Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Huu ni uongo mkubwa.
Hawa polisi wasipende kutudanganya maana vitu vilivyoibiwa ni mali ya malima wala hadaiwi na mtu yeyote.
Huyo mwizi hakunywa hata bia moja wala kuuza simu ni kkini macho tuwapuuze.
 
hata mimi nashindwa kuelewa vizuri kwa kuwa inaonekana hawa polisi wenyewe hawajaelewa wanacho kifanya.mara hakuwa na smg mara mwizi hakuiba bunduki aina ya smg nadhani pengine ni ile kauli inajidhihirisha kwamba uwongo siku zote hauwezi kuprevail.c raisi kuelewa utata huu there must be something behind the scene
 
no reality on the defence,ndoa baba ina gharama zake kamanda kisha vuta chake, ana deki kwa tambala lenye maziwa mgando.
 
Ndo kilichomuhamisha swahiba yake Dr Dau mjini na kuacha kazi zake na kwenda kupika unafiki huu
 
Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.


"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.



Ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu
Hapo anaongea nini na mwishoni anaongea nini
haiingii akilini kabisa ni mtu mmoja anaongea statement mbili kwa wakati mmoja

 
Nina maswali matatu tu,
1. Huyu naibu waziri alikuwa likizo? Mbona alibeba nguo nyingi sana kama ni safari ya siku chache tu!
2. Alikuwa na safari ya uwindaji ama alienda vitani? Inawezekana vipi usafiri na silaha mbili za moto (bastola na bunduki) kwa kujilinda tu?
3. Laptop tatu!!! Ndio utandawazi?
By the way huo ndio ukwasi wa viongozi wetu, just safarini una 23 milion wealth, nyumbani je?
Weee mutu unataka kumtembelea kiongozi usiku?
Shaullako huko utapambana na mitutu ya kitungulia ndege.
 
Hahahaaaaaaaa... Sina mbavu kwa hii hadithi ya Kamanda wa Polisi. Yani tamu sana kwa ku refresh mind.
 
Kwanini vitu visipatikane wakati Malima mwenyewe anajua alikuja na nani chumbani? Malima akubali tu wadada wa Morogoro wamemzidi maujanja yaishe. He should count himself lucky maana wangeweza kuzidisha dose akalala kwa siku tatu!
 
Naona kamanda anajaribu kulinda ndoa ya Malima.. Mkewa haelewi kitu... Ukisoma between lines za hiyo COOKED story utajiuliza yafuatayo... 1. Inakuwaje mwizi avunje dirisha la chumba cha HOTELI saa 10 usiku na mwenyewe AU walinzi wa hoteli wasisikie?... 2. Hiyo SMG alikuwa nayo au hakuwa nayo chumbani?.. Maana maelezo ya kamanda yanapingana yenyewe... 3. Huyo mwizi kapitaje maeneo ya hoteli bila kukamatwa na walinzi?... 4. Wakati dirisha linavunjwa Malima alikuwa wapi?... 5 ukifikiria kuhusu uwingi na ukubwa wa vitu vilivyoibiwa, mwizi huyo alikatizaje viunga vya hoteli hiyo bila kuonwa na walinzi?... 6. Malima, ni baada ya muda gani kupita ndo ukagundua umeibiwa?



Labda huyo mke wa malima naye awe mwanaasha. Hii skendo sio ya kupotezea kirahi rahisi namna hiyo.
 
malima.jpg
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Mali za waziri Malima zakutwa kwa ‘ma-mdogo’ [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 13 March 2012 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Fidelis Butahe
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

“Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.

MY TAKE; KUNA KILA DALILI MWIZI ALIYEIBA SIO MZOEFU, LAZIMA ATAKUWA NI MWANAMKE NA NDIO MAANA AKAFICHA KWA MAMA MDOGO[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

kumbe kaimu kamanda wa polisi hajui kutofautisha smg na silaha nyingine??
 
Gazeti la Mwananchi, kwishney wanachomtetea nini huyu Malima aliibiwa na machangudoa hili halina ubishi na haina haja ya kujitetea mbona hata watoto wadogo ukiwaambia hii habari wataelewa tu , kwani ni wangapi wanaibiwa kwa mtindo kama wake na ukifuatilia utakuja kusikia alikua na Mwanamke akawekewa madawa ya kulevya akaiibiwa

Mbona RPC hawatutajii majina ya Hao "majambazi " Kama Matukio mengine...?
 
hata mimi nashindwa kuelewa vizuri kwa kuwa inaonekana hawa polisi wenyewe hawajaelewa wanacho kifanya.mara hakuwa na smg mara mwizi hakuiba bunduki aina ya smg nadhani pengine ni ile kauli inajidhihirisha kwamba uwongo siku zote hauwezi kuprevail.c raisi kuelewa utata huu there must be something behind the scene

hakuna kitu kibaya kufanya kitu ambacho hata wewe mwenyewe hukielewi. na ndivyo wanavyofanya polisi wa morogoro
 
Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema "Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo"Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.


"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.



Ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu
Hapo anaongea nini na mwishoni anaongea nini
haiingii akilini kabisa ni mtu mmoja anaongea statement mbili kwa wakati mmoja


Duh mkuu umeniacha hoi kwa maneno haya ambayo ni sahihi kabisaaaaaa
 
Duh mkuu umeniacha hoi kwa maneno haya ambayo ni sahihi kabisaaaaaa

Ndo maana nasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu ulisema nini mwanzoni
Yaani ukisoma hapo juu anajichanganya yeye mwenyewe bila hata kujua
na mwandishi aliyemsikiliza naye hakujua kabisa kuwa mheshimiwa kashadanganya
 
Pole sana Malima, huna jipya... huyo mke laazima akunyime dudu for the whole week, wanawake mnasemaje??
 
Ndo maana nasema ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu ulisema nini mwanzoni
Yaani ukisoma hapo juu anajichanganya yeye mwenyewe bila hata kujua
na mwandishi aliyemsikiliza naye hakujua kabisa kuwa mheshimiwa kashadanganya

hapa aliyejichanganya ni kamanda... ukiangalia vizuri aya inayozungumzia uwepo wa SMG na bastola chumbani mwandishi anafafanua kuwa ni maelezo ya march 9...wakati ya kutokuepo SMG ni ya jana..labda cha mhim ni kutafuta maelezo ya polis ya tarehe tisa tulinganishe na ya leo kama yanaelekeana...kinyume na hapo polisi wanatumika.!
 
Back
Top Bottom