Uleigwanan wa Lowassa wadaiwa kugombaniwa na wawili wa familia moja ya Ole Shangai

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
232
260
  • Ni Emmanuel Ole Shangai na Joseph Ole Shangai.
  • Wamasai wamkataa Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai kutaka kujiapisha kuwa Leigwanan.
Freelancing Promotion Facebook Cover Photo (1).png

Bonyeza link chini kusikiliza

SAUTI ZA WAMAASAI WAKIPINGA EMMENUEL OLE SHANGAI KUJIAPISHA ULEIGWANAN

View: https://www.youtube.com/watch?v=Bx2TDkYrLUc

Na Mwandishi Wetu - Ngorongoro

Imethibitishwa kuwa Mbunge Jimbo la Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai anatarajia kujiapisha kuwa laigwanan wa kisiasa kwa lengo la kuongeza nguvu yake ya kisiasa kwa kuwa sehemu ya kuchukua nafasi ya Laigwanan wa Afrika Mashariki iliyoachwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge mstaafuwa Jimbo la Monduli Hayati Edward Ngoyai Lowassa.

Baadhi ya Wananchi waliozungumza kwa hasira na mwandishi wetu wameeleza kuwa Lengo la kutaka kupata uongozi huo wa kimila ni kutaka kuongeza nguvu yake kisiasa, kuwa sehemu ya viongozi wa kimasai watakaodai ardhi ya wamasai kupitia Umoja wa wamasai wa Afrika Mashariki (Maasai land) na kupata nguvu ya ushawishi ya kuzuia watu wasihame kutoka ndani ya hifadhi.

Hata hivyo kitendo hicho kimelaaniwa na kudaiwa kuwa huenda kikaibua mgogoro mkubwa katika jamii hiyo kwa kuwa baadhi ya malaigwan hawakubaliani na mchakato wa Emmanuel Ole Shangai wa kujipa uongozi wa kimila kwa kuwa hana sifa za kuwa katika nafasi hiyo na kuwa ndani ya familia moja ya Shangai haiwezi kutoa viongozi wa wawili wa kimila.

Hili linatokana na ukweli kuwa jamii inamtaka Joseph Ole Shanghai ndio apewe uongozi wa kimila ambapo anatarajiwa kusimikwa uongozi wa kimila siku za hivi karibuni.

Aidha, wananchi hao wameeleza kuwa kama suala hilo likiachwa lifanyike litasababisha mgogoro wa kifamilia kwa kuwa ndugu hao watasababisha mpasuko hata katika jamii yao ya kimasai, jambo linaloweza kuchochea machafuko na kutokuelewana kwa jamii husika.
 
Kila la kheri kwa Ndugu zetu Wamasai lakini chagueni Mtu mwenye HEKIMA na BUSARA ambae hawezi kuburuzwa na CCM na Magenge yake.
 
Kwani ulaigwanan unagombewa kama ubunge na udiwani au utaratibu kimila upoje, mimi nilidhani wanapatikana kwa kufunuliwa kama Vaticani
 
  • Ni Emmanuel Ole Shangai na Joseph Ole Shangai.
  • Wamasai wamkataa Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai kutaka kujiapisha kuwa Leigwanan.
View attachment 2921880

SAUTI ZA WAMAASAI WAKIPINGA EMMENUEL OLE SHANGAI KUJIAPISHA ULEIGWANAN
Na Mwandishi Wetu - Ngorongoro

Imethibitishwa kuwa Mbunge Jimbo la Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai anatarajia kujiapisha kuwa laigwanan wa kisiasa kwa lengo la kuongeza nguvu yake ya kisiasa kwa kuwa sehemu ya kuchukua nafasi ya Laigwanan wa Afrika Mashariki iliyoachwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge mstaafuwa Jimbo la Monduli Hayati Edward Ngoyai Lowassa.

Baadhi ya Wananchi waliozungumza kwa hasira na mwandishi wetu wameeleza kuwa Lengo la kutaka kupata uongozi huo wa kimila ni kutaka kuongeza nguvu yake kisiasa, kuwa sehemu ya viongozi wa kimasai watakaodai ardhi ya wamasai kupitia Umoja wa wamasai wa Afrika Mashariki (Maasai land) na kupata nguvu ya ushawishi ya kuzuia watu wasihame kutoka ndani ya hifadhi.

Hata hivyo kitendo hicho kimelaaniwa na kudaiwa kuwa huenda kikaibua mgogoro mkubwa katika jamii hiyo kwa kuwa baadhi ya malaigwan hawakubaliani na mchakato wa Emmanuel Ole Shangai wa kujipa uongozi wa kimila kwa kuwa hana sifa za kuwa katika nafasi hiyo na kuwa ndani ya familia moja ya Shangai haiwezi kutoa viongozi wa wawili wa kimila.

Hili linatokana na ukweli kuwa jamii inamtaka Joseph Ole Shanghai ndio apewe uongozi wa kimila ambapo anatarajiwa kusimikwa uongozi wa kimila siku za hivi karibuni.

Aidha, wananchi hao wameeleza kuwa kama suala hilo likiachwa lifanyike litasababisha mgogoro wa kifamilia kwa kuwa ndugu hao watasababisha mpasuko hata katika jamii yao ya kimasai, jambo linaloweza kuchochea machafuko na kutokuelewana kwa jamii husika.
Laigwaniani au Kiongozi wa Maleigwanani? Lowasa alikuwa mkuu wa Maleigwanani, kama ni ishu tu ya Leigwanani wako wengi sana,
 
Safari hii Laigwanan atoke upande wa pili kuondoa hii kadhia.
 
Lowassa mwenyewe kuwa Laigwanan ilikua ni batili maana Lowassa ni Mmeru siyo masai
Alifanikiwa kubadili kabila.

Anyways haina maana tena.

So long as alitaka iwe hivyo.

Tunamkaribisha umasaini.

Rest easy Laigwanani Lowassa.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Alifanikiwa kubadili kabila.

Anyways haina maana tena.

So long as alitaka iwe hivyo.

Tunamkaribisha umasaini.

Rest easy Laigwanani Lowassa.
Hivi mtu anaweza kubadili kabila? Ni njia zipi utatumia kubadili?
 
  • Ni Emmanuel Ole Shangai na Joseph Ole Shangai.
  • Wamasai wamkataa Mbunge wa Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai kutaka kujiapisha kuwa Leigwanan.
View attachment 2921880
Bonyeza link chini kusikiliza

SAUTI ZA WAMAASAI WAKIPINGA EMMENUEL OLE SHANGAI KUJIAPISHA ULEIGWANAN

View: https://www.youtube.com/watch?v=Bx2TDkYrLUc

Na Mwandishi Wetu - Ngorongoro

Imethibitishwa kuwa Mbunge Jimbo la Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai anatarajia kujiapisha kuwa laigwanan wa kisiasa kwa lengo la kuongeza nguvu yake ya kisiasa kwa kuwa sehemu ya kuchukua nafasi ya Laigwanan wa Afrika Mashariki iliyoachwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge mstaafuwa Jimbo la Monduli Hayati Edward Ngoyai Lowassa.

Baadhi ya Wananchi waliozungumza kwa hasira na mwandishi wetu wameeleza kuwa Lengo la kutaka kupata uongozi huo wa kimila ni kutaka kuongeza nguvu yake kisiasa, kuwa sehemu ya viongozi wa kimasai watakaodai ardhi ya wamasai kupitia Umoja wa wamasai wa Afrika Mashariki (Maasai land) na kupata nguvu ya ushawishi ya kuzuia watu wasihame kutoka ndani ya hifadhi.

Hata hivyo kitendo hicho kimelaaniwa na kudaiwa kuwa huenda kikaibua mgogoro mkubwa katika jamii hiyo kwa kuwa baadhi ya malaigwan hawakubaliani na mchakato wa Emmanuel Ole Shangai wa kujipa uongozi wa kimila kwa kuwa hana sifa za kuwa katika nafasi hiyo na kuwa ndani ya familia moja ya Shangai haiwezi kutoa viongozi wa wawili wa kimila.

Hili linatokana na ukweli kuwa jamii inamtaka Joseph Ole Shanghai ndio apewe uongozi wa kimila ambapo anatarajiwa kusimikwa uongozi wa kimila siku za hivi karibuni.

Aidha, wananchi hao wameeleza kuwa kama suala hilo likiachwa lifanyike litasababisha mgogoro wa kifamilia kwa kuwa ndugu hao watasababisha mpasuko hata katika jamii yao ya kimasai, jambo linaloweza kuchochea machafuko na kutokuelewana kwa jamii husika.

Lowasa hakuwahi kustaafu aliachia ngazi mwenyewe, upotoshaji haukuongezei siku za kuishi duniani sana unakuongezea dhambi.
Mrema naye hakustaafu aliachia ngazi mwenyewe tena ndani ya bunge.
 
Back
Top Bottom