Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

Wamiliki wa Bodaboda za biashara tukutane hapa

MTOTO KITAA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
245
Reaction score
116
Wakuu habar, nimewaita hapa, tupeane mbinu za biashara na changamoto zake, mbinu zangu mimi ni zifuatazo, huwa natumia mbinu ya kumwambia dereva kuwa ukileta hesabu wiki nzima, wiki inayofuata nampunguzia hesabu, badala ya 7000, namwambia alete 6000, hapo akirin nimepiga hesabu kuwa nimemuachia hesabu ya siku moja kama offer, na hapo biashara inaenda vizuri sana. njia nyingine, nawaambi kila tarehe 15 hutakiwi kuleta hesabu, na kila tarehe 30 utakiwi kuleta hesabu, na achukue yeye hizo pesa, lakini sharti langu siku zote lazima ulete hesabu kamili, ili uweze kupata offer hiyo.nawaombeni na nyinyi wenzangu mtoe mbinu zenu, ili tufanikiwe na hizi biashara.
 
kwa nini usifanye mkataba kabisa, akulipe elfu 10 kila siku kwa mwaka au mezi kumi matengenezo juu yake baada ya hapo iwe yake?

Nami nimejiuliza hilo mkuu, maana mi nilianza mkataba mwezi wa tisa, Kila siku elfu kumi na wengi wanafanya hivyo. Sijaelewa mleta mada kwanini afanye hivyo, sidhani kama atafaidika na chombo chake, naomba aje atwambie.
 
nadhani mkataba unakusaidia kuondoa stress za madereva, leo atakwambia mbovu,kesho kakamatwa lakini kwenye mkataba hakuna hayo
 
Mie ni Mmiliki.
Naungana na mleta hoja hapo juu,hii biashara lazima uwe na akili ya kuona mbali,sio hizi za kusema akupe elfu kumi then iwe yake.So,what next,inaamana wewe kila mwaka unatakiwa kubadilisha Driver mpya?hii sio akili ya kibiashara kabisaaa,na waoga wa biashara ndio wanaitumia.
Kama unakimbia changamoto za bodaboda basi sikufichi kwenye Gari ndio usisogee kabisaa,utakuafa,nakuambia kwa uzoefu

Mie hutumia hivi:-
-Hesabu yangu mie ni kwa Wiki Tsh:50,000
-Na kila baada ya miezi sita tu nauza Chombo nanunua kingine,na huwa nanunua kwanza kisha nampa Driver halafu ndio nakiuza ili asikose kazi hata siku moja.Unless kuwe na jambo katikati.
Na kwenye kuuza huwa baada ya kuuza nampa Driver kama zawadi ya pesa kwa kutunza Chombo vizuri in percentage,so hii hufanya na wao kuwa makini na chombo
-Driver akiwa na Msiba au ugonjwa wowote katika familia au Msiba wa Driver mwenzao,basi huleta pikipiki nyumbani au mdogo wangu anaenda kuichukua,na akipona anakuja kuichukua,hii huwa siangalii muda gani,hata kama ni mwezi.Ila ukizidi mwezi huwa nakuwa na option ya kumtafuta Day worker ili apige kwa muda then akipona ndio namrejeshea chombo chake,na huyo Day worker namuomba mwenyewe amtafute.
-Akiwa na dharura ya kifamilia au maafa,au ugonjwa,basi hutoa kiasi cha pesa ili kumsaidia kama sehem ya familia,tusiangalie pesa tu.

Halafu kama unapesa ya mawazo na Bodaboda moja,basi wasiwasi ndio anakuwa rafiki yako muda woote.Ila kwa mie mwenye more than one,huwa hainipi saana presha.Na thanks Allah kwamba Drivers wangu woote ni watu safi sana.Kuanzia wa Bodaboda hadi kwenye Carry.

Hakua kazi isiyo na stresses,lazima uwe na wazo endelevu kwamba leo unamiliki bodaboda moja basi kuna siku utamiliki zaidi ya moja,na baadae utamilimiku hadi gari.Sasa akili lazima uiandae kwa changamoto na sio kuzikimbia kwa kufanyakazi kwa hofu au kubahatisha kama hao wa Mkataba eti akimaliza inakuwa yake.Kinachofuata hapo unakuwa akili yako ipo limited.

Uwezo wa kujua changamoto za biashara hii inakupa uwezo mkubwa saana wa kuelewa,na ndio maana wale wenye kutaka wepesi wengi wao wameachia kazi hizi.Kuna siku nimeenda TRA kusajili nikamkuta kuna mdada anamiliki bodaboda 21,na hesabu ya wiki na hakuna mkataba wa kusema kwamba mali ni ya Driver ndani ya mwaka.vyombo vyote ni mali yake.Na anaenda vizuri na Drivers wake,leo hii wanaume ndio wanakimbia changamoto,aiseee.Kuna siku Dar itakuwa mji fulani wa wategea maisha.

Ndoto yangu ni kuunda Kampuni ya usafiri Dar,bila kujali gari aina gani.Nasuburi itimie idadi ya gari kadhaa then ni unde Kampuni ili nile vitenda vidogo vidogo,Idea ya website tayari inafanyiwa kazi Nairobi.
Na pia Drivers wangu wawili wa Carry wote walitoka kwenye Bodaboda wakaomba kama nikileta Carry niwashift,na ndio nilivyofanya na hadi leo wanaenda vizuri.Na mmoja yupo kwene option ya Noah ndio nasubiria kuipakia Dubai ili niilete.Although pia Carry zinapoteza soko inabidi nibadilike niingie kwenye Townace au liteace Tani moja ambazo zinasoko zuri sana kibiashara na demand kwa wateja ni kubwa,hii ni kutokana na Drivers wangu.

Biashara akili,ukikimbia changamoto basi kaa pembeni usubirie siku za mwisho wa ujana wako uanze kulaumu watu.

Mtoto wa Kitaa wazo lako na Plan yako aisee nimeipenda saaana,endelea nayo na usikatishwe tamaa,biashara ni mbuni na akili ya ubunifu.Na pia hesabu hizi zinategemea maeneo gani ya Biashara ndio maana hutofautiana kidogo.
Ushauri kwako pia,katika hizi siku unazowaachia za free,basi tenga muda kama nusu saa hivi ukagua chombo chako,ili kama kunatatizo dogo basi uweze kulifix kabla halijawa kubwa.
 
yaaani mzee wa zanzibar kama upo kwenye akiri yangu vile, maana kwa sas nina boda boda mbili, mwez ujao nataka kumgeza mbili tena, ili ziwe nne. Baada ya hapo nahamia kwenye bajaji. hata mimi suala la mkataba siafiki kabisa. na changamoto kabla sijafana biashara hii nilipitia jf kwanza, lakini nilipata majibu ya kukatisha tamaa, nikasema kupitia changamoto za waliopita, mi nitakuja kivingine.
 
Nikweli,unajua kuna watu waliingia kwa kubahatisha,na hawakuwa tayari na changamoto,na hapa ndio watu tunafeli.Na hawa wamikataba hakuna alieweza kudum kwenye game kwa miaka miwili,maana nawajua kibao waliosepa.Maana baada ya mkataba kuisha anakuwa hana hata senti moja ya kununua nyingine,hahaha kazi kweli.

Pia nakupongeza sana kwa kupiga hatua ya kuongeza more bodaboda,unajua ukiwanazo nyingi hata kama moja ikizingua kama kuibiwa au vinginevyo huumii sana kama ukiwa nayo moja.
Ila hakikisha vyote vina comprehensive insurances,ni muhim saana hili mkuu.

Wengi hukimbia sana changamoto,hasa vijana wa kiume,ila nimegundua na hili nimeona wakati nikienda kusajili chombo changu kimpya,yaani kina mama ndio wamekaza sana kwenye hii biashara,wanaume wengi wamekata tamaa.Sasa hii inanipa picha kwamba tunapoelekea kwa vijana wa kiume lazima hali iwe tata.Na ndio maana hata maandamano ya Siasa wanaume wengi kuliko wanawake.Maana wanawake wengi wanajiweza na wanapambana na wanaume wanasubiria nchi ya Asali na maziwa ya kusadikika na wengi kukata tamaa na kutaka biashara laini laini,wakati ulimwengu huu hakuna kabisa.

Mie baada ya Bodaboda kadhaa,ambazo niliingiza na Carry Kadhaa,then natarajia kuhamia kwenye Noah,naanza na mbili kwanza.Mwanzo nilifikiria Daladala ila nasepa kwanza,maana mradi wa mabasi bado unatisha kiasi.
Bajaji nazo niwazo zuri mkuu maana zinapiga mzigo.Na services zake nyepesi

Suala jingine ambalo mie nafanya kama nikitaka kununua Bodanoda,huwa namuuliza Driver ni aina gani anaitaka ndio nanunua,hili nalo ni muhim sana Mkuu.Maana Driver ana enjoy saana akipata chombo anachokipenda yeye.Maana mie huwa namuuliza hadi rangi ya chombo then ndio nanunua.Basie unahisi kabisa kwamba Drivers wako wana enjoy sana.
Zangu nyingi ni Boxers,ila kuna baadhi walitaka Sanlg kwa kuhofia kabali zambao nao nilifanya the same,nikawanunu hizo na rangi wanayoitaka.Sio vyema saana kununua chombo ambacho tajiri unakitaka,hili nalo zingatia sana kaka.
 
Mkuu hii hapa chini ni katika utaratibu wangu wa kuuza kila baada ya miezi sita ili kubadilisha nyingine na kumpa tena Driver.
Angalia hapo ikiwa na only six months na wiki tatu tangu kutumia.Sasa utuzwaji huo unatokana na hamasa kwa Driver kwamba pindi nikiiuza nampa percentage fulani ya bei kama motisha kwa matunzo.
Badi wanashindana kwa umaridadi.

Na Boxers zote nilizifunga GPS Tracking System,maana kipindi cha nyuma hali ilikuwa inatisha sana kwenye Boxers,hizi nyingine maana hazipo kwenye Target sana ya kuibiwa sijaweka,ili ni cost karibia laki nne kwa kila moja kuifunga.Ila nikiiuza huwa naitoa.Maana huwa nalipia huduma hiyo kwa Mwaka.

Hii hapa mkuu,ambayo nilii replace mwezi wa tano mwaka huu.Na hii ndio latest picha wakati namtumia mnunuaji,basi haikufika siku ya pili akanitafuta mbio,nikamuelekeza mdogo wangu wanakutana Bank na Lawyer wangu kesi ikaisha.Alilipa depost then muda wa Two weeks akamalizia akaja kuichukua
IMG_20140729_175337.jpg
 
Komaa kaka,we hata ukiibiwa Bodaboda moja kaza ongeza nyingine huku kesi ikiendelea.
Yaani hii biashara aisee inalipa asikudanganye mtu,ila kama mtoto wa mama unakimbia changamoto basi kaa mbali kabisa na biashara hii,utakuwa unanunia watu kila siku kwa kesi za Drivers,hahahaha

Maana wapo wamiliki hawataki kusikia Driver anaumwa wala anapata msiba wala anauguza,ebbbbo.
Na ndio maana wengi huwa hawabarikiwi kwenye game hii,maana wao wanajiangalia wao tu na pesa.

Mfanye Driver wako kama familia yako.Mie wapo Drivers wangu waliofiwa na wazee wao,basi huwa ndugu zangu waliopo Dar wanaenda msibani,na pia mie pia husafiri na kuja msibani au kama ninakazi basi Wife anapanda boat anakuja Dar kama siku nne then anageuza.Lakini lazima kati ya mie au wife aje Dar.Na the same akipata ajali lazima ndugu zangu wa Dar wahusike na the same time mie au wife anakuja Dar kumpa pole na kutoa mkono wa Pole.

Na kama ni ajali basi matibabu yoote tunasimamia sie,hata kama uzembe ni wa Driver basi mie huwa siangalii uzembe wake,kwanza ni kumshughulikia tiba yake then akiwa mzima ndio mengine yanafuata.Na sijawahi kumlaumu Driver kwa Uzembe wala kumlipish,maana hakuna anaependa ajali,muhim ni ushauri tu.Kisha natengeneza chombo changu siku zinaenda,na mungu mkubwa kwamba ajali nyingi sio kubwa saana.

Nikitengeneza naenda kugombana na watu wa bima,maana hawa jamaa wabishi kulipa kama wao hakuna.Wanaona Bodaboda kama vile ndio chanzo cha ajali zoote kumbe wazembe njiani ni wengi tu.
 
Kwa mwezi 280,000
Kwa miezi 10 2,800,00
Bei ya kununulia 2,100,000.
Faida 700,000.
Kuna madereva ambao wanapata motisha hadi miezi mitano wamekamilisha pesa zote. Anachukua pikipiki yake nampa mpya ile yeye anamkodishia mtu mwingine.
Sina mpango wa kuifanya kama biashara yangu ya milele. Hapa napatia hela ya mboga na matumizi madogomadogo.
Ni biashara nzuri kama utaifanya kwa weledi wa hali ya juu.
 
nakupata sana, mzee wa zanzibar,hilo la kuwa karibu na madereva hata mim huwa nalifanya, muda mwingine dereva anakuja geto usiku namwambia shemeji yake ampakulie chakula ale, na huwa anafurah sana, some time, anakuja na kusema bro leo kijiwe kigumu, huwa namwambia poa lete hicho ulichonacho, na siku hiyo inakuwa imepita, so naishi nao kama ndugu, mfano siu ya sikuku ya iddi iliyopita, siku moja kabla niliwaabia chukueni hesabu ya siku hiyo, ili nao kesho yake wafurahie sikukuu, basi wanafurah hao, na hii napelekea hata kama siku hali mbaya,naambiwa huwa wanaenda kukopa, ili apate hesabu yangu, kwa lengo kuepuka kuniudhi.
 
Wandugu naomba mmiliku mmoja wa bodaboda ambaye yuko hapa Dar aniPM namba yake ili nimtafute kwa ushauri personally, kuna mambo mengi nahitaji kujua personally kabla sijaanza hii biashara.
 
Mie ni Mmiliki.
Naungana na mleta hoja hapo juu,hii biashara lazima uwe na akili ya kuona mbali,sio hizi za kusema akupe elfu kumi then iwe yake.So,what next,inaamana wewe kila mwaka unatakiwa kubadilisha Driver mpya?hii sio akili ya kibiashara kabisaaa,na waoga wa biashara ndio wanaitumia.
Kama unakimbia changamoto za bodaboda basi sikufichi kwenye Gari ndio usisogee kabisaa,utakuafa,nakuambia kwa uzoefu

Mie hutumia hivi:-
-Hesabu yangu mie ni kwa Wiki Tsh:50,000
-Na kila baada ya miezi sita tu nauza Chombo nanunua kingine,na huwa nanunua kwanza kisha nampa Driver halafu ndio nakiuza ili asikose kazi hata siku moja.Unless kuwe na jambo katikati.
Na kwenye kuuza huwa baada ya kuuza nampa Driver kama zawadi ya pesa kwa kutunza Chombo vizuri in percentage,so hii hufanya na wao kuwa makini na chombo
-Driver akiwa na Msiba au ugonjwa wowote katika familia au Msiba wa Driver mwenzao,basi huleta pikipiki nyumbani au mdogo wangu anaenda kuichukua,na akipona anakuja kuichukua,hii huwa siangalii muda gani,hata kama ni mwezi.Ila ukizidi mwezi huwa nakuwa na option ya kumtafuta Day worker ili apige kwa muda then akipona ndio namrejeshea chombo chake,na huyo Day worker namuomba mwenyewe amtafute.
-Akiwa na dharura ya kifamilia au maafa,au ugonjwa,basi hutoa kiasi cha pesa ili kumsaidia kama sehem ya familia,tusiangalie pesa tu.

Halafu kama unapesa ya mawazo na Bodaboda moja,basi wasiwasi ndio anakuwa rafiki yako muda woote.Ila kwa mie mwenye more than one,huwa hainipi saana presha.Na thanks Allah kwamba Drivers wangu woote ni watu safi sana.Kuanzia wa Bodaboda hadi kwenye Carry.

Hakua kazi isiyo na stresses,lazima uwe na wazo endelevu kwamba leo unamiliki bodaboda moja basi kuna siku utamiliki zaidi ya moja,na baadae utamilimiku hadi gari.Sasa akili lazima uiandae kwa changamoto na sio kuzikimbia kwa kufanyakazi kwa hofu au kubahatisha kama hao wa Mkataba eti akimaliza inakuwa yake.Kinachofuata hapo unakuwa akili yako ipo limited.

Uwezo wa kujua changamoto za biashara hii inakupa uwezo mkubwa saana wa kuelewa,na ndio maana wale wenye kutaka wepesi wengi wao wameachia kazi hizi.Kuna siku nimeenda TRA kusajili nikamkuta kuna mdada anamiliki bodaboda 21,na hesabu ya wiki na hakuna mkataba wa kusema kwamba mali ni ya Driver ndani ya mwaka.vyombo vyote ni mali yake.Na anaenda vizuri na Drivers wake,leo hii wanaume ndio wanakimbia changamoto,aiseee.Kuna siku Dar itakuwa mji fulani wa wategea maisha.

Ndoto yangu ni kuunda Kampuni ya usafiri Dar,bila kujali gari aina gani.Nasuburi itimie idadi ya gari kadhaa then ni unde Kampuni ili nile vitenda vidogo vidogo,Idea ya website tayari inafanyiwa kazi Nairobi.
Na pia Drivers wangu wawili wa Carry wote walitoka kwenye Bodaboda wakaomba kama nikileta Carry niwashift,na ndio nilivyofanya na hadi leo wanaenda vizuri.Na mmoja yupo kwene option ya Noah ndio nasubiria kuipakia Dubai ili niilete.Although pia Carry zinapoteza soko inabidi nibadilike niingie kwenye Townace au liteace Tani moja ambazo zinasoko zuri sana kibiashara na demand kwa wateja ni kubwa,hii ni kutokana na Drivers wangu.

Biashara akili,ukikimbia changamoto basi kaa pembeni usubirie siku za mwisho wa ujana wako uanze kulaumu watu.

Mtoto wa Kitaa wazo lako na Plan yako aisee nimeipenda saaana,endelea nayo na usikatishwe tamaa,biashara ni mbuni na akili ya ubunifu.Na pia hesabu hizi zinategemea maeneo gani ya Biashara ndio maana hutofautiana kidogo.
Ushauri kwako pia,katika hizi siku unazowaachia za free,basi tenga muda kama nusu saa hivi ukagua chombo chako,ili kama kunatatizo dogo basi uweze kulifix kabla halijawa kubwa.

Braza Mwenyezi Mungu akubariki sana,ushauri wako ni wa thamani.
 
nakupata sana, mzee wa zanzibar,hilo la kuwa karibu na madereva hata mim huwa nalifanya, muda mwingine dereva anakuja geto usiku namwambia shemeji yake ampakulie chakula ale, na huwa anafurah sana, some time, anakuja na kusema bro leo kijiwe kigumu, huwa namwambia poa lete hicho ulichonacho, na siku hiyo inakuwa imepita, so naishi nao kama ndugu, mfano siu ya sikuku ya iddi iliyopita, siku moja kabla niliwaabia chukueni hesabu ya siku hiyo, ili nao kesho yake wafurahie sikukuu, basi wanafurah hao, na hii napelekea hata kama siku hali mbaya,naambiwa huwa wanaenda kukopa, ili apate hesabu yangu, kwa lengo kuepuka kuniudhi.

Huu nim fumo mzuri sana Mkuu.
Maana kama unakuwa na usimamizi mzuri basi Pikipiki inaduma katika ubora wake zaidi ya miaka 2 hadi 3 kama services zitafanywa kwa ubora wake na kama hakutakuwa na ajali kubwa.

Halafu unakuwa hauna presha kabisaa,ina namna yake ya utulivu hii biashara.Maana mie zangu zoote ziliisha nilipa zamani saaana.Nazunguushia faida tu.Na hata Carry zangu zoote hesabu imeishafungwa zamaniii,sasa nakula faida tuu.
 
Angalizo pia kwa wamiliki,hili nimekuwa nikilisema sana pia:-
Pindi unapoomba dua au maombi wakati unaenda kazini au unapoamka,basi ombea pia drivers wako au waajiriwa wako ili mungu awalinde na awape wepesi kwenye biashara yao,ikiwemo kupata wateja wengi na wenye kheir na huduma hizo.Maana Driver akipata na wewe ndio umepata.

Na kwa sie Waislam ni kwamba Mtu ukimuombea dua njema mwenzio basi mungu anakuongezea wewe zaidi,na pia hutenga malaika wa kukuombea na wewe zaidi.Ila wengi wetu kidogo hili ni tatizo.Maana hata hawa Drivers tunaowaajiri na wao pia hutuombea sie mabosi wao ila tunakuwa hatujui,maana anaomba kwamba usifilisike,na ufanikiwe zaidi,ili leo na kesho na yeye umkumbuke pindi neema zinapozidi.

Mie Drivers wangu karibia wote ni wakristo,ila katika kila sikukuu zao kwa wale nilionza nao muda wa mwaka,basi huwa natoa pesa ya sikukuu zoote kwa imani yake.Na hesabu ya siku moja au mbili za sikukuu naiacha ili na yeye aweze kuhudhuria ibada kanisani,na pia apate muda wa ku enjoy na watoto nyumbani na kuwapeleka sehem za michezo ya watoto nk.
Unapokuwa na furaha nyumbani wewe na watoto basi jua na mwenzio umkumbuke kwa imani yake.

Ila wengi wetu aisee,akiisha nunua huwa hana lugha njema,yaani ni ku force kwenda mbele,kuna jamaa mmoja yeye ni mtu wa Ulabu,basi anaweza kumstukiza Driver hata kati ya wiki ampelekee pesa bar.Asipopeleka kazi kweli.
Sasa hata hawa Drivers wanachangamoto zao nyingi sana kutoka kwa Matajiri,na ndio maana Drivers wengi hupenda kudeal na chombo anachomiliki Mwanamke.
 
Wandugu naomba mmiliku mmoja wa bodaboda ambaye yuko hapa Dar aniPM namba yake ili nimtafute kwa ushauri personally, kuna mambo mengi nahitaji kujua personally kabla sijaanza hii biashara.

Watakuja mkuu,maana wengine asili yetu Bara ila tupo Zanzibar kikazi.
Tunakuja kwa kudokoadokoa.Ila wapo wengi watakuja.
 
Back
Top Bottom