Wamachinga kutumia majengo ya NHC Kariakoo

MoureenAbel

Member
Sep 24, 2021
29
43
Kufuatia wafanyabiashara wadogo kuandika barua TAMISEMI wakiomba kutumia majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa yaliyopo mitaa ya Tandamti na Msimbazi kwa ajili shughuli zao, Wizara ya Ardhi imeridhia ombi hilo lakini kwa kuwapa majengo matatu yaliyopo mtaa wa Nyamwezi na Mkunguni karibu kabisa na Soko Kuu la Kariakoo.

Wizara imeelekeza NHC kuyaboresha majengo hayo haraka iwezekanavyo ili wafanyabiashara hao walioondolewa katikati ya Soko la Kariakoo waanze kuyatumia.

‘’Hili ni suala la msingi na lazima lifanyike kwa haraka na sisi Wizarani tulipate taarifa mapema na tujue majengo haya yatachukua watu wangapi na uendelezaji wake utachukua muda gani ili wafanyabiashara wajue kuna eneo maalum la kufanya biashara kama kama ambavyo wamekusudia wao kupatiwa’’ alisema Naibu Waziri wa Ardhi, Dkt Mabula.

Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamachinga Tanzania Stephen Lusinde kwa upande wake alisifu uamuzi wa Naibu Waziri Dkt Mabula kutembelea majengo ya NHC yaliyoainishwa na kubainisha kuwa hatua hiyo inaonesha kuwa sasa mambo yanaweza kukaa vizuri kwa wamachinga kupata muelekeo wa wapi pa kwenda.
 
Kiongozi mwanamke anaweza kumbe ndio lilikuwa tatizo hilo!?

New Microsoft Word Document (3)-1.jpg
 
Watapata madon tu humo, au machinga wakipewa watapangisha madon. Serikali inasumbuka sana na ishu ya machinga
 
Bongo buana...sasa machinga na kufanya biashara kwenye majengo wapi na wapi
 
Back
Top Bottom