Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Kuna sheria kubwa kabisa kuliko sheria zote, hii ni sheria haki ya ukweli ambayo haihitaji hakimu wala ushahidi! inaitwa
"Law of Karma" ambayo malipo yake ni hapa hapa duniani!.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Mali za waziri Malima zakutwa kwa ‘ma-mdogo’ [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 13 March 2012[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Fidelis Butahe
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

“Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.

MY TAKE; KUNA KILA DALILI MWIZI ALIYEIBA SIO MZOEFU, LAZIMA ATAKUWA NI MWANAMKE NA NDIO MAANA AKAFICHA KWA MAMA MDOGO
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Manumba alikuwepo kwenye huo uchunguzi?mi siku hizi sina imani kabisa na jeshi la polisi maana na wao wameingia kwenye siasa kinachotokea kila uchunguzi ni cooked na uhalisia unafichwa
 
Kama wamepigwa huko ni kukiuka haki za binadamu. Wanaharakati wetu inabidi watoe tamko haraka juu ya hili. Vyombo vya dola havitakiwi kuwashambulia watu wakati hao watu hawako armed. Polisi wako mbele katika kukemea wananchi kujichukulia hatua za kisheria mikononi mwao sasa kama nao wanapiga basi ni kujichukulia aheria mkononi. Hiki kitendo kikemewe kwa nguvu.
 
nliitegemea haya yangetokea haraka sana

1. MALIMA ANGEFUNGUA KESI YA MADAI KWA HOTEL YA NASHERA HARAKA IWEZEKANAVYO KWA KUSHINDWA KUMHAKIKISHIA USALAMA WAKE NA MALI ZAKE,KWANI KAMA MWIZI AMEWEZA KUINGIA CHUMBANI KWAKE BASI ANGEWEZA PIA KUMDHURU AU KUMUUA KABISA........HII KESI NAOMBA MALIMA UIFUNGUE HARAKA SANA

2. WALINZI WA NASHERA WALIOKUA ZAMU SIKU YA TUKIO WALITAKIWA WOTE WAWE WASHAFUKUZWA KAZI NA TAYARI WAKO MAHABUSU KWA KUSHINDWA KUFANYA KAZI NA KUHATARISHA MAISHA YA MHESHIMIWA

3. MANAGER WA NASHERA ANGEKUA MDA HUU ANAISAIDIA POLISI(NADHANI WANA JAMVI MNALIELEWA VIZURI HILI NENO KUISAIDIA POLISI)

4. TUSINGESIKIA POROJO NYINGI ZA POLISI BALI TUNGESIKIA HABARI KUTOKA MAHAKAMANI KWANI HII KESI INGESHUGHULIKIWA HARAKA SANA

hakuna wa kunibishia kua kwenye hili tukio watuhumiwa ni

1. ADAM MALIMA
2. CHANGUDOA ALIYEMUIBIA
3. POLISI WANAOFICHA UKWELI
4. UONGOZI WA HOTEL YA NASHERA

wafuatao ningependa kusikia tamko lao
1. WANAHARAKATI
2. WATETEZI WA WANYONGE(CHADEMA)
3. TANGANYIKA LAW SOCIETY
4.WANANCHI WA MOROGORO WANAOJUA UKWELI WA TUKIO
 
Yaani walinzi hawakukamatwa kuisaidia polisi? Huu upelelezi wa aina gani? Kama kulikuwa na walinzi basi wao walikuwa wawe the first suspect. Wangekamatwa na kuhojiwa. Pia meneja naye alitakiwa ahojiwe pamoja na Mh. Malima mwenyewe
 
.......wabongo tumegeuzwa machizi, nani sasa anakuza stori kama sio malima mwenyewe alihojiwa na kukubali kuwa alikuwa na silaha hiyo pamoja na bastola na kudai kuwa ni mtaji tosha wa maisha kama wezi/mwizi angeziiba? haya achukue tu hizo laptop amwachie mwenzie vijipesa
 
Makubwa! CHADEMA ndio walimwambia Malimu akachukue changu????

Hv hyu ribosome ni injini nyuma au? Mgomo wa maDr Chadema, malima kachukua dada poa chadema, hata Ribosome akipata ngoma, chadema. Ila kura zikipigwa na watz kwa chadema ccm wanajihalalishia ushndi. Waachieni chadema nchi yao bana.
 
Story imetungwa na mtu aliyepelekwa kufanya kazi ya upolisi kwa sababu alikosa ajira inayo mfaa, yuko hapo kuganga njaa siku ziende- tunawaita akina "kamlete" atajufunza humo humo!
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Mali za waziri Malima zakutwa kwa ‘ma-mdogo’ [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 13 March 2012[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Fidelis Butahe
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

“Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.

MY TAKE; KUNA KILA DALILI MWIZI ALIYEIBA SIO MZOEFU, LAZIMA ATAKUWA NI MWANAMKE NA NDIO MAANA AKAFICHA KWA MAMA MDOGO[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Zombe amerudi kazini au?
 
This is the Boomerang! The way the ball bounces back! I really like this new Bongo movie.
 
Malima si shwari mpaka mfungo wa sala ya toba kwa na kuomba msamaha walalahoi wenzetu wa mkoa wa Morogoro na taifa kwa ujumla wetu. Hili lipo njiani na linakuja tena kwa kasi ajabu mkuu endapo hutofanya sala ya toba.
 
ukweli ni kuwa Malima kaibiwa zaidi ya hivyo alivyovitamka. Inamuwia vigumu kutamka hivyo vingine alivyoibiwa
 
ribu sana kuficha ukweli lakini ni wazi kuwa hata kule kuchelewa kwake kuognea na waandishi wa habari ilikuwa ni njia ya kupika ukweli ili jamaa asije akaumbuka kama waziri kukutwa na hiyo kashfa ya kuibiwa na mwanamke
 
Back
Top Bottom