Waliombeba Makonda wamtelekeza rasmi

Waliombeba Makonda wamtelekeza rasmi

Kati ya hili na la kuibiwa kura kwenye uchaguzi alilosema lowasa unahisi lipi lilitakiwa liendelee kuzungumziwa Sana. Au kati ya hili la CHETI na la maufisadi yaliyofanyika lipi ni kubwa... Kwanini Yale mengine hayana nguvu tena hata za kuhojiwa.. Huu ni upepo tu watu wamekosa cha kuwaza Ila yatakuja yenyewe..
Anzisha sredi to thatbeffect na fuatilia mwamko.
 
Kuna msemo wa kiswahili usemao hivi , URAFIKI WA KWELI NI KATIKA DHIKI NA FARAJA , hivyo ndivyo watanzania tulivyoambiwa na wazee wa zamani , kwamba kama mtu wako wa karibu unatakiwa uwe naye wakati wa shida na raha , kama mlikunywa pamoja basi pia si vibaya mkipigia miayo pamoja.

Sakata la Rc wa D'salaam aliyeonekana shujaa na kubebwa sana na clouds media , ambalo sasa limegeuka huzuni kuu , limenifundisha kwamba duniani hakuna rafiki wa kweli , Kwa sasa Clouds wameruka hatua mia , Makonda hatajwi tena kutwa mara 100 !

Wito kwa vyombo vya habari - kuweni makini sana na wanasiasa wa aina ya Makonda , mtapoteza kama wanavyopoteza wao , kuna miongozo imewekwa ya namna media zinavyoweza kufanya kazi .

Hakuna haja ya kujipendekeza kwa wanadamu , fuateni sheria na utaratibu wa halali tu .

Biblia takatifu imeandika kwamba AMELAANIWA AMTEGEMEAYE MWANADAMU .

amina sana. Yote mnayofanyia gizani mkijua hamuonekani ipo siku yataanikwa hadharani mbele ya umati na itakuwa aibu mbele yenu.
 
Hata faru Yona ukiachana na kutomtumbua hakuna chochote anachomsaidia kwenye hili sakata la ku zoom nyeti vya kitaaluma.
 
Kumbe anajifanya anapambana na dawa za kulevya kumbe ni mwizi tuh

Daudi bashite mwehu sana
kweli upepo umebadilika hongera sana mkuu umeamua kusimama as mtanzania kupigana na majizi,matapeli, walaghai bila kukiangalia chama chako hongera tena
 
Mwanaume mwenye vyeti halali na vya kwake alivyosomea hawezi kulia lia kama huyu, hii ni indicator kuwa ni kweli hana vyeti...
View attachment 482781
Hizo ni Hisia zako ni sawa na mimi NIWEKE picha ya makonda akicheka halafu NIKASEMA mwanaume asiye na cheti hawezi ku smile kama huyu. Simple Sana.. Labda uje na hoja nyingine
 
Siasa zinawafanya muwaze Hisia za ovyo. Unaona clouds hawana mambo mengine ya kuendelea nayo .. Makonda anabebwa na kutetewa na MUNGU na wakazi zaidi ya million 2-3. Na hii itaendelea Kwa kipindi chote
Appeal to the pity
 
MUNGU ni mmoja tu. MUNGU wako siku moja atajifunua na
Utaamini kwamba makonda yuko chini ya MUNGU ni suala la muda tu
Kwani yeye si alisema kuwa ni MUNGU wa DAR sasa unataka atetewe na Mungu yupi km kachukua madaraka ya MUUMBAJI
 
MUNGU ni mmoja tu. MUNGU wako siku moja atajifunua na
Utaamini kwamba makonda yuko chini ya MUNGU ni suala la muda tu
Kisa ameenda kulia kanisani kwa mchungaji anayemuamini ambaye ni binadamu km wewe ndio ulete porojo kuwa yuko chini ya Mungu. Embu niambie uliongea na huyo Mungu lini??
 
Utasubili sana, Makonda ndiye Mkuu wetu wa Mkoa wa Dsm, na tunamkubali sana, huo ukaskazini wako peleka huko huko. Makonda ni mchapa kazi ni mwelewa, ni jasiri. Tena nyinyi namluki tunawajua mnalipwa na huyo Manvi ili mpost uchuro humu jf. Kwendeni zenu.

Bwege nazi!!! Anakuwa na macho mawili ila haoni (if and only if you know what it means)
 
Kuna msemo wa kiswahili usemao hivi , URAFIKI WA KWELI NI KATIKA DHIKI NA FARAJA , hivyo ndivyo watanzania tulivyoambiwa na wazee wa zamani , kwamba kama mtu wako wa karibu unatakiwa uwe naye wakati wa shida na raha , kama mlikunywa pamoja basi pia si vibaya mkipigia miayo pamoja.

Sakata la Rc wa D'salaam aliyeonekana shujaa na kubebwa sana na clouds media , ambalo sasa limegeuka huzuni kuu , limenifundisha kwamba duniani hakuna rafiki wa kweli , Kwa sasa Clouds wameruka hatua mia , Makonda hatajwi tena kutwa mara 100 !

Wito kwa vyombo vya habari - kuweni makini sana na wanasiasa wa aina ya Makonda , mtapoteza kama wanavyopoteza wao , kuna miongozo imewekwa ya namna media zinavyoweza kufanya kazi .

Hakuna haja ya kujipendekeza kwa wanadamu , fuateni sheria na utaratibu wa halali tu .

Biblia takatifu imeandika kwamba AMELAANIWA AMTEGEMEAYE MWANADAMU .
Kwani kuleta maendeleo ni kutajwatajwa Redioni. We chapa kazi kwa wananchi, Igeni mfano wa Mly Nyerere aneacha alama nzuri sana. Sio ubingwa wa Kukaa zaidi mitandaoni halafu kulialia eti maisha magumu! Masaa yote mitandaoni unategemea nini jamani? Nilisoma historia ya mdada mmoja Milionea hakumbuki lini aliangalia TV!
 
Daaah, kweli Clouds huwa wanaboa sana aisee...mfano yule Hassan Ngoma kwenye 360 sijui naye ni bashite yule dah, maana siyo kwa kujikomba huko!
 
Kisa ameenda kulia kanisani kwa mchungaji anayemuamini ambaye ni binadamu km wewe ndio ulete porojo kuwa yuko chini ya Mungu. Embu niambie uliongea na huyo Mungu lini??
Maongezi ya Mungu huyafanya kwa vitendo si hivyo mmelalamaaaa weee sasa mko Arusha hebu jatathminini jamani muone kama mnautendea muda justice!
 
Utasubili sana, Makonda ndiye Mkuu wetu wa Mkoa wa Dsm, na tunamkubali sana, huo ukaskazini wako peleka huko huko. Makonda ni mchapa kazi ni mwelewa, ni jasiri. Tena nyinyi namluki tunawajua mnalipwa na huyo Manvi ili mpost uchuro humu jf. Kwendeni zenu.
Mwizi wa cheti, mwizi wa jina, mshirika kuu wa wababe wa unga, tapeli wa magari.
 
Kuna vitu vingine akiandika mwana ukawa unaona ni uharo tu!

Sasa Wewe ulitaka clouds wafanyaje labda?
 
Back
Top Bottom