beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha
Serikali imesema kuwa wanafunzi waliopunjwa na wale waliokosa mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), wataipata kwa sababu kilichokwamisha ni mfumo.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, aliyasema hayo jana, huku akiwaeleza wanafunzi hao wenye sifa ya kuipata kuwa fedha zote zilishatolewa wiki tano kabla ya wao kuripoti vyuoni.
Ole Nasha alisema halikuwa kusudio la serikali wala bodi ya mikopo kupunguza fedha hizo, kilichotokea ni mfumo ulijielekeza vibaya.
“Mnafahamu kwa sababu mfumo huu unajiendesha unaweza kuharibika lakini tayari bodi ya mikopo wameandika barua kwa vyuo vyote kuwaambia kwamba lazima kosa hilo lirekebishwe na mwanafunzi yeyote aliyepunjwa fedha zake, atapata mpaka senti ya mwisho,” alisema.
Naibu Waziri huyo aliwatangazia wanafunzi wote waliokumbwa na kadhia hiyo kwamba jitihada zinafanyika ili wapate fedha zao kwa sababu moja kubwa, waliingia mkataba.
“Ukikubali upunjwe sasa hivi bado kwenye mfumo wa kurejesha utalipa, hatutaki upate hiyo kadhia, ni mfumo ndio ulileta shida,” alisema.
Alisema wiki tano kabla ya vyuo kufunguliwa serikali ilikuwa imeshatoa Sh. bilioni 125 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu, ikiwa ni maagizo ya Rais John Magufuli kuwa hataki wanafunzi wacheleweshewe mikopo.
“Mfahamu fedha zote zimeshatolewa kwa nusu mwaka wa kwanza, wacheleweshaji wanaanzia wanafunzi wenyewe, vyuo, taasisi zetu za udhibiti NACTE (Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi) na TCU (Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania) kama hawaendi vizuri bodi ya mikopo haitaweza kwenda mbele,” alisema.
Chanzo: Nipashe
======
Mchango wa wadau
Wengi tulifarijiwa hivi mwisho wa siku tulisoma miaka 3 bila mkopo na vigezo tulikuwa navyo.......kama mzazi anaweza kujinyima kidogo na wewe mwanafunzi ukabana matumizi basi utaishi vizuri tu
Ukiachana nawale wenye uhitaji wa kweli wa mkopo, kuna ambao wanaapply ili waishi maisha ya ndoto zao (iPhone, girlfriend mkali, kwenda shopping na supermarkets kila weekend, TV sjui fridge plus birthday parties na mambo Kama hayo) .....
Rafiki zangu wengi walipataga mkopo ila wao ndio walikuwa hawana hata 100 baada ya week 2 tu hadi week 3, pesa inakuwa imekata....
Mwisho maisha ya chuo ni mkumbo mkubwa sana, muda mwingine hata wanaotokea kwenye familia za chini wakifika chuo, utawakuta wanaenda shopping ya laki 3 hadi laki 4. wanaenda club kwa sana na kufika pesa, wanahonga mno wanawake ila ndo hivo inaumiza ila ndio lifestyle ya kichuochuo......
My take.. Mwanachuo unaweza kuishi kwa 2000 kwa siku sio lazima uishi kwa elfu 15 kwa siku..... na kwawale wadogo zetu wakiume wa chuo wajue hao kina dada ni wakawaida sana tena wengi washamba washamba tu hawana budi kutumia akili maana maisha mtaani ni magumu sana......