Waliopigania uhuru walipigania ili wajinufaishe. Hata wanaharakati na wapinzani leo wanapambana ili kujinufaisha

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,238
12,753
Viongozi wa mapambano ya uhuru walifanya yote yale ili waishi maisha waliyokuwa wanaona wakoloni wanaishi. Waliudanganya umma kuwa wanapigania maslahi ya umma lakini ulikuwa uongo mtupu.

Baada ya uhuru wakaishia kujitajirisha wao na familia zao. Wafanya mapinduzi ya kijeshi nao hufanya hivyo hivyo. Jambo hili limeanza toka pale binadamu alipoanza kuwa na taasisi za kisiasa, maelfu ya miaka huko. Wakati visiwa vya Comoro vinapata uhuru ilipitishwa kura kwa visiwa vinavyotaka kubaki Ufarsansa vibaki na vinavyotaka kutoka vitoke.

Kisiwa cha Mayotte kati ya visiwa vyote kilichagua kubaki chini ya Ufaransa. Visiwa vingine vikaingizwa mkenge na "Wapigania uhuru." Matokeo yake hao wapigania uhuru wakaanza kupigana na kupinduana wenyewe kwa wenyewe wakigombania ulaji. Leo wananchi wa Mayotte wana maisha mazuri na Wacomoro wanahangaika kuzamia Mayotte kufuata maisha bora.

Ajabu ni kuwa kila siku binadamu wanadanganyika na mbinu hii. Wanaaminishwa kuwa yanayopiganiwa ni maslahi ya wote nao wanaamini. Wanakuta wamedangannywa, akija mwingine wanaingia tena mkenge, wanaingia mkenge tena na tena hadi wanakufa.

Kuna watu waliamini Lowassa anahamia CHADEMA ili kupigania maslahi ya umma. Walipambana kufa na kupona. Kumbe mwenzao ana yake. Baada ya kuona jambo lake halijakamilika akaondoka zake. Hivyo hivyo kwa Sumaye na wanasiasa maslahi ambao ndiyo wengi duniani kote.

Kuna mifumo ovu kama ya ubaguzi wa rangi kule Afrika Kusini inatakiwa kuondoka, lakini kamwe usiamini viongozi wa harakati hizo kuwa wanapigania maslahi ya umma. Wakina Tabo Mbeki na Zuma waliishia kuwa mafisadi wakubwa. Mugabe akaishia kuwa mwizi na mbabe. Nini kifanyike?
 
Kikwete, ataipeleka Tanzania Kanani, Nchi ya Maziwa na Asali..
waliokuwa wanaimba huo wimbo were the one calling for his head at the end of his tenure.
Magulifu,kila wimbo ukaimbwa.. Wakasema"Huyu ndiye ataitransform Tanzania to El Dorado". . 😁😁
Wote ni mashahidi, mbali na kuvuruga uchumi katengeneza Ombwe la viongozi, sasa uwzo wako wa kusifia ndiyo utaamua wewe uwe Nani ndani ya Tanzania.
Sass yupo huyu Bibi!! NASEMA HAKUNA LOLOTE.
 
Ubatili mtupu
 
Back
Top Bottom