Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Mtu keshabambikiziwa kesi hapo tayari

Mkuu hapo panaweza pakawa na ukweli maana hizo story zao hata hazieleweki, hoteli ya bei mbaya halafu mwizi awe anaweza kuingia kirahisi namna hiyo?????
 
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke

As if waliulizwa

Mmh interesting! Assume tunaamini wanachosema, kwahiyo huyo mama mdogo yeye sie mwizi? Yaani unaletewa mali zote hizo na watu huulizi au hushtuki. Kwanini wanauhakika aliyeiba sio mwanamke? Kwani walimuona mwizi? Na je hao watu waliowakamata (assume tuneamua kuwaamini) wakitaja mwanamke ameshiriki itakuwaje? Unatoaje conclusion kabla hujamaliza uchunguzi? Kumkamata mtu sio hoja; maliza uchunguzi ndio uje na kitu concrete. Polisi wakikimbilia kutoa conclusion kwaajili ya kufanya damage control ndio wanaharibu kabisaaa. Kama walivyosema members wengine; kama mtu ulikuwa huamini watu wanayosema sasa ndio unaaza kuelekea ule upande wa kuamini. Jinsi Malima na wenzie wanavyojitahidi kujisafisha naona ndio wana-haribu. Mi ningemshauri amalizane na mke wake tu then akae kimya asipate pressure. Sidhani kama JK anaweza akamfanya chochote maana na yeye ana akili hizo hizo za Malima.
 
Humu Tanznaia tumezoea kuwaona masikini wakinyanyaswa kwa mambo ambayo hayaeleweki huku Mafisadi wakubwa ndio wanalindwa na dola. Namuomba Adam Malima awaangalie hawa vijana na huyu mwanamke wanavyopigwa, ajiulize moyoni kama kweli walimwibia. Kuna tetesi kwamba alikuwa na mwanamke ndiye aliyemwibia. Adam tunaona uangalie hizi picha.Hawa vijana wana familia zao, wana watoto ambao wanateseka wazazi wao wakiteswa, ila hawana pa kukimbilia. Wanalia majumbani mwao!

Uislamu unatufundisha haki, ukristo nao vilevile...........Tunaomba jibu kama haukutoka klabu na mwanamke mweupe mrefu..... Zaidi ni kwamba Mungu anayaona machozi yao yanayolilia haki. Kuwa na nguvu ya dola siyo sababu ya unyanyasaji, watendee masikini jinsi unavyoitaka haki. Hawana nguvu isipokuwa Mungu ndio nguvu yao. Ngoja wateswe na hata kuuwawa kulinda cheo chako. Ndugu yangu Adam, Naomba uangalie hizi picha kwa umakini, ukiona ukweli ndani yake naomba ukwel ukuguse moyoni mwako kwani sote dunia ni mapito yetu ila hakuna sababu ya kuwapa watu wasio na hatia mateso. Wewe na serikali yako mmekuwa watawala waonevu. Mungu Akupe Nguvu. Wasamaa kama kweli walikuibia, kama hawakukuibia basi uwaangalie usoni na maumivu wanayoyapata kisha uwaombe radhi Amina................!!!!
IMG_7297.jpg

IMG_7300.jpg

malima11.jpg
 
Polisi wa Tanzania Hawaaminiki kwa sababu wameashafanya yafuatayo bila mfumo kutathminiwa
1. Wameua raia ili kuwapora mali (kesi ya Zombe)
2.Wamekanusha Mwakyembe hakupewa sumu kwakutumia taarifa ambazo hazithibitishwa na wataalamu (taarifa ya Manumba)
3. Wamgi wao ni wavuta bangi RPC wa Wa Tabora wakati akitoa ushahidi dhidi ya Zombe aliyekua bosi wake alimwambia "usituletee bangi zako hapa". Hii ni uthibitisho kwamba kuna viongozi wa nyasi za juu polisi ambao ni wavuta bangi.
 
Du hii kali huyu Dada Chialo anajua kupika stori balaa. SMG alizitaja mwenyewe Mh. Malima wewe Chialo ukanushe. Acheni kuhadaa wananchi jamani oneni aibu. Kuhusu vitu vya wizi kufichwa kwa mama mdogo wa mtuhumiwa kisheria hata mama mdogo ni mtuhumiwa sasa mbona kimya? Hapo mama Chialo ndipo uongo wako unapojulikana na hii ni kwasababu hukujiandaa kutudanganya.
 
Humu Tanznaia tumezoea kuwaona masikini wakinyanyaswa kwa mambo ambayo hayaeleweki huku Mafisadi wakubwa ndio wanalindwa na dola. Namuomba Adam Malima awaangalie hawa vijana na huyu mwanamke wanavyopigwa, ajiulize moyoni kama kweli walimwibia. Kuna tetesi kwamba alikuwa na mwanamke ndiye aliyemwibia. Adam tunaona uangalie hizi picha.Hawa vijana wana familia zao, wana watoto ambao wanateseka wazazi wao wakiteswa, ila hawana pa kukimbilia. Wanalia majumbani mwao!

Uislamu unatufundisha haki, ukristo nao vilevile...........Tunaomba jibu kama haukutoka klabu na mwanamke mweupe mrefu..... Zaidi ni kwamba Mungu anayaona machozi yao yanayolilia haki. Kuwa na nguvu ya dola siyo sababu ya unyanyasaji, watendee masikini jinsi unavyoitaka haki. Hawana nguvu isipokuwa Mungu ndio nguvu yao. Ngoja wateswe na hata kuuwawa kulinda cheo chako. Ndugu yangu Adam, Naomba uangalie hizi picha kwa umakini, ukiona ukweli ndani yake naomba ukwel ukuguse moyoni mwako kwani sote dunia ni mapito yetu ila hakuna sababu ya kuwapa watu wasio na hatia mateso. Wewe na serikali yako mmekuwa watawala waonevu. Mungu Akupe Nguvu. Wasamaa kama kweli walikuibia, kama hawakukuibia basi uwaangalie usoni na maumivu wanayoyapata kisha uwaombe radhi Amina................!!!!
IMG_7297.jpg

IMG_7300.jpg

malima11.jpg

Jamani msichukulie vibaya. Inauma sana watu wanaponyimwa haki yao waliyopewa na Mungu....
 
Polisi Tanzania wanaongoza kwa kubambikia kesi WATU wasio na hatia....Naamini hapa wanaendeleza mchezo wao. Sababu ni kwamba aliyeziona mali na kuziiba alikua ndani ya chumba na mwenye akili za "forensic investigation" angeanzia hapo. Polisi wetu wanaharibu hata mazingira ya kutafiti wanajaa kwenye tukio wanzunguka zunguka wakishangaa halafu wanambambikia Mtu kesi wanasepa....shame on them
 
Kaka haya madhambi yote yamrudie Malima. Sasa huyu mama alimwibia nini mpaka avuje damu? Adamu Mungu atakuadhibu. Unajua kabisa Changudoa ndiye aliyekuibia matokeo yake unambambikizia mama wa watu kesi ukitumia polisi... Shame on you. Hata msikitini ukienda kutubu mungu atokusamehe
 
ishu malima naomba inde ICC manake hawa wakulima wameonewa kabisa hata technlojia ya kufika hotelini naomba haki za binadamu wakawatetee...
 
Hawa ndio viongozi mliowachagua kwa mbwembwe! Wote wapo hivi hivi!
Walafi na wanataka imago wao ulikuwa kwa gharama kubwa hata ya manyanyaso kwa vijana wasio na hatia

Polisi wamesema vitu vilivuoibiwa vipo kwa allegedly mama mdogo wa one of the mtuhumiwa, mbona hawatuonueshi zaidi ya kuwapiga hao watuhumiwa?
 
... endapo ma-alosto wenzetu hawa hapa kwenye picha watakua wamebabatizwa tu kesi kiaina ili tu kuua shoo kwa Waziri Malima na aibu ya Morogoro (ilmradi tu aonekane kakamtwa mtu ili aibu yake ipate kugeuzwa) basi tusijali saaana maana yake ya Ukiwaona Mzuzuri wa Ditopile na mshahara wa maonevu tuliyashuhudia yakitokea katika mji huo huo kasoro bahari.

IMG_7297.jpg
 
Jamani tuwaze vizuri,Hivi hiyo hotel haina ulinzi,wigo,na hata kamera za cctv,maana chumba cha dola 400,SI MCHEZO,
 
Jamani tuwaze vizuri,Hivi hiyo hotel haina ulinzi,wigo,na hata kamera za cctv,maana chumba cha dola 400,SI MCHEZO,

Mimi ninachoombea ni haki. Huyu mama kakosa nini? mama wa miaka 40 na akumuibie Adam? CCM uonevu hadi lini?
 
Eee mungu, baba yetu wa mbinguni tazama wana wako na kuwatetea!
 
Nikianza kufikiria jinsi gani huyo bibi ajuza pengine jinsi gani alivyokwea ghorofa ya hiyo hoteni yenye chumba USD 400, bila mtu yeyote kumuona, mpaka akafika chumbani kwake na Malima akaanza kukomba kopyuta 4, pete za dhahabu na za urithi, kadi za benki ... na yote hayo ...

Mhe Malima hadi hapo kichwa kinaniuma kwani hii SINEMA mkanda haujaunganishwa vizuri ki-ufundi bora mrudi tena maabara mkaipe sura zaidi. Jamii ya Tanzania wala hatudanganyiki kitu hapa.

Jiuzulu kwa kuabisha serikali na ofisi ya umma, acha hizi mbichi kwa walalahoi hawa.

Jamani tuwaze vizuri,Hivi hiyo hotel haina ulinzi,wigo,na hata kamera za cctv,maana chumba cha dola 400,SI MCHEZO,
 
Inatia huruma, kama kweli Malima umeibiwa na changudoa na unajua hivyo walahi yatakurudi. Huyu mama kama kweli kakuibia sawa lakini kama hakukuibia angalia uso wake na ujutie nafsi yako.

IMG_7297.jpg
 
Jamani tuwaze vizuri,Hivi hiyo hotel haina ulinzi,wigo,na hata kamera za cctv,maana chumba cha dola 400,SI MCHEZO,

Mwanasheria kama Tundu Lissu anaweza kuwasaidia na kuwatetea bure.
 
Duh.. Cina cha kufanya zaidi ya kumuomba Mungu awasaidie hawa masikini ambao wako mikononi mwa Jeshi la Polisi.. Jeshi ambalo limejipambanua kama Jeshi katili kwa raia..
 
Back
Top Bottom