Wamarekani wanatembea na silaha

Wamarekani wanatembea na silaha

Ritz ndio maana nikasema mimi kama mimi!. Labda nina bahati... Hahaa!. Halafu nadhani hukunielewa kuhusu sehemu ya kuishi, sijakushutumu; nilikua natoa mfano tu!. Siri kubwa ya kuepuka hizo adha ni DISPLINE!.
 
Tatizo kubwa sana la US ni haki na uhuru wa raia yeyote kuwa na bunduki na kutembea nayo. Imepunguza sana kujiamini kwa Polisi wanaposhughulika kukamata na kudhibiti watuhumiwa wa uhalifu. Na ile stereotype ya watu weusi na uhalifu ndio mambo yanazidi kuharibika.

Siamini kama tatizo la ubaguzi wa rangi ni kubwa hivyo. Tena US kuna afadhali kuliko katika baadhi ya nchi zetu za dunia ya 3. Wao wasipodhibiti huo uhuru wa mtu kujikusanyia bunduki anavyotaka basi hali itaendelea kuwa taabu mtindo mmoja. Watu wanaishi kwa kuogopana. Malumbano ya kawaida tu watu wanatoleana pisto! Usikatize jirani na uzio wa mtu huko suburbs anaweza kukulipua akihisi tishio.

Huyo jamaa mweusi aliyeuawa na Polisi kwanza ile kubugudhiwa na ombaomba tu kamtolea pisto. Haya huyo aliyeua polisi alikuwa na zana za uhakika hadi jamaa wakaamua kumpelekea bomu kwa robot kummaliza! What a country!
 
bb596a2e8f834a8275f61664309e13c0.jpg


c6dbfc6b7616644b958dd2b2f85c4a17.jpg


(Above pictures) Wamarekani weupe wanatembea na silaha (wanaogopa kuvamiwa na Wamarekani weusi).

"DUNIA KAMWE HAITOTULIA MPAKA TUPATE ADUI KUTOKA NJE YA DUNIA"
 
Hakuna kitu kibaya kama damu ya mtu, Wazungu wamemuua Saddam kwa kisingizio cha silaha za maangamizi hakuwa nazo, wamemuua Gadaffi bila kosa, matokeo yake wakasababisha kuibuka kwa ISIS, sasa wana haha..Wamesababisha vita Sirya hakukaliki wakimbizi wanakimbilia kwao sasa, wanahaha tena, hawawataki.sasa wanataka waende wapi wakati wao ndo wamesababisha vita kwao, sasa hivi wameanza kuua watu weusi, sasa wanategemea wakimuua ndugu yako wewe uchekelee au ushangilie, walijua kabisa nini kitatokea kwao sasa wanalalamika nn, haiwezekani ww umuue mtu bila sababu halafu, familia yake na marafiki zake wakuangalie tuu, eti wa kwanza, eti wa pili hee...hata kama ni uvumilivu una mwisho wake jamani, wale sio wanyama ni binadamu wana nyongo..sasa wakichukua hatua oooo kwa hiyo walitakaje ? watu watulie tuu na kuuwawa kama kuku ama...watavuna walichopanda, huwezi kupanda mahindi ukavuna choroko, ukipanda Mauti utavuna mauti tuu hakuna jinsi..
hicho ulichosema rais Philippines amekisema kwenye sikukuu ya eid
 
Ndiyo, hali siyo mbaya kabisa na hizo picha wala hazihusiani chochote na mauaji ya hao jamaa wawili.

Mnalazimisha mambo na kutamani sana Marekani ichafuke lakini haitotokea.
Hamna anayelazimisha hali halisi ndiyo hii huko Marekani hii Dallas.

Hii Atlanta.


Hii Alabama.

 
Hamna anayelazimisha hali halisi ndiyo hii huko Marekani hii Dallas.

Hii Atlanta.



Sasa huoni kwamba hao watu wanaandamana kwa amani kutoa dukuduku lao?

Hali ingekuwa mbaya kihivyo unadhani hao watu wangepata hata hiyo fursa ya kuandamana na kurudi makwao salama?

Halafu waandamanaji wala siyo weusi tu....uthibitisho kwamba idadi kubwa ya walio wengi, licha ya rangi zao za ngozi, wanakataa matendo ya polisi wachache walio waovu.
 
Sasa hivi tumeshazoea kusikia wamarekani wakimalizana wao kwa wao....
USA BABY[emoji631] [emoji631] [emoji631]
 
Hii Phoenix.


Halafu tunaambiwa hali ni swali.
 
Sasa huoni kwamba hao watu wanaandamana kwa amani kutoa dukuduku lao?

Hali ingekuwa mbaya kihivyo unadhani hao watu wangepata hata hiyo fursa ya kuandamana na kurudi makwao salama?

Halafu waandamanaji wala siyo weusi tu....uthibitisho kwamba idadi kubwa ya walio wengi, licha ya rangi zao za ngozi, wanakataa matendo ya polisi wachache walio waovu.
Dukuduku la nini?
 
"DUNIA KAMWE HAITOTULIA MPAKA TUPATE ADUI KUTOKA NJE YA DUNIA"
Umetumia akili kubwa sana mdau hadi kuongea hilo jambo,
Ni kweli " Dunia kamwe haitotulia mpaka tupate adui kutoka nje ya dunia"
Hongera sana kwa huo ukomavu wako wa akili.
 
Back
Top Bottom