Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bibikuku, Mar 13, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Mali za waziri Malima zakutwa kwa ‘ma-mdogo’ [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 13 March 2012 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Fidelis Butahe
  KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

  Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

  Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

  Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

  Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

  “Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

  Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

  "Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

  Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

  "Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

  "Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

  Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

  Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.

  MY TAKE; KUNA KILA DALILI MWIZI ALIYEIBA SIO MZOEFU, LAZIMA ATAKUWA NI MWANAMKE NA NDIO MAANA AKAFICHA KWA MAMA MDOGO[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Boonabaana

  Boonabaana JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  A cooked story?
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mabwaku yaani mwizi aibe halafu akaviweke kwa mamake mdogo.sijawahi ona hii..
   
 4. Boonabaana

  Boonabaana JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  A cooked story?
  Send to a friend!
   
 5. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Obviously
   
 6. Boonabaana

  Boonabaana JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Fiction?
   
 7. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mbona hawajawataja majina?
   
 8. JS

  JS JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii haileti sense kabisa.Utakuwa ni mwizi kilaza vibaya mno uibe vitu vyote hivyo vyenye thamani kubwa ukafiche kwa mama mdogo? na bado huyo mwizi aendelee kubaki hapo Morogoro tu? hmmm:thinking:
   
 9. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyo mwizi atakuwa ni mara yake ya kwanza kuiba tangu azaliwe. Sina imani na huyu kamanda wa polizi kwa kauli za kukamatwa hawa watu
   
 10. Ishina

  Ishina Senior Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mchanga wa macho huo..!!:glasses-nerdy:!
  Naona anataka kujisafisha kwa nguvu kulinda ndoa yake na Kitumbua chake. Na bado mbona tutasikia mengi wiki hii
   
 11. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Wanajaribu kusafisha skendo.
   
 12. J

  John W. Mlacha Verified User

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  received
   
 13. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Alikuwa anajifunza kuiba! vp kuhusu smg naona kama maelezo ya kaimu kamanda yananichanganya huko mwisho.
   
 14. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,900
  Trophy Points: 280
  Malima kaka umeingia choo cha ..,e wajibika
   
 15. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Inaonekana alikuwa na bunduki kubwa lakini sio SMG, sasa ajabu alikuwa anaipeleka wapi hiyo bunduki????? Hajakanusha kuwa na bunduki ila amekanusha sio SMG
   
 16. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  wanamsafisha mamba kwa kutumia OMO
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  I will definitely reject this as a spam!
  I don't buy this story....
   
 18. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  yale yale ya mwakyembe. Kila mtu anaongea lake,mtu muongo daima anafahamika. Fuatilia maelezo yake,mwisho atajichanganya tu. Jamaa inaonekana kawaagiza wamsafishe ili ionekane hakuwa na kahaba,polisi wenyewe hawajajiandaa.
   
 19. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Biashara ya pembe za Tembo kwani ilishakwishaga?
   
 20. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  That's TRUE!
   
Loading...