Waliuzwa utumwani mara tatu

Waliuzwa utumwani mara tatu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,508
Reaction score
830,009
Millie na Christine McKoy walikuwa mapacha wa Kiafrika walioungana waliozaliwa Julai 11, 1851, na Jacob na Monemia McKoy, ambao walikuwa watumwa.

Waliuzwa mara tatu kati ya umri wa miezi 6 na miaka 6. Walikuwa wameungana kwenye uti wa mgongo wa chini. Ili kudhibiti mwendo wasianguke watembeapo walianzisha utembeajii wa upande upande ambao ulibadilika na kuwa mtindo wa dansi maarufu kwa umma. Na Wamiliki wao wakawatumia kama vivutio vya sarakasi na majumba ya maonesho katika sehemu za Marekani na ulaya

Mnamo Januari 1, 1863, Millie na Christine waliachiliwa kutoka utumwani.

Kauli mbiu yao ilikuwa: “Kama Mungu alivyoamuru, tunakubali.” Walikuwa na sauti nzuri na walijulikana kama "Nightingale of Two Heads."

Walipata umaarufu, wakisafiri kwenda nchi nyingi kutumbuiza na hata walionekana na Barnum Circus, wakicheza mbele ya Malkia wa Uingereza.

Walizungumza Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kijerumani, na Kiitaliano, pamoja na kuimba na kucheza piano vizuri sana.

Mnamo Oktoba 8, 1912, Millie na Christine walikufa wakiwa na umri wa miaka 61 kutokana na kifua kikuu.
1742099712275.jpg
 
Hichi ndicho nilichokiwaza.

Au mmoja anataka kwenda mahali kutembea mwingine hataki anataka kupumzika.
Mhh hapo itabidi wakubaliane sasa.

Ila kikawaida twins wana lots of similarities.. na wanapokua conjoined maana yake wanashare almost everything including thoughts.

Mungu ana miujiza yake kwa kweli.
 
Back
Top Bottom