewe ina specifications nyingi mno.Na kila moja ina gharama zake.zipo hadi zinaangalia mafuta yamo lita ngapi,zipo ambazo unazowez kuzima mwenyewe hata kama upo ulaya
Sasa kwa bodaboda,unaweka ila ya kawaida tu ya kuwezesha kujua chombo kipo wapi,na access ya Start and off.Halafu unapewa short training pale na consultation ya kuweza kutambua kama chombo chako kimeibiwa kutokana na speed na pia muelekeo wa chombo chako.Maana unaweza kuona kitu kinaeleke dodoma,hapo lazima utastuka,so unaweza kuwasiliana na kituo cha polisi na wakaikamata na unaweza pia kuizima ukiwa popote pale.
Ila wengi wakiibiwa na kama mwizi hajui,basi mtu huizimi,ila unawasiliana na kampuni iliyokufungia,then wao wana link a poloce wa kwenye doria kisha wanaikamata hata kama ipo Kyela huko.

KWa ufupi hakuna usumbufu wowote,unaponunua bodaboda ndio unasajiliwa kila kitu,inabakia wewe tu kwenda TRA kupata kadi maalum kama chombo cha biashara.GPS kuna mtu naweza kukupa number yake ila siku hizi kampuni nyingi saana wanafunga hizi stystem so unaweza ku google na ukazipata
Mkuu zanzibar spices nisaidie kampuni waliyokufungia GPS, mie pia nataka kufunga kwenye vyombo vyangu vya usafiri. Gharama zake zipoje mkuu?
 
Nikweli,unajua kuna watu waliingia kwa kubahatisha,na hawakuwa tayari na changamoto,na hapa ndio watu tunafeli.Na hawa wamikataba hakuna alieweza kudum kwenye game kwa miaka miwili,maana nawajua kibao waliosepa.Maana baada ya mkataba kuisha anakuwa hana hata senti moja ya kununua nyingine,hahaha kazi kweli.

Pia nakupongeza sana kwa kupiga hatua ya kuongeza more bodaboda,unajua ukiwanazo nyingi hata kama moja ikizingua kama kuibiwa au vinginevyo huumii sana kama ukiwa nayo moja.
Ila hakikisha vyote vina comprehensive insurances,ni muhim saana hili mkuu.

Wengi hukimbia sana changamoto,hasa vijana wa kiume,ila nimegundua na hili nimeona wakati nikienda kusajili chombo changu kimpya,yaani kina mama ndio wamekaza sana kwenye hii biashara,wanaume wengi wamekata tamaa.Sasa hii inanipa picha kwamba tunapoelekea kwa vijana wa kiume lazima hali iwe tata.Na ndio maana hata maandamano ya Siasa wanaume wengi kuliko wanawake.Maana wanawake wengi wanajiweza na wanapambana na wanaume wanasubiria nchi ya Asali na maziwa ya kusadikika na wengi kukata tamaa na kutaka biashara laini laini,wakati ulimwengu huu hakuna kabisa.

Mie baada ya Bodaboda kadhaa,ambazo niliingiza na Carry Kadhaa,then natarajia kuhamia kwenye Noah,naanza na mbili kwanza.Mwanzo nilifikiria Daladala ila nasepa kwanza,maana mradi wa mabasi bado unatisha kiasi.
Bajaji nazo niwazo zuri mkuu maana zinapiga mzigo.Na services zake nyepesi

Suala jingine ambalo mie nafanya kama nikitaka kununua Bodanoda,huwa namuuliza Driver ni aina gani anaitaka ndio nanunua,hili nalo ni muhim sana Mkuu.Maana Driver ana enjoy saana akipata chombo anachokipenda yeye.Maana mie huwa namuuliza hadi rangi ya chombo then ndio nanunua.Basie unahisi kabisa kwamba Drivers wako wana enjoy sana.
Zangu nyingi ni Boxers,ila kuna baadhi walitaka Sanlg kwa kuhofia kabali zambao nao nilifanya the same,nikawanunu hizo na rangi wanayoitaka.Sio vyema saana kununua chombo ambacho tajiri unakitaka,hili nalo zingatia sana kaka.
Hapo kwenye comprehensive insurance, bodaboda zimefungiwa wanatoa comprensive kwa pikipiki binafsi tu..ndo shida ya bodaboda sijajua kwanini makampuni ya bima yamesitisha huduma hii.
 
Mkuu hii hapa chini ni katika utaratibu wangu wa kuuza kila baada ya miezi sita ili kubadilisha nyingine na kumpa tena Driver.
Angalia hapo ikiwa na only six months na wiki tatu tangu kutumia.Sasa utuzwaji huo unatokana na hamasa kwa Driver kwamba pindi nikiiuza nampa percentage fulani ya bei kama motisha kwa matunzo.
Badi wanashindana kwa umaridadi.

Na Boxers zote nilizifunga GPS Tracking System,maana kipindi cha nyuma hali ilikuwa inatisha sana kwenye Boxers,hizi nyingine maana hazipo kwenye Target sana ya kuibiwa sijaweka,ili ni cost karibia laki nne kwa kila moja kuifunga.Ila nikiiuza huwa naitoa.Maana huwa nalipia huduma hiyo kwa Mwaka.

Hii hapa mkuu,ambayo nilii replace mwezi wa tano mwaka huu.Na hii ndio latest picha wakati namtumia mnunuaji,basi haikufika siku ya pili akanitafuta mbio,nikamuelekeza mdogo wangu wanakutana Bank na Lawyer wangu kesi ikaisha.Alilipa depost then muda wa Two weeks akamalizia akaja kuichukua
View attachment 295889
Bosi hebu niambie hua unauza sh ngap nataka moja niieke kene duka langu la gesi inisaidie kunisambazia mitungi kwa wateja.
 
Hapo kwenye comprehensive insurance, bodaboda zimefungiwa wanatoa comprensive kwa pikipiki binafsi tu..ndo shida ya bodaboda sijajua kwanini makampuni ya bima yamesitisha huduma hii.
Mkuu hata bajaji NIC hawatoi comprehensive insurance sijajua makampuni menginw
 
Nimejifunza mengi sana hapa. Niliwahi kufikiri niitumie hii biashara ili kukuza vihela vyangu kabla ya kuhamia kwenye Noah ila baada ya kusoma nyuzi tofauti tofauti kuhusu hii biashara niliingiwa na hofu sana na hii ni kutokana na shughuli zangu muda mrefu sipo nyumbani nikaona driver anaweza kuuza kabissa chombo. Baada ya kukutana na wakatisha tamaa wazoefu niliamua kuachana na hili wazo kabisa na kuwekeza kwingine ambako naona stress ni ndogo na haihitaji uangalizi wa kila siku/wiki. Ila najionea kwa mwenzangu ambaye tulikua na mawazo sawa hadi kufikia sahii anazo kama 4 hivi ingawa ananunua kwa watu ambazo zina hali nzuri kiasi zinamlipa vizuri tu na anazisimamia vyema.

Changamoto zipo katika kila bashara ni akili yako tu kuitumia vizuri ili uweze kuzitatua kwani unavyotatua hizo hangamoto ndio mwanzo wa kushika pesa. ingekua biashara ni kucopy na ku paste kila mtu angekua anafanya wakati huu, kila mmoja yupo uniq katika kutatua changamoto zake ndio maana utaona huyu biashara inamshinda na mwenzake anainunua na inafufuka upya. Bado nipo kwenye kujifunzakabla sijaingia kwenye Noah. ahsanteni kwa uzi huu mzuri
 
Mkuu hata bajaji NIC hawatoi comprehensive insurance sijajua makampuni menginw
Hawatoi kwasababu vyombo vya usafir vya biashara vina kuwa na risk kubwa sana ya kupata ajali kwahyo hawatapata faida koz ukipata ajali kama una hyo comprehensive bima bas wao ndio watakao itengeneza kuwa mpya au kununua mpya na kukupatia....
 
nadhani mkataba unakusaidia kuondoa stress za madereva, leo atakwambia mbovu,kesho kakamatwa lakini kwenye mkataba hakuna hayo
Wabumba ubovu ili wapige hela mi nilimpa dogo fulani mkataba wa miezi 7 ila kwa hesabu ya 15 elfu kila siku
 
Zanz spices nimependa idea yako.
Kwa upande wangu namiliki BAJAJI ya abiria, sina uzoefu sana lkn ningependa kujua suala la siku 6 za kazi na 1 ya dereva imekaaje mana dereva wangu ananiambia siku 5 kazi, siku ya sita service ya saba inakuwa cku ya dereva.
 
Nitarejea tena biashara hii baada ya kuikatia tamaa,ila nimejifunza kitu kuwa ukiipenda biashara au kazi yako basi Mungu huwa anaipa Neema zaidi na baraka,hata ukiamua kuuza upupu ukiipenda biashara yako utatoka tuu iwe isiwe ila kama unadharau kazi yako hata ungekuwa ni gavana wa BOT kila siku utaandamwa na dhiki tuuuu
 
M
Hili nilitaka kulijaribu:-(BODABODA ALL ARROUND SERVICES)
Nilikuwa na ndoto ya kuvuta hadi kufikia bodaboda kama kumi na tano hivi ili niunde kikampuni changu cha kutoa huduma kwa mfumo wa Call center(mtanielewa tu na kizungu changu cha bodaboda)
Yaani nakuwa na home office,halafu pikipiki zangu zoote nazifunga GPS Tracking System.
Ambapo itanifanya nijue pikipiki fulani ipo maeneo gani.

Sasa nilitaka kutengeneza website ya huduma zangua Vipeperushi,na aina zoote za kuitangaza huduma zangu.
-Yaani kwanza na guarantee huduma nzuri kwa wateja wangu,all drivers in uniform.

-Yaani kama mteja yupo Sinza,basi mie na track pikipiki gani ipo sinza au inaelekea Sinza,then na mdirect driver amfuate mteja alipo
Na hii inaendana na pia kila siku kuhakikisha kila Driver and bundle ya airtime kwenye sim yake on daily duty.

-Yaani nikakuwa na Stations zangu ambazo nakuwa naweka bodaboda kama tatu kila Center ndani ya jiji.
Na kama Driver base yake ipo Sinza,na akapata route ya Buguruni,basi hatorudi,atakaa Ilala ili ikitokea kazi ya huko aifanye ili kusave mafuta na ku make more profit.

Mfumo huu unaendana pia na personal businesss contacts za Drivers,maana wao wanakuwa na wateja wao,ila nilitaka kuweka mfumo ambao Drivers wote wanatoa huduma zinazofanana,ili kama personal Customer wa mhusika hayupo,basi anae take over afanye zaidi ya yule ili kuwa uniform.


Research:-
Ila nililifanyia uchunguzi wa kutosha saana,ikiwemo kwenda makampuni kadhaa mjini kuonana na staffs wa pale,na wengi sana waliniambia nianze haraka saana,wengine wanasema huwa wanahofu sana kuchukua bodaboda hovyo,lakini kwa vile wewe ni kampuni na una guarantee basi kwetu pia ni salama.Na unaweza hata kupata vitenda vya kutumwa mizigo midogo ya watu kama drivers wako wakionyesha uaminifu.Na mmoja akaniambia kwamba endapo iki work out basi kuna mengine mengi yatajitokeza yenye faida kwa kazi zangu.

Na hasa hili la kulipa kwa mwenzi pia wengi sana liliwavutia pia,maana wengine wanawatoto mashuleni walitaka niingie nao mkataba kwa maeneo yao.

Na kwa wafanyakazi wa Sekta binasfi na Serikali:-
Kwakuwa ni Kampuni na ina drivers wenye weledi na Smart,basi nilitaka kuingia mkataba na wafanyakazi binafsi wa kutoa huduma kwao,na malipo wafanye kwa mwezi.Hapa hata kama Driver hana mafuta,basi anakuja kuchukua Movement order ya full tank ili aweze kuhudumia wateja wetu.

Vyuo Vikuu,vyuo vya kawaida na baadhi ya Shule kwa wanafunzi :
Nilienda mlimani na Chuo cha Fedha,na vingine vidogo pamoja na shule kadhaa
Nashkuru sana nilipata support nzuri saana hasa kwa wanafunzi wa kike.Walionesha sana kuvutiwa na huduma hii.Na pia walinipa pia changamoto kadhaa.
Na hii ni ni kwamba sio muda wote wanakuwa na pesa,nikawaambia mie kwanza huduma then kama kuna uhakika wapesa mie nafaham mazingira ya wanafunzi,mtalinipa mkipata.Ilimradi uungwana uwepo.Basi hili liliwavutia saana.Maana unahudumiwa then utalipa katika muda wa mwezi au muda ukipata pesa hata kabla ya mwezi,au inaweza kuwa zaidi ya mwezi pia kwa dharura za kipesa au kuchelewa kwa pesa.

Je Driver anafaidika vipi:-
Driver analipwa malipo yake in Percentage ya huduma atakazotoa.Kwanza kunakuwana basic Salay ambazo woote hupata.Then ndio kuna ratio ya huduma atakayotoa.
Na nilifanya uchunguzi kwamba hii huduma ndio ingeingizia Drivers pesa nyingi saana.Maana ingekuwa ajira rasmi

Je kwanini nilisita:-
Nilipeleka wazo kwa baadhi ya family members,na mwanasheria wangu.
Akaniambia wazo ni zuri sana tena ubunifu mzuri.Ila kipindi hiki ambazo bodaboda zipo kwenye Target ya wizi,ni hatari kwako pia.Wanawez kutokea majambazo,wakavaa uniform kama za Driver wako ili wafanye tukio,then ukaja kuzolewa wewe.Aisee hii ilinitisha kweli.Maana jambazi siku zote hutafuta wapi pa kusukumizia ushahidi ili awe Salama.
Ikabidi niache kabisaa wazo hili,na baada ya kuacha basi kila wiki kesi za bodaboda na ujambazi,duhhh ndio nikalifuta wazo kabisaaa.

Ila habari iliishia hapo,maana mie mtoto wa maskini,kuja kuingiza mtego wa ujambazi kirahisi duuh.Jela sitoki.

Kwa mwenye kuwa na Bajaji anaweza kuifanya hii naikafanyakazi vizuri:

Je nini nitafanya au mtu anaweza kufanya:-
Unajua kama mtu akiitumia JF vizuri aisee kama anamtaji atapiga hela kweli,ila mie ni kwa mawazo yangu tu wakuu juu ya hili.Maana mie hupenda sana kuheshim mawazo yangu hata kama mtu atanicheka huwa sijali.
Maana nimeanza kuchekwa zamani saaana juu ya maisha.Maana anaekucheka leo basi siku ukifanya na ukifanikia basi huwa hacheki tena ila anatabasam.Kwa hiyo kucheka Rukhsa na Kejeli kama kawaida yetu wana JF rukhsa,maana mie mwenyewe kuna siku nawazingua wenzangu humuhumu,hahaha
Na unajua wapo wanaokuecha na kukujelei na the same time wanakupa njia ya kufanya,humu wamo wengi sana na ninawakubali sana pia.

Wazo ni hili
Mfano,ukawa na Bajaji maalum au hata Taxis licha ya kwamba watu wanasema hazilipi,ila inategemea na ubunifu wako.
Mfano unaongea na mabosi wa JF kina MAX,kwamba unataka kutumia Jina lao kwa makubaliana,naamini ni waelewa,kisha ukafanya Car Branding,nimeweka picha hapo chini mfano.Yaani Logo na jina la kampuni yoote JF,yaani full JF urembo
Yaani inakuwa Branded kama JF na nakshi kibaooo
Mie naamini Members wengi will be proud kutumia gari lako kwa kukodi,hii ni imani yangu na mtizamo wangu wakuu.Huu mfumo unaweza kuanza na Taxi kama tano hivi au Bajaji kama Tano hivi.

Naamini na kwa imani yangu,Members karibia woote tutajivunia saana kutumia huduma zako,maana tunajua tunarejesha mrejesho kwenye JF family member.Ni wazo langu tu wakuu.
View attachment 296102View attachment 296103
Mkuu umeogopa bure tu changamoto hyo inaweza ikawepo ama isiwepo ni bonge la wazo,hivi unajua baadae ungeweza kuanzisha kampuni ya ku supply hadi parcel,kama ilivyo DHL leo,kikubwa ni kujua jinsi ya kwenda na hyo changamoto,mfano usiyumie uniform yenye nembo kubwa ila ni kumfanya tu driver wako awe smart,nimegundua kuwa watu wengi wanapenda usafiri wa Bajaj au pikipiki ila changamoto ni uamninifu wa boda boda walio wengi,ila biashara hii ikipata kampuni inayoeleweka na ukawa una uwezo wa kuwafanyia drivers wako semina mara kwa mara na kuonyesha unawajali aisee watakuwa smart na waadilifu,
Asikwambie mtu huitaji kuongeza mshahara kwa mfanyakazi wako ili ajue unamthamin,we thamini anachokifanya na anapokuwa na shida usimtupe,Upo msemo mmoja wa kiarabu unasema Mtu siku zote ni mtumwa kwa yule anayempa kula au anayemthamini,kila mfanyakazi humuombea boss wake afanikiwe,hata mimi napenda kampuni iende juu zaid kwa kua inanipa kula
 
Asante mkuu nitakupa maelezo kwa ninavyoelewa,ila wengine watajazia,maana mie binaadam na sio mkamilifu wa kujua kila kitu,nitakapokosea watu watarekebisha.

Kwanza lazima uwe unaipenda hii biashara,sio kuona kwamba fulani anaifanya,au wengine hupenda kuitwa maboss.
Maana siku hizi ukiwa na bodabodam moja tu,basi kama Driver wako anapaki kituo fulani basi yeye anakuita boss,sasa na wenzie woote ukipita pale unasikia boss wake fulani yuleee,sasa kuna wengine wagonjwa kweli kuitwa boss wanaona rahaaa,hovyo kabisa
Sasa lazima iwe kwenye dam,na ukubali changamoto zake,ni biashara ngum sana ila nyepesi kama unajitambua.
Maduka mengi unapoenda kununua wanakusajilia pale pale kila kitu kama ukienda Mapema.Mie huwa naenda pale makao makuu ya Boxer duka lao kubwa.Na ukifika mapema wanakusajilia kila kitu an pia wanaku advise bima.So unatoka pale umekamilika,kinachofuata ni siku ya pili mwenyewe kwenda TRA ambapo ni procces fupi saana.
Unaweza haya yote ukayamaliza ndani ya siku mbili tu ukaanza kazi.
GPS system hii inategema na system ipi unatakiwa uwekewe ina specifications nyingi mno.Na kila moja ina gharama zake.zipo hadi zinaangalia mafuta yamo lita ngapi,zipo ambazo unazowez kuzima mwenyewe hata kama upo ulaya
Sasa kwa bodaboda,unaweka ila ya kawaida tu ya kuwezesha kujua chombo kipo wapi,na access ya Start and off.Halafu unapewa short training pale na consultation ya kuweza kutambua kama chombo chako kimeibiwa kutokana na speed na pia muelekeo wa chombo chako.Maana unaweza kuona kitu kinaeleke dodoma,hapo lazima utastuka,so unaweza kuwasiliana na kituo cha polisi na wakaikamata na unaweza pia kuizima ukiwa popote pale.
Ila wengi wakiibiwa na kama mwizi hajui,basi mtu huizimi,ila unawasiliana na kampuni iliyokufungia,then wao wana link a poloce wa kwenye doria kisha wanaikamata hata kama ipo Kyela huko.

KWa ufupi hakuna usumbufu wowote,unaponunua bodaboda ndio unasajiliwa kila kitu,inabakia wewe tu kwenda TRA kupata kadi maalum kama chombo cha biashara.GPS kuna mtu naweza kukupa number yake ila siku hizi kampuni nyingi saana wanafunga hizi stystem so unaweza ku google na ukazipata
Mkuu irudie tene upya proposal yako uifanyie kazi,kampuni huwa inakuwa kwa kupita kwenye tanuli la changamoto,jaribu ukishindwa utajua ulikosea wapi utarekebisha utakwenda juu,badae unaamin kwenye NOah Mahotelini humu Noah zinalipa balaaa,kuna mashule yanataka hizi noa sana mkuu,mimi sijafikia hatua kama yako ila pia kukupa ushauri mwenzangu uliyeko juu Mungu Hubariki zaidi,umefika mbali mkuu usiishie hapo
 
Kwa mwezi 280,000
Kwa miezi 10 2,800,00
Bei ya kununulia 2,100,000.
Faida 700,000.
Kuna madereva ambao wanapata motisha hadi miezi mitano wamekamilisha pesa zote. Anachukua pikipiki yake nampa mpya ile yeye anamkodishia mtu mwingine.
Sina mpango wa kuifanya kama biashara yangu ya milele. Hapa napatia hela ya mboga na matumizi madogomadogo.
Ni biashara nzuri kama utaifanya kwa weledi wa hali ya juu.
usiwe na haraka kutoka, mpaka hapo utakapoona mambo hayaendi vizuri. Niko Mkoani, nimejaribu naona inafaa. Nina bajaji 1 na pkpk 3, na bado kuna dogo ameniganda anataka nimnunulie na yeye. Ntamnunulia mwisho wa mwezi huu, Inshaallah.. Life goes on
 
Angalizo pia kwa wamiliki,hili nimekuwa nikilisema sana pia:-
Pindi unapoomba dua au maombi wakati unaenda kazini au unapoamka,basi ombea pia drivers wako au waajiriwa wako ili mungu awalinde na awape wepesi kwenye biashara yao,ikiwemo kupata wateja wengi na wenye kheir na huduma hizo.Maana Driver akipata na wewe ndio umepata.

Na kwa sie Waislam ni kwamba Mtu ukimuombea dua njema mwenzio basi mungu anakuongezea wewe zaidi,na pia hutenga malaika wa kukuombea na wewe zaidi.Ila wengi wetu kidogo hili ni tatizo.Maana hata hawa Drivers tunaowaajiri na wao pia hutuombea sie mabosi wao ila tunakuwa hatujui,maana anaomba kwamba usifilisike,na ufanikiwe zaidi,ili leo na kesho na yeye umkumbuke pindi neema zinapozidi.

Mie Drivers wangu karibia wote ni wakristo,ila katika kila sikukuu zao kwa wale nilionza nao muda wa mwaka,basi huwa natoa pesa ya sikukuu zoote kwa imani yake.Na hesabu ya siku moja au mbili za sikukuu naiacha ili na yeye aweze kuhudhuria ibada kanisani,na pia apate muda wa ku enjoy na watoto nyumbani na kuwapeleka sehem za michezo ya watoto nk.
Unapokuwa na furaha nyumbani wewe na watoto basi jua na mwenzio umkumbuke kwa imani yake.

Ila wengi wetu aisee,akiisha nunua huwa hana lugha njema,yaani ni ku force kwenda mbele,kuna jamaa mmoja yeye ni mtu wa Ulabu,basi anaweza kumstukiza Driver hata kati ya wiki ampelekee pesa bar.Asipopeleka kazi kweli.
Sasa hata hawa Drivers wanachangamoto zao nyingi sana kutoka kwa Matajiri,na ndio maana Drivers wengi hupenda kudeal na chombo anachomiliki Mwanamke.
te teh teh.
Ni kweli.
 
jaman eti spocket ina dum kwa muda gani? maana dreva wangu kila baada ya miez 3 nanunua nyingine
POle, kuna wakati nulikuwa na hii changamoto. Walinizingua kwa ubovu wa pikipiki, nikauza. Na aliyenunua ni yuleyue dereva msumbufu. Kwa sasa dogo ana pikipiki 4. Nikaacha hii biashara. Baaada ya juzi kuanza hii ya mkataba, naona na yeye kaja, nimempa.
So, usiogope changamoto. Pambana nazo kwa njia tofauti tofauti.
 
Asante mkuu nitakupa maelezo kwa ninavyoelewa,ila wengine watajazia,maana mie binaadam na sio mkamilifu wa kujua kila kitu,nitakapokosea watu watarekebisha.

Kwanza lazima uwe unaipenda hii biashara,sio kuona kwamba fulani anaifanya,au wengine hupenda kuitwa maboss.
Maana siku hizi ukiwa na bodabodam moja tu,basi kama Driver wako anapaki kituo fulani basi yeye anakuita boss,sasa na wenzie woote ukipita pale unasikia boss wake fulani yuleee,sasa kuna wengine wagonjwa kweli kuitwa boss wanaona rahaaa,hovyo kabisa
Sasa lazima iwe kwenye dam,na ukubali changamoto zake,ni biashara ngum sana ila nyepesi kama unajitambua.
Maduka mengi unapoenda kununua wanakusajilia pale pale kila kitu kama ukienda Mapema.Mie huwa naenda pale makao makuu ya Boxer duka lao kubwa.Na ukifika mapema wanakusajilia kila kitu an pia wanaku advise bima.So unatoka pale umekamilika,kinachofuata ni siku ya pili mwenyewe kwenda TRA ambapo ni procces fupi saana.
Unaweza haya yote ukayamaliza ndani ya siku mbili tu ukaanza kazi.
GPS system hii inategema na system ipi unatakiwa uwekewe ina specifications nyingi mno.Na kila moja ina gharama zake.zipo hadi zinaangalia mafuta yamo lita ngapi,zipo ambazo unazowez kuzima mwenyewe hata kama upo ulaya
Sasa kwa bodaboda,unaweka ila ya kawaida tu ya kuwezesha kujua chombo kipo wapi,na access ya Start and off.Halafu unapewa short training pale na consultation ya kuweza kutambua kama chombo chako kimeibiwa kutokana na speed na pia muelekeo wa chombo chako.Maana unaweza kuona kitu kinaeleke dodoma,hapo lazima utastuka,so unaweza kuwasiliana na kituo cha polisi na wakaikamata na unaweza pia kuizima ukiwa popote pale.
Ila wengi wakiibiwa na kama mwizi hajui,basi mtu huizimi,ila unawasiliana na kampuni iliyokufungia,then wao wana link a poloce wa kwenye doria kisha wanaikamata hata kama ipo Kyela huko.

KWa ufupi hakuna usumbufu wowote,unaponunua bodaboda ndio unasajiliwa kila kitu,inabakia wewe tu kwenda TRA kupata kadi maalum kama chombo cha biashara.GPS kuna mtu naweza kukupa number yake ila siku hizi kampuni nyingi saana wanafunga hizi stystem so unaweza ku google na ukazipata
Naomba namba ya hao jamaa wa GPS. Gharama kwa mwaka huwa kiasi gani?
 
Wabumba ubovu ili wapige hela mi nilimpa dogo fulani mkataba wa miezi 7 ila kwa hesabu ya 15 elfu kila siku
15,000x7x30=3,150,000
Iko powa hiyo.
Ukimpata wa hivyo mpe tu. faida yake ni 50% kwa muda wa miezi sita. Hiyo ni super profit.
 
Back
Top Bottom