Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,832
Wananchi wanaoishi bonde la Msimbazi waliokumbwa na mafuriko wametoa maoni yao baada ya Rais Samia kutangaza wapewe fidia huku ya ardhi ikiwa milioni nne huku jumla wengine wakipata jumla ya milioni sita wakihoji wanaenda kufanyaje ili wapate kiwanja na nyumba huko wanapoenda.
Kijana mmoja amesema hawezi kuondoka kwake kwa fidia iliyotajwa huku mwingine akisema wameambiwa hakuna sheria inayomlazimisha Rais kulipa fidia bali ni huruma ya Rais.
Serikali ilipokea bilioni 463 kwa ajili ya mradi wa bonde la mto Msimbazi ikiwemo ujenzi wa daraja na kuboresha matumizi ya ardhi katika bonde hilo, nusu zikiwa msaada na nusu mkopo.