Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Vijana waandamana jijini Dar es Salaam Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari wamekamatwa eneo la Mnazi Moja.

Maandamano Bandari.jpg

========

WALIOANDAMANA WAISHIA MIKONONI MWA POLISI

Taarifa za awali zinaeleza kuwa vijana waliokuwa wameandamana kupinga Mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Mmoja kuelekea Ikulu ya Magogoni Dar es salaam wamekamatwa na Jeshi la PolisiTaarifa zaidi zitawajia endelea kutufatilia.


MRATIBU WA MAANDAMANO AINGIA MITINI

Jeshi la Polisi limewakamata baadhi ya vijana waliojitokeza kuandamana kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo, a mratibu wa maandamano hayo, Deus Sokkatika hali ya kutofahamika, hajatokea kwenye maandamano hayo yaliyopangwa kuanzia Temeke na kuishia Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Mwananchi Digital ilipomtafuta kwa simu zake zote za kiganjani, hakupatikana na katika majina ya waliokamatwa na polisi pia jina lake halikuwepo.

Juni 15 mwaka huu Deus Soka ambaye aligombea udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, alitangaza kuitisha maandamano kupinga mkataba wa ushirikiano wa uendeshaji wa bandari kati ya Kampuni ya DP World na Tanzania.

Hata hivyo Juni 17 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likipiga marufuku maandamano hayo na kueleza kuwa, mtu aliyeandaa maaandamano hayo ameshajibiwa kwa barua akielezwa ni marufuku kufanyika maandamano yoyote.

Juni 10, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha azimio kuhusu pendekezo la kuridhiwa kwa mkataba baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kwa lengo la kuanzisha ushirikiano katika uendelezaji wa maeneo ya bandari nchini.

Pendekezo hilo liliwasilishwa bungeni Juni 10, na kupitishwa na Bunge baada ya wabunge kupata fursa ya kuchangia na kuishauri Serikali kuhusu mkataba huo.


Mwananchi

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
  2. - Vijana kufanya Maandamano kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai
  3. - Polisi yapiga marufuku maandamano ya kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam, Jumatatu Juni 19, 2023
 
Nguvu ya Umma ijitokeze kwa namna zote kupinga maeneo ya Tanganyika kugeuzwa makoloni ya mabeberu

19 June 2023
Dar es Salaam, Tanzania


Vijana walioandamana jijini Dar es Salaam kupinga mkataba wa Bandari eneo la Mnazi Moja wame kamatwa na jeshi la polisi
 
HABARI ZA HIVI PUNDE
Vijana waliotangaza maandamano, leo wameandamana jijini Dar es Salaam #Tanzania kupinga mkataba wa bandari kati ya serikali na Dubai Ports World pamoja na muswada wa marekebisho ya sheria ya Usalama wa Taifa.

View attachment 2662134
Wawe vijana kweli SASA!

Sio wawe wale jamaa pekee halafu wawaite vijana!!
 
Tukiondoa uoga, kujipendekeza na unafiki,tunaweza kuionesha serikali kuwa Tanzania hii siyo ile ya Nyerere.

Hii ni Tanzania iliyochangamka, ni Tanzania inayojua nini inahitaji.

Cha msingi ni kuwa na umoja,
(Unit is power) na dhamira ya kweli.

Nguvu ya umma ni zaidi ya risasi na mabomu.
 
Back
Top Bottom