Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

Wakuu nisaidieni hapa Mmoja wa driver wangu alikamatwa tangu j5 wiki iliopita kwa kosa la kutokua na kofia 2. akapelekwa central (Moshi) ikadaiwa faini ya 30,000 nikalipa ila wakawa wanaendelea kumzungusha kuhusu pikpik alipoendelea kuwasumbua pale wakamsweka ndani akalala akaamkia alhamis, alipotoka wameendelea kumpiga kalenda kila siku tukifatilia apo kituoni wanasema njoo kesho. siku ya mwisho ni ijumaa tumeenda akasign kisha akaambiwa arudi tena J3 nashindwa kuelewa nitumie njia gani ili kutoa mashine pale. msaada wowote pls au kama unamjua yeyote anayeweza kunisaidia. T.I.A
 
Wakuu nisaidieni hapa Mmoja wa driver wangu alikamatwa tangu j5 wiki iliopita kwa kosa la kutokua na kofia 2. akapelekwa central (Moshi) ikadaiwa faini ya 30,000 nikalipa ila wakawa wanaendelea kumzungusha kuhusu pikpik alipoendelea kuwasumbua pale wakamsweka ndani akalala akaamkia alhamis, alipotoka wameendelea kumpiga kalenda kila siku tukifatilia apo kituoni wanasema njoo kesho. siku ya mwisho ni ijumaa tumeenda akasign kisha akaambiwa arudi tena J3 nashindwa kuelewa nitumie njia gani ili kutoa mashine pale. msaada wowote pls au kama unamjua yeyote anayeweza kunisaidia. T.I.A
Polisi kukupiga kalenda hujui anataka nini? Jiongeze
 
Komaa kaka,we hata ukiibiwa Bodaboda moja kaza ongeza nyingine huku kesi ikiendelea.
Yaani hii biashara aisee inalipa asikudanganye mtu,ila kama mtoto wa mama unakimbia changamoto basi kaa mbali kabisa na biashara hii,utakuwa unanunia watu kila siku kwa kesi za Drivers,hahahaha

Maana wapo wamiliki hawataki kusikia Driver anaumwa wala anapata msiba wala anauguza,ebbbbo.
Na ndio maana wengi huwa hawabarikiwi kwenye game hii,maana wao wanajiangalia wao tu na pesa.

Mfanye Driver wako kama familia yako.Mie wapo Drivers wangu waliofiwa na wazee wao,basi huwa ndugu zangu waliopo Dar wanaenda msibani,na pia mie pia husafiri na kuja msibani au kama ninakazi basi Wife anapanda boat anakuja Dar kama siku nne then anageuza.Lakini lazima kati ya mie au wife aje Dar.Na the same akipata ajali lazima ndugu zangu wa Dar wahusike na the same time mie au wife anakuja Dar kumpa pole na kutoa mkono wa Pole.

Na kama ni ajali basi matibabu yoote tunasimamia sie,hata kama uzembe ni wa Driver basi mie huwa siangalii uzembe wake,kwanza ni kumshughulikia tiba yake then akiwa mzima ndio mengine yanafuata.Na sijawahi kumlaumu Driver kwa Uzembe wala kumlipish,maana hakuna anaependa ajali,muhim ni ushauri tu.Kisha natengeneza chombo changu siku zinaenda,na mungu mkubwa kwamba ajali nyingi sio kubwa saana.

Nikitengeneza naenda kugombana na watu wa bima,maana hawa jamaa wabishi kulipa kama wao hakuna.Wanaona Bodaboda kama vile ndio chanzo cha ajali zoote kumbe wazembe njiani ni wengi tu.

Mkuu!
Hizo Bodaboda zako huwa Drivers wanalala nazo makwao wewe unachukua hesabu tu!?
Au usiku wanarudisha kwako?
 
Asantee ulietela uzi huu
Samahani wakuu mimi ni mwanafunzi wa chuo naingia mwaka wa Pili sasa ninampango Kufikia mwakani mwezi wa pili ninunue Boxer kwa mtu kupitia online website ya Kupatana kwa bei inayorange kwene M 1.2 hadi 1.4 nataka napomaliza Chuo niwe nazo mbili kwa Kuanzia na baadae Nifungue Duka la Vitenge sabu hii biashara ndiyo nina uzoefu nayo .... ila naombeni ushahuri kuhusu wazo langu kuwa je Kununua pikipiki kwa mtu sio Risk. Ushahuri Wenu Wakubwa
 
Asantee ulietela uzi huu
Samahani wakuu mimi ni mwanafunzi wa chuo naingia mwaka wa Pili sasa ninampango Kufikia mwakani mwezi wa pili ninunue Boxer kwa mtu kupitia online website ya Kupatana kwa bei inayorange kwene M 1.2 hadi 1.4 nataka napomaliza Chuo niwe nazo mbili kwa Kuanzia na baadae Nifungue Duka la Vitenge sabu hii biashara ndiyo nina uzoefu nayo .... ila naombeni ushahuri kuhusu wazo langu kuwa je Kununua pikipiki kwa mtu sio Risk. Ushahuri Wenu Wakubwa
[emoji121]
UKINUNUA HII UTAKUJA KULIA MUDA SI MREFU!!!

[emoji121] [emoji121] [emoji121]
 
Mie ni Mmiliki.
Naungana na mleta hoja hapo juu,hii biashara lazima uwe na akili ya kuona mbali,sio hizi za kusema akupe elfu kumi then iwe yake.So,what next,inaamana wewe kila mwaka unatakiwa kubadilisha Driver mpya?hii sio akili ya kibiashara kabisaaa,na waoga wa biashara ndio wanaitumia.
Kama unakimbia changamoto za bodaboda basi sikufichi kwenye Gari ndio usisogee kabisaa,utakuafa,nakuambia kwa uzoefu

Mie hutumia hivi:-
-Hesabu yangu mie ni kwa Wiki Tsh:50,000
-Na kila baada ya miezi sita tu nauza Chombo nanunua kingine,na huwa nanunua kwanza kisha nampa Driver halafu ndio nakiuza ili asikose kazi hata siku moja.Unless kuwe na jambo katikati.
Na kwenye kuuza huwa baada ya kuuza nampa Driver kama zawadi ya pesa kwa kutunza Chombo vizuri in percentage,so hii hufanya na wao kuwa makini na chombo
-Driver akiwa na Msiba au ugonjwa wowote katika familia au Msiba wa Driver mwenzao,basi huleta pikipiki nyumbani au mdogo wangu anaenda kuichukua,na akipona anakuja kuichukua,hii huwa siangalii muda gani,hata kama ni mwezi.Ila ukizidi mwezi huwa nakuwa na option ya kumtafuta Day worker ili apige kwa muda then akipona ndio namrejeshea chombo chake,na huyo Day worker namuomba mwenyewe amtafute.
-Akiwa na dharura ya kifamilia au maafa,au ugonjwa,basi hutoa kiasi cha pesa ili kumsaidia kama sehem ya familia,tusiangalie pesa tu.

Halafu kama unapesa ya mawazo na Bodaboda moja,basi wasiwasi ndio anakuwa rafiki yako muda woote.Ila kwa mie mwenye more than one,huwa hainipi saana presha.Na thanks Allah kwamba Drivers wangu woote ni watu safi sana.Kuanzia wa Bodaboda hadi kwenye Carry.

Hakua kazi isiyo na stresses,lazima uwe na wazo endelevu kwamba leo unamiliki bodaboda moja basi kuna siku utamiliki zaidi ya moja,na baadae utamilimiku hadi gari.Sasa akili lazima uiandae kwa changamoto na sio kuzikimbia kwa kufanyakazi kwa hofu au kubahatisha kama hao wa Mkataba eti akimaliza inakuwa yake.Kinachofuata hapo unakuwa akili yako ipo limited.

Uwezo wa kujua changamoto za biashara hii inakupa uwezo mkubwa saana wa kuelewa,na ndio maana wale wenye kutaka wepesi wengi wao wameachia kazi hizi.Kuna siku nimeenda TRA kusajili nikamkuta kuna mdada anamiliki bodaboda 21,na hesabu ya wiki na hakuna mkataba wa kusema kwamba mali ni ya Driver ndani ya mwaka.vyombo vyote ni mali yake.Na anaenda vizuri na Drivers wake,leo hii wanaume ndio wanakimbia changamoto,aiseee.Kuna siku Dar itakuwa mji fulani wa wategea maisha.

Ndoto yangu ni kuunda Kampuni ya usafiri Dar,bila kujali gari aina gani.Nasuburi itimie idadi ya gari kadhaa then ni unde Kampuni ili nile vitenda vidogo vidogo,Idea ya website tayari inafanyiwa kazi Nairobi.
Na pia Drivers wangu wawili wa Carry wote walitoka kwenye Bodaboda wakaomba kama nikileta Carry niwashift,na ndio nilivyofanya na hadi leo wanaenda vizuri.Na mmoja yupo kwene option ya Noah ndio nasubiria kuipakia Dubai ili niilete.Although pia Carry zinapoteza soko inabidi nibadilike niingie kwenye Townace au liteace Tani moja ambazo zinasoko zuri sana kibiashara na demand kwa wateja ni kubwa,hii ni kutokana na Drivers wangu.

Biashara akili,ukikimbia changamoto basi kaa pembeni usubirie siku za mwisho wa ujana wako uanze kulaumu watu.

Mtoto wa Kitaa wazo lako na Plan yako aisee nimeipenda saaana,endelea nayo na usikatishwe tamaa,biashara ni mbuni na akili ya ubunifu.Na pia hesabu hizi zinategemea maeneo gani ya Biashara ndio maana hutofautiana kidogo.
Ushauri kwako pia,katika hizi siku unazowaachia za free,basi tenga muda kama nusu saa hivi ukagua chombo chako,ili kama kunatatizo dogo basi uweze kulifix kabla halijawa kubwa.
Mm nauliza hii service ya pikipiki kila muda gani na inagharimu kiasi gani
 
Asantee ulietela uzi huu
Samahani wakuu mimi ni mwanafunzi wa chuo naingia mwaka wa Pili sasa ninampango Kufikia mwakani mwezi wa pili ninunue Boxer kwa mtu kupitia online website ya Kupatana kwa bei inayorange kwene M 1.2 hadi 1.4 nataka napomaliza Chuo niwe nazo mbili kwa Kuanzia na baadae Nifungue Duka la Vitenge sabu hii biashara ndiyo nina uzoefu nayo .... ila naombeni ushahuri kuhusu wazo langu kuwa je Kununua pikipiki kwa mtu sio Risk. Ushahuri Wenu Wakubwa
Pikipiki used huwa inagharama za ukarabati nyingi tu haina faida kama mpya
 
Asante mkuu nitakupa maelezo kwa ninavyoelewa,ila wengine watajazia,maana mie binaadam na sio mkamilifu wa kujua kila kitu,nitakapokosea watu watarekebisha.

Kwanza lazima uwe unaipenda hii biashara,sio kuona kwamba fulani anaifanya,au wengine hupenda kuitwa maboss.
Maana siku hizi ukiwa na bodabodam moja tu,basi kama Driver wako anapaki kituo fulani basi yeye anakuita boss,sasa na wenzie woote ukipita pale unasikia boss wake fulani yuleee,sasa kuna wengine wagonjwa kweli kuitwa boss wanaona rahaaa,hovyo kabisa
Sasa lazima iwe kwenye dam,na ukubali changamoto zake,ni biashara ngum sana ila nyepesi kama unajitambua.
Maduka mengi unapoenda kununua wanakusajilia pale pale kila kitu kama ukienda Mapema.Mie huwa naenda pale makao makuu ya Boxer duka lao kubwa.Na ukifika mapema wanakusajilia kila kitu an pia wanaku advise bima.So unatoka pale umekamilika,kinachofuata ni siku ya pili mwenyewe kwenda TRA ambapo ni procces fupi saana.
Unaweza haya yote ukayamaliza ndani ya siku mbili tu ukaanza kazi.
GPS system hii inategema na system ipi unatakiwa uwekewe ina specifications nyingi mno.Na kila moja ina gharama zake.zipo hadi zinaangalia mafuta yamo lita ngapi,zipo ambazo unazowez kuzima mwenyewe hata kama upo ulaya
Sasa kwa bodaboda,unaweka ila ya kawaida tu ya kuwezesha kujua chombo kipo wapi,na access ya Start and off.Halafu unapewa short training pale na consultation ya kuweza kutambua kama chombo chako kimeibiwa kutokana na speed na pia muelekeo wa chombo chako.Maana unaweza kuona kitu kinaeleke dodoma,hapo lazima utastuka,so unaweza kuwasiliana na kituo cha polisi na wakaikamata na unaweza pia kuizima ukiwa popote pale.
Ila wengi wakiibiwa na kama mwizi hajui,basi mtu huizimi,ila unawasiliana na kampuni iliyokufungia,then wao wana link a poloce wa kwenye doria kisha wanaikamata hata kama ipo Kyela huko.

KWa ufupi hakuna usumbufu wowote,unaponunua bodaboda ndio unasajiliwa kila kitu,inabakia wewe tu kwenda TRA kupata kadi maalum kama chombo cha biashara.GPS kuna mtu naweza kukupa number yake ila siku hizi kampuni nyingi saana wanafunga hizi stystem so unaweza ku google na ukazipata
We jamaaa bado upo mm ndugu yako apa njoo unipe njia
 
Pesa ni zaidi ya kilevi ,Hao jamaaa wengi wao ni hawajielewi kabisa yaan
 
Nilifanya uchunguzi kwa madogo hatimaye nikampata dogo mmoja ambaye hatumii kilevi cha aina yoyote na pia anaishi kwao(kwa baba na mama) tunasali nae jumuiya
Bado sijaelewa mahesabu yako
 
Back
Top Bottom