Elections 2010 Waliopiga kura Oktoba 31, milioni 12 walienda wapi Jumapili ile?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,343
39,013
Walioandikishwa kupiga kura ni milioni 19

Waliopiga kura (turn out) ni milioni 8.6

Kikwete kapata kura milioni 5.2

Slaa kapata kura milioni 2.2

Katika chaguzi kuu kumi zilizopita hatujawahi kuwa na waliojitokeza kupiga kura chini ya asilimia 70, HAIJAWAHI KUTOKEA. Asilimia 70 ya milioni 19 ni watu milioni 13.3

Mwaka huu waliojitokeza (kuanzia saa kumi alfajiri sehemu nyingine) ni asilimia 42.84.

Ina maana karibu watu milioni 12, hawakupiga kura Jumapili ile kwa sababu mbalimbali. Naomba tutoe sababu ambazo zingeweza kuwafanya watu wasipige kura na makisio ya idadi ya watu waliokumbwa na sababu hizo kitaifa tuone kama tunaweza kufikia watu milioni 12.

Unafikiri wale wote waliopiga kura uchaguzi huu uliopita wakiitwa wajitokeze au kuhesabiwa idadi yao itakuwa karibu na 13.3 au na 8.6?

NB: Kuna idadi ya watu milioni 4 wamepungua kutoka kura za Kikwete 2005 na 2010; na kuna watu milioni 4.7 wanapungua kutoka makisio ya asilimia 70 ya waliojiandikisha kulinganisha na wale tulioripotiwa wamepiga kura. WHAT HAPPENED?

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,780
4,415
Waliojiandikishwa ni milioni 19

Waliopiga kura (turn out) ni milioni 8.6

Kikwete kapata kura milioni 5.2

Slaa kapata kura milioni 2.2

Katika chaguzi kuu kumi zilizopita hatujawahi kuwa na waliojitokeza kupiga kura chini ya asilimia 70, HAIJAWAHI KUTOKEA. Asilimia 70 ya milioni 19 ni watu milioni 13.3

Mwaka huu waliojitokeza (kuanzia saa kumi alfajiri sehemu nyingine) ni asilimia 42.84.

Ina maana karibu watu milioni 12, hawakupiga kura Jumapili ile kwa sababu mbalimbali. Naomba tutoe sababu ambazo zingeweza kuwafanya watu wasipige kura na makisio ya idadi ya watu waliokumbwa na sababu hizo kitaifa tuone kama tunaweza kufikia watu milioni 12.

Unafikiri wale wote waliopiga kura uchaguzi huu uliopita wakiitwa wajitokeze au kuhesabiwa idadi yao itakuwa karibu na 13.3 au na 8.6?

NB: Kuna idadi ya watu milioni 4 wamepungua kutoka kura za Kikwete 2005 na 2010; na kuna watu milioni 4.7 wanapungua kutoka makisio ya asilimia 70 ya waliojiandikisha kulinganisha na wale tulioripotiwa wamepiga kura. WHAT HAPPENED?

SABABU KUBWA NI VISHAHADA VILINUNULIWA SANA, INGAWAJE WATU HAWATAKI KULIONA HILO.SURVIVAL YA UPINZANI NI KUWA WATU WENGI WALIKUWA NA SHAHADA HIVYO CCM WAKASHINDWA KUTARGET THE RIGHT ENEMY KATIKA KUNUNUA SHAHADA.HAPA MUSOMA TEAM YA CCM ILIKUWA INANUNUA SHAHADA KWA SH 10,000 USIKU, NA WENGI HASA WAZEE NA AKINA MAMA WALIUZA UKILINGANISHA NA VIJANA. kUONYESHA UKWELI JUU YA HILI MDOGO WAKE NA KATO MGOMBEA UBUNGE KYERWA KARAGE KUPITIA CHADEMA HAKUPIGA KURA NA ALIPOULIZWA NYUMBANI AKASEMA AMEPOTEZA SHAHADA LAKINI KATIKA KUFUATILIA IKAGUNDULIKA KUWA ALIUZA SHAHADA KWA SH 5,000. HILI SUALA LA SHAHADA KUNUNULIWA LIFANYIWE UCHUNGUZI ZAIDI LAKINI NDO SABABU KUBWA IMECHANGIA UPUNGUFU WA WAPIGA KURA

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,343
39,013
Unafikiri kati ya waliojiandikisha milioni 19 ni wangapi waliuza shahada zao, kwa bei ya 5000 kwa shahada unafikiri ni watu wangapi waliuza shahada zao katika nchi nzima? rusha namba yako yoyote tu.. watu kama milioni 2, 4 au laki kadhaa? give me your generous estimates.

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,723
Kati ya changuzi nilizo wahi kuzifatilia za mwaka huu ziliombewa sana mpaka watu wakajenga hofu kwamba huko kwenye vituo itakuwa vita tu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,343
39,013
Hili analosema Kimla lilikuwa limeenea kiasi gani kwa nchi nzima? Maana sidhani kama linaweza kuwa projected kwa nchi nzima au kuwa limetokea katika nchi nzima pasipo mtu hata mmoja kukamatwa akiuza au kununua shahada.

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
13,244
14,358
Ingawa shahada ziluzwa, bado watu wengi sana walipiga kura kuliko kawaida. To the least, kulikuwa na turnout isiyopungua 65%. Nina imani kuwa hesabu kamili ya wapiga kura haikutolewa kwenye majumuisho, ndiyo maana leo tunasikia jimbo la vunjo kura zinaongezeka. Kuna majimbo mengi sana ambayo kulikuwa na uharibifu wa makusudi wa kura.

Inabidi ndugu zangu tujitafutie utaratibu mpya wa kupiga kura; baadhi ya mapendekezo yangu ni:

(a) Kuharamisha opotezaji shahada ya kura kusudi liwe ni kosa la jinai. Sambamba na hili kosa, iwe pia ni kosa la jinai kwa mtu kumsaidia mpiga kura kupoteza shahada yake ya kupigia kura ikiwa ni pamoja kununua shahada hizo. Vile vile iwe ni kosa la jinai kwa mtu kumiliki shahada isiyokuwa yake.

(b) Kuharamisha uzembe wa kutopiga kura bila sababu ya maana ili pia liwe ni kosa la jinai (kama ilivyo Australia na New Zealand)
(c)Kuwa na masanduku mawili ya kura: sanduku la kura halisi linalokaa ndani ya chumba cha kura, na sanduku la vishina litakalokuwa sehemua ya wazi. Daima lazima hesabu ya masanduku hayo mawili ikubaliane wakati wote...........( I may have to think further on this proposal).

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,343
39,013
Kichuguu.. lakini waliojitokeza kupiga kura ni milioni 8.6 kati ya milioni 19? what happened to more than 10 million people.

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Hili la 2010 limeshapita, kilichobaki ni kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015, ni wakati muafaka kwa wanasiasa hasa vyama vyenye nia ya dhati ya kuiletea maendeleo nchi hii kuwahamasisha watu hasa vijana ambao wamefikia umri wa kupiga kura kujiandikisha kupiga kura.

Ninaamini chama changu cha CHADEMA kitakuwa mstari wa mbele kuwahamasisha jamii hasa vijana, mimi binafsi nilishaanza hii kazi ya kuwahamasisha vijana.

Silas A.K

JF-Expert Member
Apr 23, 2008
807
153
Ingawa shahada ziluzwa, bado watu wengi sana walipiga kura kuliko kawaida. To the least, kulikuwa na turnout isyopungua 65%.

Nina imani kuwa hesabu kamili haikutolea, ndiyo maana leo tunasikia jimbo la vunjo kura zionaongezeka. Kuna majimbo mengi sana ambayo kulikuwa na uharibifu wa makusudi wa kura.

Inabidi ndugu zangu tujitafutie utaratibu wetu wa kupiga kura. baadhi ya mapendeklezoa yangu ni:

(a) Kuharamisha potezaji shahada ya kura kusudi liwe ni kosa la jinai.

(b) Kuaharamisha uzembe wa kutopiga kura bila sababu ya maana ili pia liwe ni kosa la jinai (kama ilivyo Australia na New Zealand)

(c)Kuwa na masanduku mawili ya kura: sanduku la kura halisi linalokaa ndani ya chuma cha kura, na sanduku la vishina litakalokuwa sehemua ya wazi. Daima lazima hesabu ya masanduku hayo mawili ikubaliane wakati wote...........( I may have to think further on this proposal).

Mkuu Kichuguu,hii proposal yako kama kuna viongozi wa vyama makini watai-note na kuipendekeza wakati tutakapofanya mabadiliko katika taratibu zetu za uchaguzi. Hii ni control nzuri sana japokuwa nayo bila ku-revamp muundo wa NEC haitaweza kusaidia.

Ilulu

Senior Member
Mar 22, 2008
161
29
Mimi naona tangia mwanzo wa zoezi zima kumekuwa na Deliberate Exaggeration ya namba ya wapiga KURA. Ikumbukwe mwanzo NEC ilisema waliojiandika kupiga KURA ni 19+mil na wakati wa kutangaza ikaja kuwa ni 20+mil.
Naungana na wenzangu hapo juu kuwa kadi a kupiga KURA this time zilinunuliwa sana na si kwa ajili ya kwenda kupigia kura bali kuziondoa katika mzunguko wa kupigia kura hasa Upinzania na ikilengwa wagombea wa CHADEMA.
Hata hivyo nashindwa ku-conclude kuwa uhaguzi wa mwaka huu watu wengi hawakujitokeza kupiga KURA. Mahali ninapoishi mimi na nilipopigia KURA watu walijitokeza sana na hasa muda wa asubuhi, ni kama vile kila mtu alitamani kuitumia haki yake ya kupiga mapema iwezekanavyo na kisha kurudi nyumbani.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,343
39,013
Mimi naona tangia mwanzo wa zoezi zima kumekuwa na Deliberate Exaggeration ya namba ya wapiga KURA. Ikumbukwe mwanzo NEC ilisema waliojiandika kupiga KURA ni 19+mil na wakati wa kutangaza ikaja kuwa ni 20+mil.
Naungana na wenzangu hapo juu kuwa kadi a kupiga KURA this time zilinunuliwa sana na si kwa ajili ya kwenda kupigia kura bali kuziondoa katika mzunguko wa kupigia kura hasa Upinzania na ikilengwa wagombea wa CHADEMA.

Unafikiri kwa nchi nzima ni kama watu wangapi waliuza shahada zao?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
43,604
95,520
Hili la 2010 limeshapita, kilichobaki ni kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015, ni wakati muafaka kwa wanasiasa hasa vyama vyenye nia ya dhati ya kuiletea maendeleo nchi hii kuwahamasisha watu hasa vijana ambao wamefikia umri wa kupiga kura kujiandikisha kupiga kura.

Ninaamini chama changu cha CHADEMA kitakuwa mstari wa mbele kuwahamasisha jamii hasa vijana, mimi binafsi nilishaanza hii kazi ya kuwahamasisha vijana.
Mungi, ndio maana tuna soma la historia, lengo sio tuu kujua Mangi Meli, Sina na Marealle walifanya nini au kulitokea nini, lengo ni kuangalia tulipotoka, kupima tulipo ili kujua tunakokwenda. Hivyo lazima tujue kimetokea nini na kwa sababu zipi watu hawakujitokeza?.

Kama walijiandika watu milioni 20, wakapiga kura watu milioni 8, watu milioni 12, hawakupiga kura, bila kujua sababu halisi zilizofanya hao watu milioni 12 wasipige kura, uchaguzi wa mwaka 2015, watajiandikisha watu milioni 25 ila watapiga kura mioni 5, na milioni 20 hawatapiga na mwishowe serikali itaamua, hakuna haja tena ya kuendelea kupiga kura kwani ni kujisumbua tuu, bora chama kilichoko madarakani, chenye hati miliki ya utawala wa Tanzania, kiendelee tuu kutawala milele!.

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
Wale milioni 12 sehemu ya kubwa ilipiga kura, lakini ili kumpa JK ushindi wa kifisadi, NEC walichakachua ikaonekana hawakupiga kura!!!!!!!!!!!!!! Nguvu ya uhamasishaji kwa uchaguzi wa 31.10.2010 ni kubwa kuliko zote katika historia ya taifa letu. Idadi ya waliojiandikisha na kujitokeza inatisha!!!!!!!!!!!!!! Tatizo ni mbinu za kifisadi zilizotumika katika hatua ya kujumlisha matokeo. Ushahidi wa mbinu hizo chafu ni jinsi tume ya makame na kiravu walivyofanya usiri hata kwa waangalizi wa kimataifa kuzuiliwa kushudia aggrgegation-subiri ripoti yao itoke utaona maajabu haya!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Siyo siri kwamba demokrasi ilinyongwa kwa teknik ya mugabe/kibaki style!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Jibu ni pipooooooooooooos pawaaaaaaaaaaaa tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kichakoro

JF-Expert Member
Sep 10, 2008
2,740
4,531
Sababu ni kama ifuatavyo

Waliokufa tangu daftari liliporekebishwa 300,000
Waliokua wagonjwa siku ya kupiga kura 400,000
waliokua safarini (ndani na nje ya nchi) 150,000
walikosa majina yao kwenye daftari 2,000,000
waliopoteza/uza shahada zao 700,000
wanachama wa ccm waliokataa kupiga kura 800,000
watanzania wazembe waliokataa kupiga kura 500,0000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,343
39,013
Hivi kwanini tusiitishe siku moja kuwa wote waliopiga kura waje kuhesabiwa (reverse counting) tuone kama namba yetu itakaribia milioni 8.6 au milioni 13

Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
64
MM,
kwa kiasi fulani kulikuwa na duplication kwenye hiyo orodha. Siamini kama watu wotwe waliokufa baada ya 2005 walifutwa kwenye daftari, hii ni kutokana na ukweli kuwa watanzania wengi ni rahisi kufatilia vyeti vya kuzaliwa ila si vya kifo. Kwa hiyo hata marehemu hawakuripotiwa wafutwe, kwahiyo walijumuishwa kwenye hiyo orodha.

Jambo lingine klilichongangia kufanya idadi ionekane kubwa, ni "wapiga kura feki" nyinyi wenyeqwe mnakumbuka humu jamvini kulikuwa na zile namba ambazo hazikuwa na details kwa maana ya majina, bali zilionekana ziko vituo fulani fulani na hizi pia zilijumuishwa kwenye hiyo listi. Pia wale mliokuwa mnafatilia matukio ya siku ile ya uchaguzi, James Mbatia aliwaonyesha waaandishi wa habari kadi iliyokuwa na jina na namba isipokuiwa haikuwa na picha, kwa hiyo hizi ni kadi za namna hii zilikuwa nyingi sana na kuongeza idadi ya wapiga kura hewa. Hawa wote walionekana hawakijitokeza kupiga kura.

Pia ile hofu waliyokuwa nayo wananchi siku ya kupiga kura iliongeza idadi ya wale waliokaa nyumbani na hawakwenda kupiga kura.

Sababu nyingine ni wananchi ambao hawakupiga kura kwa sababu ya kukosa majina yao vituoni kwa kuwa inawezekana kabisa majina yao yalipelekwa vituo vingine kimakosa bila ya wao kujua majina yao yako wapi. Mfano halisi ni jamaa yangu ambaye hakupiga kura kwa sababu hakukuta jina lake kituoni na nilipomchekia kwenye mtandao nililiona jina lake liko kwenye kituo kingine cha mbali ambapo yeye pamoja na wenzake waliokuwemo kwenye hicho kitabu majina yao yalipelekwa kwenye hiko kituo kwa hiyo watu kama 30 na zaidi hawakupiga kura, hawa nao waliingizwa kwenye orodha ya wasiopiga kura, na kesi za namna hii zilikuwa nyingi sana. Jambo la maana hapa nafikiri ni majina yawe yakibandikwa vituoni mwezi mmoja au miwili ili kila mtu awe na muda wa kutosha kuhakiki jina lake, na kuripoti wale marehemu walioorodheshwa kimakosa.

Binafsi naamini turn out ya mwaka huu ilikuwa ni kubwa kuliko ya mwaka 2005, ila imeonekana turn out kuwa ndogo kwa sababu ya idadi "feki" ya NEC, nimeconclude idadi ya NEC ilikuwa ni "feki" kwa ushahidi wa hapo juu

Ikimita

JF-Expert Member
Oct 23, 2010
300
20
Mkuu mimi naona sababu kama nne hivi.

Kwanza, nakubaliana na mchangiaji wa kwanza kwamba shahada ziliuzwa au kuhodhiwa na baadhi ya wagombea wakidhani wanapunguza kura za watu ambao wanadhani hawatawachagua. Kadirio ni milioni 2.

Pili, baadhi ya watu hawakujitokeza kwa kukosa elimu ya kutosha ya mpiga kura. Hawa watu ukiwauliza kwa nini hawaendi kupiga kura watakuambia wao waende wasiende kiongozi atapatikana, wanategeana. Kadirio ni milioni 5.5.

Tatu, hili kundi la watu ambao hawakujitokeza kwa kuchoshwa na hali kwamba hapatakuwepo mabadiliko. Mawazo yao ni kwamba hata kama wakiamua kumpigia mtu mwingine kura bado mgombea wa CCM ndiye atashinda. Kadirio milioni 4.

Nne, hawa hawakujitokeza kwa dharura mbali mbali ama kuondoshwa kwa makusudi kwenye maeneo ambayo walijiandikisha kama vile wanafunzi wa vyuo, maaskari na wengineo. Kadirio ni milioni 0.5.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,343
39,013
Sababu ni kama ifuatavyo

Waliokufa tangu daftari liliporekebishwa 300,000
Waliokua wagonjwa siku ya kupiga kura 400,000
waliokua safarini (ndani na nje ya nchi) 150,000
walikosa majina yao kwenye daftari 2,000,000
waliopoteza/uza shahada zao 700,000
wanachama wa ccm waliokataa kupiga kura 800,000
watanzania wazembe waliokataa kupiga kura 500,0000

nimejumlisha kwa kichwa tu hapa inanipa milioni 4.85.. tukiwafuta hao wote tunabakia bado na kama milioni 14.25 .. inabidi uongeze idadi wengine wa kuwafuta ni kiasi gani na kina nani?

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
966
529
Kichuguu.. lakini waliojitokeza kupiga kura ni milioni 8.6 kati ya milioni 19? what happened to more than 10 million people.

mwanakijiji hao millioni 8.6 ni wale tuliotangaziwa na tume. Na ukweili hautajulikana kwa maana tume inalindwa na katiba feki ya Tanzania kuwa hakuna atakayehoji kazi ya tume mahali popote.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom