Watangazaji Clouds wavunja rasmi "urafiki" na Makonda, sasa kutangaza habari bila maelekezo toka juu

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,865
Haikuwa desturi yangu sana kuangalia Clouds Tv,hii ni kwa sababu ya mambo fulanifulani,watoto wangu pia na wife hujua kuwa mimi sipendelei kituo hiki cha habari.Hata ninapokaa sebuleni kama wameweka channel hii,wao wenyewe huitoa.

Toka sakata la Makonda kuvamia,nimejipa muda kuangalia hii Tv,vipindi na nyimbo wanazopiga ni kama wanafikisha ujumbe kwa mkulu na RC wa Dsm.Wanapiga nyimbo za "vijembe" na leo wameimba wimbo wa "Solidality Forever" huku wameshikana mikono studio.

Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha "Clouds 360",nimesikiliza nukuu zilizotolewa na watangaji wote watatu, lakini nimefurahia zaidi nukuu ya pili ya mtangazaji Sam Sasali

"Kuanzia sasa nitasoma kila kitu, nitasoma kila gazeti liwe la michezo siasa na kila kitu sitaki kupangiwa, sitaki kupigiwa simu za maelekezo kwamba hiyo story soma au hiyo usisome"

Hii imetoa picha kuwa kumbe hawa jamaa huko nyuma walikuwa "wanatumika",walikuwa wanapangiwa nini cha kusoma na kujadili kwa maslahi ya watu fulani.

Ndio maana katika siku zote za sakata la "Bashite na vyeti feki",hawa Clouds inasemekana hawakulizungumzia sana wala kulijadili kwa mapana ktk vipindi vyao.Lakini toka jana na leo,kuanzia kipindi cha muziki cha XXL mpaka Alasiri ya Clouds Tv,mjadala wa vyeti ulianza kushika hatamu.

Huu ni ujumbe kwa hawa wamiliki wa vyombo vya habari,zama za unafiki zimekwisha,wasimamie ukweli,maana wengine wanashindwa kusimama na Clouds Media Group sbb kwa muda mrefu walikuwa kama tawi la chama na kitengo cha propaganda mpaka wengine "tukazila" kuwafuatilia.Hili ni fundisho kwao.
 
Good.
 
Afadhali waache unafiki.... Maana nilikuwa nakereka sana wanavyomsifia Magufuli hadi anapata mzuka wa kupiga simu 360.

Sasa kama Makonda alikuwa anawapangia habari za kusoma, angeshindwaje kuwaingilia na bunduki.?

Mbwa ukizoea kucheza nae ipo siku utaingia nae msikitini.!
 
Pambaffff kabisa hao yani ndo wanashtuka sahizi na kumbe walikuwa wakipewa maelekezo ya habari ipi kwenye magazeti waisome na ipi wasiisome eeeh..? Kama TBC vile Sasa wameamua kuzivujisha siri zao wenyewe..
Ila huyo bashite wamemuendekeza wenyewe wasitafute mchawi.., ukicheza na mbwa atakufuata hadi msikitini.....
 
Back
Top Bottom