Kuna maamuzi ya kukubaliana nayo ila hilo sio mojawapo
Kosea kila kitu ila sio kuoa au kuolewa
Sawa nimekuelewa my dia, wewe unataka mama akubali kuonana na msichana then kwanini usikae ukaongea na mama!Mueleze kwamba anavyofanya si vyema kumchukia mtu asomfahamu,ampe nafasi huyo binti kwanza kabla hajamuweka kwenye black list!Lakini dogo alitoa introduction tu akapata negative response. Namfahamu Maza ni mtu wa kusali na hata siku moja hajawahi kuamini Mambo ya kienyeji.
Dah! I'm sorry ila your mom is sthing else. Hivi anajua kitu anachomuandalia mdogoako psychologically? Mapenzi ni suala jingine aisee mwenyewe ameona mtu ambae atamfurahia ktk maisha. Hivi unafikiri drug addicts na walevi au wazee wa michepuko wanatokeaga wapi saa zingine?What if ataoa anaemtaka yeye then wasielewane ndo atafurahi kumuona mwanae hivyo?Huyu wa kwetu wala hata hajaletwa home. Dogo mpaka anasema hatataka asikie habari za kuoa.
Wote mko sawa ila mtu nzima dawa kaona mengi ,ni mama na hamna kama yeye anakushauri kwa sababu ya upenda. Penda kuzingatia ushauri
Ukiona baba ametia neno juu ya mchumba wako basi ujue hapo kuna jambo na yakupasa uwe mwepesi wa kuchunguza na ikiwezeka kumdadisi baba hasa huo wasi wasi wake kwani mara nyingi hutokea kweli. Kuhusu wamama unapaswa kuwaelewa ingawa wengine wanakuaga na hoja za msingi jambo la muhimu ni kuangalia nafsi yako je unampenda huyo mchumba wako na je una uhakika ukiwa juu ya mawe bado atakupenda.Unajua nilimsikiliza mama mpaka nikapata hasira kama mie ndio ninayezuiwa. Wanafaa kuwa washauri na sio waamuzi wakuu. wao wenyewe sasa hivi ukiwaambia wakutafutie mchumba hawawapati ila tuu wanalazimisha mtu wa kabila lao. Mbona kina baba huwa hawaulizii mambo kama haya?
Inawezekana mama amekosea kwa upande flani lkn na ninyi vijana mnakosea mnapowaambia wachumba wenu kuwa mama alikua hakutaki kabisa . sasa hii inategemea sana hekima mwanamke akiwa mwelewa ataelewa hofu ya mama na kama si mwelewa basi utakua umeanzisha uhasama kati ya mama na mkeo/mchumba. Wamama wana emotions sana nafikiri ni wajibu wenu kukaa na huyo mama mkamuelewesha na kumuuliza kwanini anakua mkali wakati mlengwa hajamuona. Naamini mkimuuliza kistaarabu atawaaambia na pengine aweza kumpokea mlengwa kwa mikono miwili.Mkuu the way walivyokuwa wanaongea walimkatisha tamaa kabisa.! Walikuwa hawataki hata kusikia habari hizo. Mwingine angesema kamlete basi tumuone.
Dah! I'm sorry ila your mom is sthing else. Hivi anajua kitu anachomuandalia mdogoako psychologically? Mapenzi ni suala jingine aisee mwenyewe ameona mtu ambae atamfurahia ktk maisha. Hivi unafikiri drug addicts na walevi au wazee wa michepuko wanatokeaga wapi saa zingine?What if ataoa anaemtaka yeye then wasielewane ndo atafurahi kumuona mwanae hivyo?
Mwambieni aache hizo mambo, madhara ni makubwa kuliko anavyofikiri.Alafu mamako anaonekana mpaka familia ya mdogoako ataicontrol yeye. Niwe muwazi mkwe wa namna hii I can't handle tutafikia pabaya aisee.Hawa ndo wanalazimishaga wajue upande wa pili wa mtu ukoje maana atakusukuma mwisho utaamua kama Pinda. "Liwalo na liwe"
Sawa nimekuelewa my dia, wewe unataka mama akubali kuonana na msichana then kwanini usikae ukaongea na mama!Mueleze kwamba anavyofanya si vyema kumchukia mtu asomfahamu,ampe nafasi huyo binti kwanza kabla hajamuweka kwenye black list!
WaPo waliozuiwa wakaleta kichwa ngumu baadae ndoa ikawa gunia la misumari kichwani mwa mwenye kipara. WaPo waliopuuza ya wazazi na ndoa zao hadi leo ni chemchem inayobubujika furaha kila saa na kila wakati
Rafiki wazazi wetu walio wengi wana desturi hizo kwasababu hata enzi zao wao wakiolewa kulikuwa na ile hulka kwamba watu wa kabila fulani si zuri kuoa n.k kwahio hio fikra bado wamebaki nayo.. mimi mama yangu mpaka leo hii ana tabia hizo na anataka anichagulie mume,nikimpa green light mbona atapiga vigelegele,wamama wana ile tabia ya kuwa overprotective kwamba wanajua yaliyobora kwa watoto wao aidha awe wa kike au wakiume!Na kama kawaida ya wanawake wote wanapenda kuongea mpaka dini zimesema; kwahio asipopata atakalo lazima atabwabwaja sana tu!
mama yangu ananiambiaga neno moja MWANANGU MUNGU AKUSAIDIE
Rafiki wazazi wetu walio wengi wana desturi hizo kwasababu hata enzi zao wao wakiolewa kulikuwa na ile hulka kwamba watu wa kabila fulani si zuri kuoa n.k kwahio hio fikra bado wamebaki nayo.. mimi mama yangu mpaka leo hii ana tabia hizo na anataka anichagulie mume,nikimpa green light mbona atapiga vigelegele,wamama wana ile tabia ya kuwa overprotective kwamba wanajua yaliyobora kwa watoto wao aidha awe wa kike au wakiume!Na kama kawaida ya wanawake wote wanapenda kuongea mpaka dini zimesema; kwahio asipopata atakalo lazima atabwabwaja sana tu!
Hapana aisee, wanawake wanajuana tabia kwa kutazamana tu. Mama mtu mzima anaweza akabashiri tabia ya binti kwa kumtazama tu na kumsemesha na ni mara chache mno kukosea. Mara nyingi wamama huwa hawakosei, sema ni ngumu mno kumpata binti perfect.
Wakinamama wanawajua wanawake wenzao, na wana "extra sensory perception". Wanapokukataza kitu wanakutakia mema na wala hawana nia mbaya kwako, ni kwa nia njema tu, labda huyo mama awe mchawi.
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
Pole sana umekutana na mtoto wa mama,kwahiyo ndo yameisha kimasihara hivyo