Waliopewa dhamana ya kutunza mikataba ya Siri ya rasilimali za nchi wamenyimwa dhamana yakushiriki majadiliano kabla ya mikataba

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Tanzania ni nchi pekee ambayo wanaotunza nyaraka za mikataba nyeti ya rasilimali za nchi siyo sehemu ya majadiliano na uandishi wa mikataba hiyo. Hivyo waliopewa dhamana ya kuhifadhi nyaraka hizi wamevaa nafsi ya uadilifu lakini wanachohifadhi hakina uadilifu.

Kwa mantiki nyingine mahali patakatifu pamefanywa sehemu ya kuhifadhi najisi. Labda niiweke katika muktadha huu.
Ukiona nchi inapeleka mkataba mahakama ya Kimataifa na mkataba huo ukatumiwa kama ushahidi wa kujibu hoja za nchi husika lakini baadaye hukumu ikatoka inayosomeka kwamba mkataba ulioingiwa umevunja misingi ya makubaliani au protocol za Kimataifa basi utagundua endapo muhifadhi wa mkataba angeulizwa ana hifadhi ya nyaraka ngapi zakutumika kufanya majadiliano may be angewawekea mezani hoja za kuwasaidia kujadiliana na kufikia hatua ya mikataba isiwe weza kudhuru nchi.

Mikataba mingi inasainiwa Kwa mwanasiasa kukaa na wataalamu na kufikia muafaka na siyo wataalamu wa serikali kukaa na wataalamu wa nje kufikia muafaka.

Mikataba mingi inaingiwa kijamaa kwamba Marekani ni marafiki zetu au China ni marafiki zetu au Italy ni marafiki zetu na siyo Kwa kuzingatia sheria.

Mikataba mingi ni Siri na uanzia nje ya nchi na kumalizikia huko, nayasema haya nikitaka kuwauliza mawaziri wetu wanaposaiini mikataba au makubaliano nje huwa majadiliano yamefanyika ndani au anapoona fursa hapo hapo umwaga wino?

Natabiri mashtaka mengi huko nje, natambua juhudi zinazoendelea za kutatua migogoro iliyotengenezwa awamu ya Tano. Lakini jinai au uvunjaji wa Sheria hauna Siri.

Tujifunze kuwaachia wataalam watunza Siri na nyaraka waingie kwenye majadiliano Kwa sababu wao wameingia mkataba wakufikisha miaka mitano ninyi mnaingia mkataba wa miaka mitano mitano.

Katiba muhimu
 
Tangu nchi hii kuumbwa kwake mikataba imekuwa ikikubaliwa na watawala tu inasainiwa. Ilianza tangu enzi za chifu Mangungo kwa wajerumani mpk leo.
 
Back
Top Bottom