Wakili Msando na mkewe wachemka mahakamani, waamuriwa kulipa fidia ya milioni 175

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,820
Mahakama Kuu, imewaamuru wafanyabiashara Albert Msando na Jacquelene Msando, kumlipa mfanyabiashara Bahati Mgonja anayemiliki kampuni ya Y&H Mgonja Enterprises, Sh175 milioni kama fidia ya biashara ya vinywaji.

Hii ni baada ya mrufani wa kwanza, The Don’s Group Tanzania ya Jijini Arusha na Albert Msando na mkewe Jacquelene kushindwa rufaa waliyoifungua mahakama kuu, kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Albert Msando kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambapo yeye na mkewe ndiyo wamiliki wa klabu maarufu ya The Don’s Lounge ya Jijini Arusha inayofanya vizuri kibiashara katika jiji hilo la utalii.

Bahati Mgonja anayefanya biashara kwa jina la Y&H Mgonja Enterprises, alifungua kesi ya madai Mahakama ya Hakimu Arusha, akidai malimbikizo ya madai ya Sh181.2 milioni zilizotokana na deni la vinywaji aliowauzia wadaiwa hao.

Mwananchi

Pia, soma=> DC Msando adai atakata rufaa kuamriwa kulipa fidia ya 175M, asema mdai amemshtaki Msando badala ya kampuni yake in Habari na Hoja mchanganyiko
 
Mahakama Kuu, imewaamuru wafanyabiashara Albert Msando na Jacquelene Msando, kumlipa mfanyabiashara Bahati Mgonja anayemiliki kampuni ya Y&H Mgonja Enterprises, Sh175 milioni kama fidia ya biashara ya vinywaji.

Hii ni baada ya mrufani wa kwanza, The Don’s Group Tanzania ya Jijini Arusha na Albert Msando na mkewe Jacquelene kushindwa rufaa waliyoifungua mahakama kuu, kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Albert Msando kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga ambapo yeye na mkewe ndiyo wamiliki wa klabu maarufu ya The Don’s Lounge ya Jijini Arusha inayofanya vizuri kibiashara katika jiji hilo la utalii.

Bahati Mgonja anayefanya biashara kwa jina la Y&H Mgonja Enterprises, alifungua kesi ya madai Mahakama ya Hakimu Arusha, akidai malimbikizo ya madai ya Sh181.2 milioni zilizotokana na deni la vinywaji aliowauzia wadaiwa hao.

Mwananchi
Ukila lazima uliwe (JK). Yeye amekula vinywaji vya wenzake na mahakama imemla. Sheria ni msumemo, aache ujinga alipe vinywaji vya watu.
 
Back
Top Bottom