Hamas yakubali kuweka silaha chini Gaza; Trump kutangaza mpango wa Bodi ya Amani
.Chanzo cha picha, Reuters
Afisa mwandamizi wa Hamas ameliambia shirika la habari la BBC kwamba kundi hilo limekubali mpango wa Bodi ya Amani wa kuachana kabisa na silaha katika Ukanda wa Gaza huku akiongeza kuwa taarifa rasmi itatolewa hivi karibuni.
Trump atangaza mpango wa Bodi ya Amani
.Chanzo cha picha,EPA
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Bodi ya Amani imefikia makubaliano ya kuhakikisha Hamas na makundi mengine yenye silaha katika Ukanda wa Gaza yanaweka silaha chini kabisa.
Afisa mwandamizi wa Hamas ameliambia shirika la habari la BBC kwamba kundi hilo limekubali mpango wa Bodi ya Amani wa kuachana kabisa na silaha huko Gaza, na kwamba taarifa rasmi itatolewa hivi karibuni.
Kwa upande wake, Israel bado haijatoa maoni au kauli rasmi kuhusu tangazo hilo.
Trump amesema kuwa Israel itaondoka katika Ukanda wa Gaza kadri zoezi la kuachana na silaha litakapokamilika, na akayataja makubaliano hayo kuwa "hatua muhimu kuelekea Gaza hatimaye kutawaliwa na serikali mpya ya Kipalestina."
Awamu ya pili ya mpango wa usitishaji mapigano huko Gaza ulioratibiwa na Marekani inajumuisha kundi la Hamas kuachana kabisa na serikali.
Awamu hiyo ya pili pia inahusisha ujenzi upya wa Ukanda wa Gaza, ambao umeathiriwa vibaya na vita vya muda mrefu