Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Nlitaka kujenga nyumba mkoa *****, mwenzangu akasema:-

"mmmh pale utaona wenzio wanaachia migorofa tu, we unabaki na ya kawaida, kwa nini usijenga hapa *********"

Tokea siku iyo akili imeganda .
 
kuna wale hawajawahi kununua hata mfuko wa cement ndio wanaosema ujenzi rahisi. Hata kama una kipato kizuri ujenzi ni gharama. Usione wenye nyumba wanatoa lugha ngumu mnapobamiza milango they know its price.
You made my day.... Watu hawashangai watu wanakimbia site wanaacha magofu...
 
mi nimejenga chumba na sebule kila kitu.. basic finishing.. no tiles.. kwa 5m tu... ila kuna uzi humu watu walikuwa wanasema milion 10.. nikakata tamaa..

nilivyokaza roho na kuanza ujenz hadi nimeamia
inatagemea na location na materials used, unaweza kujenga kwa tofali za kuchoma ukatumia mbao za bei nafuu kuezeka na madirisha ya bei nafuu pia. ila ujenzi ni finishing na hapo ndio kazi ilipo
 
Nadhani sentensi yako ya mwisho ndo ushauri unaotufaa wote humu.

Wengi tunajenga kwa kuangalia Fulani kajenga vipi. Cha muhimu jipange mapema. Fanya utafiti wa kutosha. Omba ushauri wa kitaalam. NA tumia mali ghafi ambazo una uwezo nazo. Mwisho wa siku nyumba ni finishing. The quality of your finishing determines resources required.
Achaneni na immitation, mm nilianza na kazi ya kawaida kabisa early 2005 nikanunua uwanja. Ujenzi unauma! Uchungu! Hela yote inaishia kwenye nyumba hasa pale mafundi wamefikia kwenye finishing uko radhi hata usinywe soda.! Ilifika kipindi nikataka kuuza baada ya kuona saving inakuwa ndogo kila mwezi.. All in all jitose! Never give up! Kadri unavyojitavidi the more the trouble knocking on to you! Jikakamue
 
Kama ni mtanzania wa kawaida mwenye kipato cha halali kisichozidi milioni kwa mwezi huwezi kusema ujenzi ni rahisi. Tuliojaribu tunajua gharama zake. ukuta mpaka uwe safi kuna mafundi kadhaa wameupitia. Tena hapo umetumia local fundis sikwambii ukitaka wale wa kukukabidhi funguo.
 
dahhh!! nikiona hayo mamilioni mnayosema eti ndo gharama ya chini navurugwa tumbo, ama hakika ujenzi noma, ila kufikia mwaka 2020 lazima niwe kwenye mjengo wangu mzuuuri!!
Mungu akutangulie ndoto yako na dhamira yako itimie, inshallah!!
 
mi nimejenga chumba na sebule kila kitu.. basic finishing.. no tiles.. kwa 5m tu... ila kuna uzi humu watu walikuwa wanasema milion 10.. nikakata tamaa..

nilivyokaza roho na kuanza ujenz hadi nimeamia
Hongera mkuu. Kapicha tafadhali.
 
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
Upo sahihi sana, ila ujenzi hauna ghalama maalum. Kwa mfano kuna mtu anaweza kujenga nyumba kwa Milioni 70 na mwingine akajenga nyumba hiyo hiyo na kwa ramani hiyo hiyo kwa M100. Tofauti kubwa hapo ni nyumba unaijenga wapi na unafanyia finnishing vifaa gani na vya bei gani
 
Ndio nyie tunaowazungumzia.
Nyumba ya mabati sabini kwa elfu kumi na tano bati moja ni milioni moja hiyo.
Mbao za milioni na nusu zinatosha kupaua.
Matofali elfu mbili na mia tano ni milioni tatu hiyo, cement ya kujengea mifuko mia ni sh milioni moja hiyo.. Fundi wa kujenga na kupaua, milioni nne hiyo.. Hizo gharama unazozungumza, unajenga shule?
Safi mkuu umekuwa objective.
 
Back
Top Bottom