Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,717
- 239,303
Kuna msemo wa kiswahili usemao hivi , URAFIKI WA KWELI NI KATIKA DHIKI NA FARAJA , hivyo ndivyo watanzania tulivyoambiwa na wazee wa zamani , kwamba kama mtu wako wa karibu unatakiwa uwe naye wakati wa shida na raha , kama mlikunywa pamoja basi pia si vibaya mkipigia miayo pamoja.
Sakata la Rc wa D'salaam aliyeonekana shujaa na kubebwa sana na clouds media , ambalo sasa limegeuka huzuni kuu , limenifundisha kwamba duniani hakuna rafiki wa kweli , Kwa sasa Clouds wameruka hatua mia , Makonda hatajwi tena kutwa mara 100 !
Wito kwa vyombo vya habari - kuweni makini sana na wanasiasa wa aina ya Makonda , mtapoteza kama wanavyopoteza wao , kuna miongozo imewekwa ya namna media zinavyoweza kufanya kazi .
Hakuna haja ya kujipendekeza kwa wanadamu , fuateni sheria na utaratibu wa halali tu .
Biblia takatifu imeandika kwamba AMELAANIWA AMTEGEMEAYE MWANADAMU .