Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shanghai anadaiwa kujiapisha kuwa Laigwanan wa jamii ya kimaasai

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
232
260
Mbunge wa Ngorongoro Mhe. Emmanuel Ole Shanghai anadaiwa kujiapisha mwenyewe kuwa Laigwanan, Uapisho uliohudhuriwa na watu takribani ishirini wa familia yake katika sherehe ndogo iliyofanyika nyumbani kwake katika kijiji cha Enduleni kata ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro. Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni madiwani wawili wa Tarafa ya Ngorongoro, kiongozi mmoja wa Kijiji hicho pamoja na majirani takribani 17.
IMG_0241.JPG

Hata hivyo ndugu wa Mbunge huyo ambae ni Wakili Msomi Joseph Ole Shangai hakuweza kuhudhuria sherehe hizo kwa kuwa utaratibu wa alioutumia kujiapisha mwenyewe umekiuka misingi ya kimila, hivyo kuliita tukio hilo kuwa ni kiini macho kwa wasiojua mila za kimaasai, hivyo amemuita kuwa ni Laigwanan wa Mchongo, akiwataka wamaasai kukataa kudanganywa na kufanyiwa maigizo kama hayo.

Pia ameeleza kuwa utaratibu wa kumpata Laigwanan wa Jamii unajulikana na kila mmasai kwamba anapaswa kuchaguliwa na jamii ikijumuisha koo zao zote mbili yaani ukoo wa Oldomony na Ukoo wa Lwakiteny ambao hao huwahusisha wazee kwa kufanya utafiti wa siri katika jamii yao kisha hupendekeza jina ambalo hupelekwa kwenye kikao cha jamii ambapo sherehe huandaliwa kabla mhusika kuambiwa kuwa ameteuliwa na atatawazwa kuwa Laigwanan.

Ameendelea kueleza kuwa wazee Wakisha Kamisha maandalizi yote ndipo mhusika huambiwa Habari hiyo ambayo hupokelewa kwa kilio kikubwa. Lakini sio kwamba mhusika mwenyewe ndiye anaepaswa kuamua kualika watu na kufanya sherehe kama siasa kisha kujiita Laigwanan kama alivyofanya Mhe. Mbunge wa Mgorongoro Emmanuel Ole Shangai ambae ni kaka yake wa kufikia.
images-1.jpg

Vilevile ameeleza kuwa aliyekuwa akitarajiwa kuwa mgeni rasmi ambae ni mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka pamoja na mbunge wa Afrika mashariki Mhe. James Ole Milya hawakuhudhuria sherehe hiyo kama ishara ya kulaani tukio hilo lililofanywa na mbunge huyo wa Ngorongoro wakiliita kuwa ni tukio la kihuni ambalo linapaswa kulaaniwa na jamii yote ya kimasaai wenye mapenzi mema Afrika ya Mashariki.

Hivyo amehitimisha kuwa Ulaigwan wa Mhe. Emmanuel Ole Shangai haukubaliki kwa jamii ya kimasai kwa kuwa haukufuata taratibu na kuwa ametumia ushawishi wa kifedha ili kupata uongozi huo akilenga kupata uenyekiti wa malaigwanani Tanzania ili kugombea nafasi ya ulaigwan wa Afrika Mashariki ambao vikao vyake vitatumika kudai ardhi ya maasai (Maasai Land) zikijumuisha wilaya za Narok, Kajiado, Ngorongoro, Oldonyo le ngai, Simanjiro na Kiteto.

Ole Shangai amelaani kitendo cha marafiki zake kumtenga katika sherehe yake hiyo akidai kuwa atalitolea tamko baada ya kushauriana na washauri wake wa kisiasa baada ya kutathmini kilichotokea ambacho hakukitarajia.
 
Raisi aliyewaletea maumivu Wamasai anapunguziwa maumivu yakuoza kwa makaburi.
 
Ole Shangai amelaani kitendo cha marafiki zake kumtenga katika sherehe yake hiyo akidai kuwa atalitolea tamko baada ya kushauriana na washauri wake wa kisiasa baada ya kutathmini kilichotokea ambacho hakukitarajia.
 
Mwamba huyu hapa sasa .
Yaani kashikaji kameona kajiapishe kenyewe na kawe ka kakiongozi .
Duh ngoja na mimi nirudi Mvuti nijiapishe kuwa kiongozi wa ndugu zangu wote wa Dar es salaam .
 
Back
Top Bottom