Wamachinga,
Wamachinga ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Lindi, wilaya za Kilwa na Lindi.
Lugha yao ni Kimachinga. Inasadikiwa asili ya kabila hili ni kandokando ya ziwa Mkoe, hasa mto Mbwemkuru unapoingia baharini.
Wamachinga katika biashara. Kwa kipindi cha karne ya 20 na 21 wamekuwa maarufu katika miji mbalimbali kwa kuuza bidhaa, hasa nguo za mitumba, wakiwa wamezishika mikononi wakisaka wateja.
Hali hii imepelekea wafanyabiashara wa namna hiyo wote kuitwa Wamachinga ingawa baada ya muda mfupi mtindo huu wa biashara ulianza kuhusisha watu wa rika na makabila tofauti.