Matokeo ya Urais DR Congo kutangazwa Jumapili (Desemba 31, 2023)

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
Matokeo ya uchaguzi wa urais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yanatarajiwa kutangazwa kesho kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume ya uchaguzi, huku ushindi ukitarajiwa kwa Rais aliye madarakani Felix Tshisekedi.

Takriban watu milioni 44 walijiandikisha kupiga kura Desemba 20 katika uchaguzi uliokumbwa na sintofahamu kwa kuchagua rais, wabunge wa kitaifa na wa kikanda na madiwani wa manispaa.

Kati ya kura milioni 15.9 zilizohesabiwa kufikia jana Ijumaa Desemba 29, Tshisekedi alikuwa anaongoza kwa asilimia 73 ya kura katika taifa hilo la Afrika ya kati.

Upigaji kura uliongezwa siku moja, lakini uliendelea kwa muda mrefu zaidi katika baadhi ya maeneo ya mbali.

Mkuu wa tume ya uchaguzi, Denis Kadima, aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa kwamba matokeo kamili ya muda yatatangazwa Desemba 31.
 
Back
Top Bottom