Ukimchagua anayetumia mbinu za udanganyifu kupata kura ataendelea kudanganya hata akiwa madarakani

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Moja ya mambo yanaoangamiza mataifa mengi ni ukosefu wa viongozi thabiti kwani viongozi wengi hasa wa Bara la Afrika hupatikana kwa njia ya udanganyifu kama wizi wa kura, kunadi sera za uongo zisizotekeleka mbele ya wananchi ili kuwashawishi wawapatie madaraka.

Hata hivyo, pamoja na ubaya wa kumchagua kiongozi aliyetumia mbinu au njia za ulaghai kuweza kujipatia madaraka bado sehemu kubwa ya jamii haitambui athari wanayoweza kupata kwa kuwa na viongozi wa aina hiyo.

Wananchi wengi huishia kulalamika hali ya maisha kuwa ngumu mfano kupanda kwa gharama za maisha, kutokuwepo kwa miondombinu mizuri katika jamii, uchumi kudidimia na mengine mengi bila kujua chanzo ni kuwa na viongozi waliowapa madaraka kwa kukubali uongo wa viongozi hao wakati wa uchaguzi.

Mara nyingi viongozi wadanganyifu, na waliopata madaraka kwa njia za udanganyifu huwa na sifa zifuatazo katika uongozi wao.

Hawapendi kuhojiwa kwani wengi wao huwa hawana uwezo mzuri katika nafasi walizopo, kitu pekee wanapenda kusikia ni sifa hata kama haziwastahili, hivyo ukihoji unaonekana unataka kufichua uongo waliouficha kwa kuwa huendeleza uongo hata baada ya kushika madaraka.

Kauli zao huwa si za kweli hata baada ya kushika madaraka huendeleza kauli za uongo ili kuwadangaya wananchi wawaone ni bora hata kama wanaharibu
Siyo wawazi (Huficha taarifa)

Huwa Wala rushwa na mafisadi ili kufidia gharama walizotumia wakati wa kuwadanganya wananchi ili kuwalaghai wawape madaraka

Kupungua Kasi ya Maendeleo Maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kwani maendeleo yanahitaji uongozi thabiti, muwazi na muwajibikaji. Kiongozi asiye mkweli anaweza kusababisha kucheleweshwa au kupungua kwa kasi ya maendeleo kwa sababu ya sera dhaifu, maamuzi yasiyo sahihi au uvurugaji wa rasilimali kwani mara nyingi huwa na uwezo mdogo katika nafasi walizozishikilia

Huvuruga Utawala Bora kwani Uongozi mzuri unahitaji uwazi, uwajibikaji na uaminifu. Kiongozi asiye mkweli anaweza kusababisha kuvurugika kwa mifumo ya utawala bora kwani atakuwepo kwa ajili a maslahi yake tu na si jamii, atajikita kwenye rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na ukiukaji wa haki za binadamu.

Huua uhuru wa kujieleza, viongozi wadanganyifu wengi huua uhuru wa kujieleza ili kunyamazisha sauti za watu wanaotaka kujua taarifa, au wanatoa taarifa

Pia ni maadui wakubwa wa uhuru wa habari, viongozi wengi waliongia kwa njia ya udanganyifu wengi huwa maadui wakubwa wa uhuru wa habari, hudhibiti vyombo vya habari kuchapisha, kuhoji, au kufuatilia taarifa zozote za masuala ambayo wana maslahi nayo, watu hawa huwa maadui wa habari kabla na baada ya kuingia madarakani.

Wengi hununua waandishi ili waanike habari zinazowakuza kisiasa ikiwemo kuwasifia na kuwaandalia njia ya kupata tena nafasi kwa kuwalisha wananchi habari nzuri tu kuhusu wao.
 
Ni kweli kabisa, na wala siyo Afrika tu. Amerika nao wana sarakasi zilezile.

Tofauti tu ni kwamba wao wanafanya udanganyifu wa kiwango.

Siasa = udanganyifu (mostly!)
 
N
Moja ya mambo yanaoangamiza mataifa mengi ni ukosefu wa viongozi thabiti kwani viongozi wengi hasa wa Bara la Afrika hupatikana kwa njia ya wao.
asikia ccm wapo wanajifariji na matokeo ya haram wa chaguzi walizo fanya na ACT maana katika vyama vilivyo simama Angalau ACT unaweza wazungumzia

Sasa Bwana anasema ukifanyika uchaguzi wa kitaifa na kama utakuepo ccm mtaiona kila ragi mda mwalim
 
Moja ya mambo yanaoangamiza mataifa mengi ni ukosefu wa viongozi thabiti kwani viongozi wengi hasa wa Bara la Afrika hupatikana kwa njia ya udanganyifu kama wizi wa kura, kunadi .
Umesema ukimchagua !

Na nisipomchagua kwani atakubali ??
 
Moja ya mambo yanaoangamiza mataifa mengi ni ukosefu wa viongozi thabiti kwani viongozi wengi hasa wa Bara la Afrika hupatikana kwa njia ya wananchi habari nzuri tu kuhusu wao.
kuchagua vibaraka ni hatari na zaidi sana ni kuchagua utumwa 🐒

Hayuko mTanzania mzalendo achachagua makelele, malalamiko, ghadhabu na mihemko 🐒

Mipango madhubuti, dira na uelekeo wa sera nzuri zitakazo simamiwa na watu makini, mahiri na wanao aminika kitaifa na kimataifa 🐒

wanasingizia wengine ni wadanganyifu, hali yakua wao ni waongo wazoefu wanaofahamika 🐒
 
Back
Top Bottom