Wamasai na Ngorongoro: Siasa ya Maendeleo ya Vitu au ya Watu?

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Asalam, pamoja na kuamua kuweka bandiko hili, lakini nimeshuhudia uchache ama kupotea kwa haraka bandiko lolote lenye neo "masai". Lkn huenda hili likabaki.

Ngongoro kama zilivyohifadhi nyingine Tz imekuwepo kwa miaka mingi japo ina utofauti na nyingine. Pale wanyama mwitu, wanyama wa kufugwa, binadamu na shughuli za kilimo vimefanyika kwa pamoja. Simba wa ngorongoro hali Ng'ombe anakula Nyati. Na havamii binadamu, anavamia kundi la swala (Coexistence?)
Mshiriki mmojawapo wa Royal Tour akawaita Primitive Community (jamii ya kishenzi). Tukalipokea, hatukulikemea.

Ikafuatiwa na hotuba, ikasema 1950s walikuwa 9000, sasa wamefika 100,000+. Ikawekwa hoja katika hotuba hiyo .. "Ama tuache ngorongoro ife, au tuqngalie namna ya kufanya.."

Ikaanza kampeni ya kuwaondoa hawa Maasai pale. Mwanzo ikasemwa sio maasai wa Tanzani, ni wa Nchi jirani.

Yakafanyika mengi, wakajengewa nyumba huko Handeni, wakawekewa na vyoo vya maji na sebule za kukaa na viti, pamoja na sakafu za tiles. Maasai wa ngorongoro akapewa sasa godoro la kulalia na mkate wa kuanzia maisha. Hatukujali tamaduni, mazingira ili tuokoe ngorongoro. Wazo linaweza kuwa zuri lkn likakosa uhalali katika utekezaji.

Kwanini tumetafuta njia fupi ya transformation ya jamii ya kimaasai? Je, kila mahala ambapo population ya Tz imeongezaka tuihamishe? Mbona dar watu wakiongezeka tunawapekea barabara? Kwanini Serikali isiwe na mpango wa muda mrefu wa kuwekeza kwenye Social transformation ya ile jamii ili taratibu watoto wao wapate kazi mijini na kuachana na maisha ngorongoro kutokana na kusoma masomo ya SAYANSI, TEKNOLOJIA, UFUNDI NA HESABU?

Kwanini mpango huu haujahusisha tafiti za kisayansi za kupima athari ya hili zoezi (IMPACT assessment) kama ile ya Prof Chachage S Chachage ya Ufugaji wa kamba hadi kuzaa kitabu cha MAKUWADI WA SOKO HURIA?

Je, Senti mbili tatu za Utalii zitaifikisha Tanzania kuwa nchi iliyoendelea kiasi cha kuwaoka Wanasai?
Maswali ni mengi... Wamasai wanapata tabu kwa kosa la kiasili la wao kujikuta wanaishi Ngorongoro. Mikakati ya kuondoa vizazi vyao itaendelea hadi lini.

NANI WA KUWASEMEA? NA KUWASEMEA WAPI?
 
Hivi lile tamsaha la wamasai huko Ngorongoro ambalo lingehudhuriwa na wawakilishi wa ufalme kutoka huko UAE limeshafanyika au bado?. Sioni bandiko lolote kuhusiana na hicho kitu hapa JF,kulikoni?
 
Hivi lile tamsaha la wamasai huko Ngorongoro ambalo lingehudhuriwa na wawakilishi wa ufalme kutoka huko UAE limeshafanyika au bado?. Sioni bandiko lolote kuhusiana na hicho kitu hapa JF,kulikoni?

Sijui, lkn kwa ujumla mabandiko yanayohusu Maasai na Ngorongoro yameadimika sana hapa. Ni kama hakuna habari kabisa
 
Back
Top Bottom