Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Hii itamlipa Malima hapahapa duniani! Ushamba wake kukurupukia malaya bila kuwa na mbinu za ziada za kujilinda zinasababisha haki za binadamu kukiukwa. Yule malaya hawawezi kumkamata kuogopa ataweka mambo hadharani. Angalia huyo mama maskini ya Mungu anaweka hata kuisogelea Nashera hotel? Anaonekana ni ordinary mpika maadazi/chapati. Eee Mungu waokoe vijana hawa wasio na hatia, kosa lao pekee ni kuzaliwa katika nchi ambayo haki inanunuliwa na wanyonge wanabambikiziwa kesi. Malima is a winner kwani ndoa yake imesalimika, kazi iko salama, bao alipiga kwa yule malaya, SMG imetetea kuwa ilikuwa ni KABUNDUKI KA KAWAIDA tu sio SMG na mshahara mwezi huu atapata na posho. Wale walalahoi wanaozea lupango. JK anadai kuna utawala wa sheria/ haki ha ha ha haaa
 
Haki inapatikana mahakamani kwani mwizi hajaandikwa usoni
Hata hivyo hakuna kesi hapo, watayamaliza nje ya mahakama kuua soo
Changudoa kampiga halafu akawapa masela wazisukume
Hawezi kumkamata huyo changudoa ataharibu
 
Wamepigwa...
Watalazimishwa maelezo ya kukiri...
Halafu,Wote pia ni wanachama wa Magamba..
 
hivi huyu jamaa bado hajapata jina mbadala? Heshima yake imeshuka hawezi kuitwa adam malima ndani ya jf.
 
Wanaharakati nchini, kwa heshima zote, umma wa Tanzania tunawaombeni sana kutoa uwakilishi wenye utaalam wa hali ya juu KISHERIA kwa hawa ma-alosto wenzetu wanaoonekana KUHUKUMIWA kwa kipigo na kutokwa damu hata kabla hawajafikishwa mahakamani.

Vile vile muangalie ni madhara gani yatakua yametendeka kwa kitendo cha Global Publishers kuwandi hawa ma-alosto kama 'Wezi wa Malima' wakaati sheria inawapa watu hawa haki za kulindwa heshima zao bila kudhalilishwa kihivi na hata kupata kuhukumiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwahamisha kwa makusudi kutoka katika kundi la 'WATUHUMIWA' hadi kundi lingine kabisa lisiloheshimika la 'WEZI WA MALIMAA'.


Mwanasheria kama Tundu Lissu anaweza kuwasaidia na kuwatetea bure.
 
Mimi ninachojua ni kuwa malima alichukua kichwa KAUMBA hawa wengine ni mkuficha aibu yake tu sijui wale wa mapokezi kwanini hawaelezei MALIMA aliingia na kichwa cha aina gani>>>>>>>>
 
Hakuna watakalofanya litakalobadili mawazo ya watu juu ya kilichotokea hotelini. Taarifa ya afande kwa ufupi badala ya kubadili mtazamo wa watu ndio umezidi kuimarisha mtizamo wa awali. So work done is zero, all in vain!
 
Everybody will be rewarded according to their deeds. We shall see it happening right here. God bless.
 
Mungu simama angalia wayu wako. ina maana kikundi kilivamia kuiba siyo? walijuaje kuwa kuna waziri kalala kwa hiyo hotel na alikuwa na mzigo wa kutosha ....kudadadek
 
JF Morogoro, tunawaombeni ufuatiliaji wa karibu sana juu ya Ma-Alosto wenzetu hawa na kuwatembelea mara kwa mara Rumande ili kutoa UPDATES kwa wakati kwa Umma wa Tanzania kujua nini kinachoendelea na taratibu zipi zifuate kunapo haja ya walalahoi kupata utetezi kwa walalahoi tulioko mitaani endapo itabainika kesi ni ya kuchonga.
 
Hii stori kweli naishindwa kuilewa. RPC anadai Malima hakukutwa na SMG wakati kwenye video akihojiwa na wahandishi wa habari aliulizwa habari ya hiyo bunduki akadai "kwani wananchi hawajui kuwa wao huwa wanapita huko maporini, je wakivamiwa?" This is very confusing....hata hivyo siwezi kushangaa maana uongozi kuanzia ngazi ya Taifa huwa wanawachanganya wananchi na stori zisizokuwa na miguu wala kichwa.
 
Malima unasikia kweli kilio cha WaTanzania wenzako humu na jinsi gani tunavyojua kufanya mchezo mchafu ili wewe ukajiokolee sura kwa jamii lakini kwa majonzi ya hivi viumbe dhaifu na masikini wasioweza kitu kosogelea ha kusogelea tu hako ka hoteli ya kifahari ulikofikia Morogoro???

Wengine hapa tuliwahi kumtaka Mhe Edward Lowassa AFANYE SALA YA TOBA lakini hakulizingtia hilo kwa wakati na wewe pia leo hii tunakuambia kwamba Uwaziri wako usiwe mateso na majonzi kwa WaTanzania walalahoi hivyo katubu leo na wala si baadaye kwa haya unayowafanyia huyu bibi na wajukuu wake hao.
 
Malima ndio picha halisi ya viongozi wa serikali tulionao kwa sasa.Magazeti makini yafanye uchunguzi wa kina wa habari hii na kuiweka hadharani ili jamii iwaelewe hawa viongozi waliowachagua kwa mbwembwe. Inahudhunisha sana raha zake zinawapa shida WaTZ maskini kupitia jeshi la polisi lisilo adilifu
 
Humu Tanznaia tumezoea kuwaona masikini wakinyanyaswa kwa mambo ambayo hayaeleweki huku Mafisadi wakubwa ndio wanalindwa na dola. Namuomba Adam Malima awaangalie hawa vijana na huyu mwanamke wanavyopigwa, ajiulize moyoni kama kweli walimwibia. Kuna tetesi kwamba alikuwa na mwanamke ndiye aliyemwibia. Adam tunaona uangalie hizi picha.Hawa vijana wana familia zao, wana watoto ambao wanateseka wazazi wao wakiteswa, ila hawana pa kukimbilia. Wanalia majumbani mwao!

Uislamu unatufundisha haki, ukristo nao vilevile...........Tunaomba jibu kama haukutoka klabu na mwanamke mweupe mrefu..... Zaidi ni kwamba Mungu anayaona machozi yao yanayolilia haki. Kuwa na nguvu ya dola siyo sababu ya unyanyasaji, watendee masikini jinsi unavyoitaka haki. Hawana nguvu isipokuwa Mungu ndio nguvu yao. Ngoja wateswe na hata kuuwawa kulinda cheo chako. Ndugu yangu Adam, Naomba uangalie hizi picha kwa umakini, ukiona ukweli ndani yake naomba ukwel ukuguse moyoni mwako kwani sote dunia ni mapito yetu ila hakuna sababu ya kuwapa watu wasio na hatia mateso. Wewe na serikali yako mmekuwa watawala waonevu. Mungu Akupe Nguvu. Wasamaa kama kweli walikuibia, kama hawakukuibia basi uwaangalie usoni na maumivu wanayoyapata kisha uwaombe radhi Amina................!!!!
IMG_7297.jpg


IMG_7300.jpg

malima11.jpg

Wakuu me nimefuatilia sakata ili la mh Malima kwa kweli nimebaki na maswali mengi kichwani,hata muda wa tokea tukio lenyewe litokee na upatikanaji wa watuhumiwa umekua mfupi mno,kama kweli jeshi la polisi lingekua na utendaji huu,basi haki ingekua inapatikana haraka sana na jeshi la polisi lingepata sifa kemkem!tahadhari yangu ni kua hawa watu isije kua wametolewa kafara wakati si wahusika,amini nawaambia Mungu atajibu haraka mno tena na pigo takatifu!tuombeane uhai
 
Naona paka wezi mnawatetea . Hawa si wamekamatwa na vile vitu vilivyoibiwa ? Mlitaka wasishikwe nini ? Kazi kwelikweli.
 
Ndio kazi ya polisi wa bongo ni kulinda maslai ya walionacho na voiongozi tu.
 
Humu Tanznaia tumezoea kuwaona masikini wakinyanyaswa kwa mambo ambayo hayaeleweki huku Mafisadi wakubwa ndio wanalindwa na dola. Namuomba Adam Malima awaangalie hawa vijana na huyu mwanamke wanavyopigwa, ajiulize moyoni kama kweli walimwibia. Kuna tetesi kwamba alikuwa na mwanamke ndiye aliyemwibia. Adam tunaona uangalie hizi picha.Hawa vijana wana familia zao, wana watoto ambao wanateseka wazazi wao wakiteswa, ila hawana pa kukimbilia. Wanalia majumbani mwao!

Uislamu unatufundisha haki, ukristo nao vilevile...........Tunaomba jibu kama haukutoka klabu na mwanamke mweupe mrefu..... Zaidi ni kwamba Mungu anayaona machozi yao yanayolilia haki. Kuwa na nguvu ya dola siyo sababu ya unyanyasaji, watendee masikini jinsi unavyoitaka haki. Hawana nguvu isipokuwa Mungu ndio nguvu yao. Ngoja wateswe na hata kuuwawa kulinda cheo chako. Ndugu yangu Adam, Naomba uangalie hizi picha kwa umakini, ukiona ukweli ndani yake naomba ukwel ukuguse moyoni mwako kwani sote dunia ni mapito yetu ila hakuna sababu ya kuwapa watu wasio na hatia mateso. Wewe na serikali yako mmekuwa watawala waonevu. Mungu Akupe Nguvu. Wasamaa kama kweli walikuibia, kama hawakukuibia basi uwaangalie usoni na maumivu wanayoyapata kisha uwaombe radhi Amina................!!!!
IMG_7297.jpg


IMG_7300.jpg

malima11.jpg

Mkuu hii ni Bonge ya advice...du, nadhani na watawala wengine nao waiangalie kwa kutumia picha hii... Mbona wezi wa EPA na RICHMOND, MEREMETA, Wezi wa Wanyama hatuwaoni ktk picha kama hizi?? Kwa kweli Jeshi la Polisi sina hamu nanyi.
 
Back
Top Bottom