Dodoma: Rais Magufuli amezindua Jengo la "UCHAGUZI HOUSE" lililopo na Jengo la TAKUKURU lililopo Ihumwa. Rais hajafurahishwa na jengo la TAKUKURU

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, leo tarehe 22/07/2020 atazindua jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi "CHAGUZI HOUSE" lililopo Njedengwa Saa 3:00 Asubuhi na baadae jengo la TAKUKURU lililopo Ihumwa mkoani Dodoma.

Ntawaletea Mubashara kile kinachojiri kutoka Dodoma.

=====

UPDATES

======



10:00 Rais Magufuli imefika Sehemu y atukio, na Sasa ni Maombi kutoka Madhehebu Mbalimbali yanaendelea.

10:12 Utambulisho wa viongozi mbalimbali waliohudhuria unafanyika, wapo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Viongozi wengine wakubwa kitaifa.

10:16 Taarifa ya Ujenzi wa jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasomwa na Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Charles Mbuge. Aidha, anasema Jengo lilikabidhiwa likiwa na ghorofa nane na kwa sasa jingo hili linakabidhiwa likiwa na ghorofa huu. Jengo kuu la tume limefikia asilimia 97, la kutangazia matokeo lipo asilimia 80.

Jeneral Charles Mbuge anasema mradi huu unatarajia kukamilika mnamo august 30 mwaka huu.

10:32 Salamu kutoka kwa Jaji Kaijage
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amepata nafasi ya kutoa salamu zake. Amemshukuru Rais kwa kuhudhuria tukio hilo la uzinduzi wa jengo hilo.

Kaijage anasema "Muda mrefu tume ya uchaguzi ilikuwa inatumia jengo la kupanga katika Jiji la Dar es Salaam jambo lililokuwa linaleta changamoto za kiutendaji."

Amemshukuru Rais kwa kutenga fedha na kukubali ombi la kuidhinisha Ujenzi wa jengo la Tume huru ya Uchaguzi katika mji wa Dodomapamoja na Jengo la kutangazia na kuhifadhia vifaa vya uchaguli.

Mradi huu ulipangwa kutekelezwa kwa awamu mbili mabpo awamu ya kwanza iligharimu zaidi ya bilionio 11 na awamu ya pili iligharimu zaidi ya bilioni 2. Hivyo kufanya jumla ya gharama za mkataba huo kufikia zaidi ya bilioni 13.

Tume iliingia mkataba mpya na Suma JKT wenye Thamani zaidi ya bilioni 12 ambao ulitarajiwa kukamilika mwezi aprili lakini mkandarasi aliongezewa muda mpaka Julai 30.

“Tangu kuingia mkataba kati Tume ya Uchaguzi na SUMA JKT, mradi umekuwa ukienda kwa kasi na hadi sasa mradi huu umekamilika kwa wastani wa asilimia 89 ambapo jengo la ofisi utakalozindua limekamilika kwa asilimia 97,” Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage
Tangu kuingia mkataba Kati ya Tume na Jkt mradi umeenda kwa kasi na umekamilika kwa asilimia kubwa.

Kaijage ameeleza kuwa Uzinduzi wa majengo hayo unaashiria kuanza rasmi kwa shughuli za tume katika mji wa Dodoma.

Kaijage amewapongeza JKT kwa kufanya kazi hiyo kwa kasi, weledi na uzalendo mkubwa na kutoa rai kwa Rais kuwa kama miradi mingine itafanyika katika mji huo basi Rais awape Makandarasi wa JKT.

10:55 Salamu kutoka kwa Mh. Jenista Mhagama,

"Viongozi wa vyama vya siasa wameniagiza nikufikishe salamu wanakupongeza sana kwa kutufikisha uchumi wa kati, pia wanakupongeza kwa kuliongoza taifa katika mapambano ya janga la Corona" Jenista Mhagama, Waziri wa Sera, Bunge, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu.

Waziri wa Sera, Bunge, Vijana, ajira na Wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama, amesema"Kwangu na ofisi ya Waziri Mkuu na Waziri Mkuu mwenyewe tunatambua uwepo wa vyama vya siasa kama wadau wakubwa wa Tume ya Uchaguzi, mimi nimekutana nao katika warsha mbalimbali"

11: 15 Hotuba ya Rais Magufuli

Watani zangu wagogo wanapenda pesa, mtani wangu wa Kigogo alikuwa anaimba, alipopewa hela tu akaacha kuzungumza na kuimba. Kwa hiyo spika ushahidi leo umejihidhirisha lakini nawashukuru sana kwa nyimbo nzuri, maadili na maneno mazuri sasa makao makuu ni Dodoma.

Nawashukuru wananchi na viongozi ambao imewapendeza kutukaribisha na walioweza kutusaidia kuapata jengo hili, ujenzi sio tu umependesha mandhari ya Dodoma pia umesogeza huduma na kuwarahisishia wadau wa uchaguzi

03 June 2016 alikuja Ikulu mwenyekiti mstaafu, Damiani Lubuva kunikabidhi fedha zilizosalia 2015/16 Tsh bilioni 12. Wakati akinikabidhi alinipa ombi la fedha kujenga ofisi zake. Walibakiwa na bilioni 12, walivyoleta ilikuwa nikabidhi serikali kwa paymaster General, akawa mjanja akaingiza ombi la fedha. Kwa kutambua changamoto za ofisi nililiridhia ombi hilo na nilielekeza kujenga Dodoma badala ya Dar.

Naipongeza tume ya uchaguzi kwa kujenga ofisi zake Dodoma kwa sababu tangu ianzishwe 93 haijawahi kuwa na jengo lake, imekuwa kwenye majengo ya kupanga. Hongereni sana pia naipongeza ofisi ya waziri mkuu kwa kufuatilia ujunzi, nampongeza jaji Lubuva aliweza kuokoa bilioni 12 ambazo ziliwezesha ujenzi wa ofisi hii. Mkataba wa awali ulisainiwa March 2017 na kutakiwa kukamilika June 2018. Hata hivyo TBA alishindwa kukamilisha kwa wakati, namshukuru sana waziri mkuu kusitisha mkataba hhuu na kuwapa vijana wachapakazi wa JKT chini ya Major General Mbuye. Nataka niwaambie JKT kila napotembelea miradi yenu, madeni kwangu yanaongezeka, sitawasahau, mmeonyesha ushujaa mkubwa. Inawezekana tungeweka kandarasi yangekuwa na gharama kubwa.

Hamkulisahau taifa hili na mimi sitawasahau katika ufalme wangu. Hivyo nawashukuru pia namshukuru consultant chuo kikuu cha ardhi, mmesimamia na kutoa michoro mizuri. Nimefika kule nmeanza kuliona hili jengo, hata kama umefika hapa umeshindwa utasaini tu kama walivyosaini wale wengine waliopata zero. Kwa sababu mahali penyewe ni pazuri.

Niwashukuru viongozi wenzangu wa vyama mbalimbali, shughuli hii ni yetu sote. Hivyo niwashukuru wenyeviti wenzangu, tutakuja kuchukulia fomu hapa lakini mnaweza kuacha kuchukua mkasema Magufuli umepita ili fedha hizi zikatumike katika matumizi mengine ya maendeleo ya taifa letu.

Niwaombe wanasiasa kama ambavyo kama ambavyo imekuwa kawaida yenu, uchaguzi huu uwe special, tufanye kampeni kwa upole, kwa kujua sisi ni taifa, tunadi sera na wananchi waweze kupima kutokana na sera zetu, tukienda hivyo uchaguzi huu utakuwa mzuri, utakuwa huru na niwahakikishie mimi ni mwenzenu tunajenga nyumba moja, nitatoa ushirikiano mzuri sana kama tulivyofundishwa na baba wa Taifa.

Niviombe vyombo vya kusimima haki ikiwemo vyombo vya usalama vituvumile kidogo. Niwaombe Wanasiasa wasiwachokoze wale walinda amani, msiwafanye wakatumia nguvu mahali ambapo nyinyi mmewafanya watumie nguvu, Mimi ninatukamtangulize Mungu katika kampeni zetu. Tufanye kampeni nzuri. Na sasa uwanja upo huru, Mh. Jaji ameshatangaza ratiba huu ndi wakati wa kujinadi, huu ndio wakati wa kupiga siasa. Baada ya hapo yule atakayeshinda tunaanza kazi. Siasa zinabaki bungeni na kwenye Halmashauri za wilaya. Kwa hiyo kwa sasa hivi ni ruksa kila mtu akafanye kampeni zake kwa uhuru na uwazi.

Hata Mungu ametusikia maombi yetu, Corona imepotea inakoromea mbali, tulimuomba Mungu siku tatu madhehebu yote. Tukamshukuru pia kwa siku tatu. Nataka niwahakikishie ushindi huu wa Corona kukimbia ni ushindi wa yule aliyepo juu. Tuendelee kumshukuru na kumtanguliza katika shughuli zetu.

Navihimiza Vyama vya siasa kushiriki uchaguzi huu na kujiepusha na vitendo vya vurugu kwa sababu vurugu hazijengi, zinabomoa. Na niviombei vyombo vya ulinzi na usalama visimamie usalama wa Watanzania. Yule atakayechokoza na kufaya vurugu basi atakuwa amechokoza mwenyewe.

Aidha, Rais Magufuli amesisitiza wananchi kujitokeza katika kampeni za vyama mbalimbali kusikiliza sera mbalimbali pamoja na kujitokeza kupiga kura. Siku ya Uchaguzi itakuwa siku ya mapumziko tutaitangaza rasmi.

Leo nimekuja kwa ajili ya kufungua jengo hili Namesikia kuna changamoto sehemu fulani. Tutawaongezea Milioni 500 mnunue vifaa mnavyotaka. Vile vifaa vya Dar mvibebe mlete hapa. Hakuna sababu ya kuanza nyumba mpya na kitanda kiwe kipya na gorodo liwe jipya. Mwisho mtasema na mke awe mpya.

Mej. Jen. Charles amesema wana madai yao ya Bilioni 11 katika Taasisi mbalimbali kwa ajili ya Suma Guard Nitoe wito kwa Taasisi mbalimbali zinazotumia Suma Guard walipe madeni yao. Ndani ya wiki 2 Taasisi zote zinazodaiwa ziilipe JKT

Waziri Mkuu fuatilia, ndani ya wiki 2. Watakaoacha kulipa kwasababu Urais bado nitakuwa nao, Wewe nijulishe popote nitakapokuwa nafanya kampeni - Wewe nijulishe, bahati mbaya niwe nimechoka na kampeni. Wewe nijulishe Taasisi gani imekataa kulipa.

Mwisho, Rais Magufuli amewamshukuru Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Kaijage, na viongozi wote wa Tume. Ameomba akamtangulize Mungu katika kazi yake ili uchaguzi ukafanyike kwa ukweli na uwazi. Sambamba na hilo Rais Magufuli amempongeza Meja Jenerali kwa kazi nzuri ya utendaji ya Ujenzi wa Jengo la Tume.
=====
UZINDUZI WA JENDO LA TAKUKURU




Salamu kutoka kwa Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa
Ameanza kuwashukuru na kuwapongeza Takukuru kwa juhudi zao za kukemea na kupambana na rushwa nchini.

Furaha yangu tena leo ni kuona Taasisi kama hii inapata eneo la kufanyia kazi. Tuko mbele ya Watanzania tunaizindua Ofisi hii ikiwa moja kati ya ofisi zinavyojengwa na taasisi hii ikiwa ni moja ya Ofisi za kufanyia kazi. Jambo hili ni jema naamini kwamba kila wilaya itapata jengo kama hili ili kuwawezesha Watanzania kusema na kusimulia vitendo vinavyohusiana na rushwa.

Mh. Majaliwa amewaomba Watanzania kuwa na ushirikiano na kutoa taarifa ya vitendo mbalimbali vinavyohusu rushwa kwani na watapewa ushirikiano wa kutosha na hawatatajwa kwani taasisi hiyo inafanya kazi yake kwa makini kabisa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wananchi wawe huru kwenye kuwapa taarifa za rushwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU). Amesema TAKUKURU haitawataja watu watakaokuwa wanawapa taarifa za rushwa kuhusu sehemu yoyote

Salamu kutoka kwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai
Amewapongeza Takukuru kwa kazi wanayoifanya pamoja na kuwapongeza kwa matumizi mazuri ya fedha kwa kiwango cha juu jambo lililoiwezesha Taasisi hiyo kuweza kujenga jengo lao.

Aidha, akikazia kauli ya Mh. Majaliwa ya Watanzania kutoa taarifa Mh. Magufuli amesema kuwa Watanzania wanaotoa taarifa kwa takukuru wasitoe kiuchochezi au kwa kutyumia chuki isipokuwa wanapaswa kutoa taarifa za kweli. Ndugai amesema "Watu wanaotoa taarifa feki nao wang'atwe"

Salamu kutoka kwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan
Nakumbuka mwaka 2017 nadhani mlikuwa na shughuli yenu pale mnazi mmoja na nikabahatika kuwa mgeni rasmi wa ile shughuli. Moja kati ya mambo nayozungumza wakati ule Takukuru hamkuwa na hali ile ambayo mnayo leo. Nikawaambia mkitaka kufanya haki kwanza toeni boriti katika macho yenu kisha mtoe vibazi katika mamho yenu. Wakati ule Taasisi haikuwa safi.

Lakini mnalonifurahisha Takukuru ni kusimamia wale wanaodhulumiwa. Kinamama wanaodhulumiwa mnasimama mnatetea haki zao. Tungependa zoezi hili mlifanye nchi nzima, kwasasa tunaiona mikoa ya kati zaidi. Niwaombe sana kawasimamieni wananchi.

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
Rais Magufuli amewashukuru Uongozi wa Wizara kwa kumkaribisha kuja kushiriki hafla ya kuzindua jengo la Takukuru.

Nafarijika kuona kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kazi kubwa imefanyika katika kupambana na rushwa na hili nalisema kwa dhati kabisa kazi mmefanya. kwa taarifa tu kwa ufupi katika miaka mitano iliyopita Takukuru imeweza kufungua jumla ya mashauri 2256 ambapo mashauri 1926 tayari yametolewa uamuzi na serikali kufanikiwa kushinda mashauri 1013, hii ni kazi ya TAKUKURU.

Aidha, Takukuru imeweza kuokoa jumla ya shilingi bilioni 273.38 zikiwemo fedha walizokuwa wamedhulumiwa wakuliwa wakiwemo wa Lindi. Vilevile Takukuru imeweza kutaifisha fedha taslimu milioni 899. Dola za Kimarekani milioni 1, 191,651 walitaifisha Takukuru. Euro, Milioni 4,301,399, Nyumba zilizotaifishwa ni 8 zenye thamani ya shilingi Bilioni 11. 6, magari matano yenye thamani ya shilingi milioni 126 pamoja na viwanja vitano hongereni sana Takukuru.

Halikadhalika, Takukuru imerejesha mali za serikali zilizochukuliwa na watu binafsi a,ma taasisi kinyume cha sheria zikiwemo nyumba na majengo 98, ikiwemo Mbeya hotel imerudishwa ni mali za serikali. Kazi ya Takukuru hongeeni sana.

TAKUKURU imeweka kwenye zuio Bilioni 52.1, Dola za Marekani Milioni 55.8, Yuro Milioni 4.3, Magari 75, Nyumba 41, Viwanja 47 na mashamba 13. Ni kwaajili ya kusubiria kukamilika kwa taratibu za kisheria za utaifishaji. TAKUKURU hongereni.

Rushwa ni mbaya sana na imetuchelewesha sana. Kuna miradi mingi ni hewa, imetengenezewa value zisizo za kweli. Wala rushwa walikuwa wafalme kweli, walikuwa hawaguswi. Nawapongeza wafanyakazi wa TAKUKURU ambao kwa asilimia kubwa mnajituma

Palipo na mazuri dosari hazikosi, zimezungumzwa. Salamu zenu hapa ni kung'ata ila mama Kuluthum aliwang'ata ninyi. Alikaa muda mrefu bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa sababu ya 'connection' aliyokuwa nayo ndani ya TAKUKURU.

Hii inaleta picha mbaya ndani ya TAKUKURU kwamba yakitokea mabaya ndani yenu hamshughulikiani. Hii inapoteza picha nzuri ya Taasisi. Mnatimiza wajibu wenu ila kuna asilimia kubwa hamtimizi wajibu wao. Mkurugenzi nataka ushughulikie hii.

Rais Magufuli ameona hakuna uwiano kati ya nyumba Takukuru na gharama zilizotumika, katika hili Rais "amesema Mimi nimejenga nyumba na ninyi mmejenga. Na hili siwezi kuficha, ndiyo maana nimezunguka kuangalia. Nikasema hakuna kitu hapa tumeliwa. Nikazungumzie wapi, Ofisini? Hapa hapa ili Jenerali ujue. Nina uhakika kama umejenga nyumba huwezi kujenga hii kwa Milioni 143.

Rais Magufuli amesema "Nilikuwa namuuliza Waziri Mkuu. Wewe unaweza kujenga nyumba hii kwa Milioni 143? Akasema mimi hapa kama Milioni 60. Nikaangalia mimi nyumbani nimejenga nyumba ukubwa kama huu Milioni 40. Nilikuwa naangalia hawa Wataalamu, nikasema ni wa Variation pia."

Sasa mbadilike na mabadiliko haya yawe 'total change'. Mkianza na gharama za ujenzi na nimezisikia zamani kabla hata hujawa Mkurugenzi. Mmeokoa fedha nyingi, ningetamani hata niwape hizo fedha za kujenga ukuta lakini si kwa gharama hiyo.

Mmeniomba pesa hapa za kujenga ukuta Bilioni 1 kwa nyumba 7. Tulipoamua kuanzisha Makao Makuu Dodoma, kila Wizara ilipewa Bilioni kujenga Makao Makuu yake na ikamaliza kila kitu - Sasa Mgema akisifiwa Tembo hulitia maji. TAKUKURU msianze kuweka maji

TAKUKURU mmekuwa Chombo ambacho hakiguswi na hata akipatikana mbaya miongoni mwenu wala hapelekwi Mahakamani na kufungwa. Mnatafuta njia, amerudishwa ame-recover, si ange-recover akiwa ndani amefungwa? Kwanini wengine hawa-recover?

Inawezekana watu wako wanaokufanyia 'variation' wasikupe variation za kweli. Wewe (Mkurugenzi) si ulichukua law? Ukipiga hesabu, matofali yaliyoenda hapo unayajua! Unapima urefu wa nyumba unachukua tofali moja la nchi 6 unagawa kwa Mita utakazopata.

Mnaomsaidia Mkurugenzi hebu kaeni vizuri, nisije mimi nikajenga nyumba hapa ya Milioni 60 ikawa kubwa kuliko hii. Huyu ataondoka na ninyi mliomsaidia mtaondoka. Na nyie Watumishi mnafahamu. Wanajua mengine ya TAKUKURU sio mazuri. Ila wapo wanaofanya vizuri sana.

Kwa Chama changu cha mapinduzi kashirikianeni katika kujenga Chama kachapeni kazi. Sijui kama mna ofisi ya Chama. Mtakapoanza kuijenga msisahau namimi nitatoa changiua na Ndugai naye achangie na Waziri Mkuu. Chemwino ndio makao Makuu ya nchi hayatabadilika kamwe mashetani yote yashuke yatakuta hapa ndio makao makuu ya nchi.

Nyumba ya TAKUKURU, Namtumbo itafunguliwa na Mkuchika. Ya Ruangwa imeshafunguliwa na Waziri Mkuu - Jengo la hapa Dodoma la Intelijensia atalifungua Waziri Mkuu. Hii ya hapa nitafungua mimi japo gharama zake zipo Juu ila nimeamua kufungua

Utakaponileta gharama ya kuta zote katika nyumba 7 ile itakayokuwa nzuri si Bilioni 1 nitawapa. Nina uhakika haitazidi Milioni 500 -

Aidha, rais Magufuli akihoji kuhusu urefu na vipimo vya ukuta unaotarajiwa kujengwa alisema:

Rais Magufuli: Mna ukuta wa urefu wa ngapi kwa ngapi?

Anajibiwa: Urefu wa ukuta wa ofisi kama hii ya Chamwino ni Mita 350

Rais Magufuli: Kwanini unajenga Mita 2? Ni Gereza? Ujue mtawekea vitu visivyo na msingi

Anajibiwa: Hapana

Rais Magufuli: Mimi urefu wangu ni Sentimita 168, Mita 1 na kitu. Wewe una mita ngapi?

Anajibiwa: Mita 1.65

Rais Magufuli: Sasa ukijenga ukuta mpaka ufike juu kama Gereza?

Rais Magufuli: Wewe zidisha Urefu kwa Upana sio kuhusu mzunguko (Circumference).

Anajibiwa: Ni square meter 7,800

Rais Magufuli: Utatumia matofali mangapi?

Anajibiwa: Naomba muda kidogo nifanye mahesabu

Rais Magufuli: Ukuta una urefu gani?

Anajibiwa: Una urefu wa Mita 2.2

Mlitaka nifungue nyumba 7 kwa pamoja. Ila kwa heshima ya TAKUKURU kila nyumba itafunguliwa peke yake. Za Mpwapwa zitafunguliwa na Makamu wa Rais. Ya Manyoni itafunguliwa na Spika, ya Masasi itafunguliwa na Mkurugenzi wa TAKUKURU.

Nyumba ya TAKUKURU, Namtumbo itafunguliwa na Mkuchika. Ya Ruangwa imeshafunguliwa na Waziri Mkuu. Jengo la hapa Dodoma la Intelijensia atalifungua Waziri Mkuu. Hii ya hapa nitafungua mimi japo gharama zake zipo Juu ila nimeamua kufungua.

Nilitegemea Mkurugenzi wenu aniombe fedha kujenga nyumba za Wafanyakazi. Kama ninyi mnataka na Mkurugenzi anataka nitatoa Bilioni 2. Ila wasiende kusimamia watu wako hawa. Peleka michoro yako wape JKT wakajenge hizo nyumba. Mkuu wa JKT, hizi fedha wakupe wewe.

Mkurugenzi usiwape hizo fedha hawa (Waliojenga nyumba za TAKUKURU). Hawa nimewashtukia mimi. Nataka Wafanyakazi hawa waishi kwa raha wanapoenda kwenye kazi zao waifanye kama Malaika. Anamkamata mla rushwa na kurudi kwakwe. TAKUKURU ni muhimu katika nchi hii.

Wakuu wa Wilaya na Mikoa washirikiane na TAKUKURU, haiwezekani Mkuu wa Wilaya ana jengo kubwa anashindwa kumuweka wa TAKUKURU. Nitoe wito kwa Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa, kama kuna ofisi ya Wilaya sehemu na Ofisi ya TAKUKURU iwepo hapo.

Aidha, Rais Magufuli amepinga suala la kujengwa kwa ofisi ya Takukuru Chato kwa sababu eneo hilo tayari lina ofisi ya Takukukuru. Rais magufuli amedai jambo hilki ni matumizi mabaya ya fedha.

Rais Magufuli amesema "Chato wana ofisi ya TAKUKURU. Lilikuwa jengo la TBA, wakachelewa kuingia pale ilikuwa ni jengo la Mkuu wa Wilaya. Nikiwa Wizara ya Ujenzi. Nilimuita Hosea na kukabidhi. Sasa jengo mnaenda kujenga jingine la nini? Mjipendekeze Chato nikiwa nimeondoka kwenye Urais.

"Mnajenga ofisi ya TAKUKURU Chato ya nini? Mlifikiri nitafurahi mkisema Chato? Mimi moyo umeshakuwa sugu - Mkurugenzi hujui kama Chato kuna Ofisi ya TAKUKURU? Kwanini wakudanganye watu wako. Haya ni matumizi mabaya ya fedha"

Hapa mmesema mnataka kujenga ofisi ya TAKUKURU Chato ninawashangaa! Kwasababu TAKUKURU Chato tulikuwa na jengo, ghorofa lipo mlimani. Unataka kujenga ofisi ya wapi? Msizungumze mambo kunifurahisha mimi na kujipendekeza. This is not the way

Spika hapa Kongwa hakuna Ofisi, mmeacha hapa karibu na kwenda hadi Chato? Unajua mambo ya ajabu sana - Hiyo ofisi ya Chato ipelekeni basi Kongwa. Spika anajua kuna wala rushwa wengi nataka mkawashike huko. Msipeleke maeneo fulani ofisi 2

Ninyi watu wa TAKUKURU huku ndiko kung'ata? Mimi natoka Chato na ile ofisi ipo kwenye shamba la marehemu baba yangu alinyang'anywa. Ni ghorofa limejengwa na TBA kwa fedha nyingi. Jengo lingine la nini wakati Wilaya nyingine hakuna Ofisi?

Mkurugenzi Mkuu aliyekuletea haya unamfikiriaje? Wewe ni mwanasheria, hii sio rushwa? Mkurugenzi TAKUKURU: Nilichoambiwa ni kuwa lile jengo lilikuwa ni la makazi. Kiongozi wa Chato hana nyumba ya kudumu. Tuliwaza ibaki kuwa makazi na kisha tupate ofisi.

Wakuu wa Wilaya na Mikoa washirikiane na TAKUKURU, haiwezekani Mkuu wa Wilaya ana jengo kubwa anashindwa kumuweka wa TAKUKURU. Nitoe wito kwa Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa, kama kuna ofisi ya Wilaya sehemu na Ofisi ya TAKUKURU iwepo hapo

Akizungumzia mpango wa maendeleo na miradi inayotarajin kutekelezwa Mkoani Dodoma, Rais Magufuli amesema "Jiji la Dodoma litakuwa jiji kweli. Nataka kuwathibitishia ndugu zangu wa Dodoma hili litakuwa jiji kweli. Uwanja wa ndege sasa hivi wanatafuta Mkandarasi. Uwanja ule utakuwa Mkubwa kama wa Dar es Salaam na hela ipo zaidi ya bilioni 500. Tunatafuta mkandarasi aanze kuujenga wa Msalato.

Tunataka mtu awe anatoka hapa anaenda London anatoka hapa moja kwa moja anaenda Marekani. anatoka hapa anaenda uchina na bahati nzuri ndege nazo zipo na nyingine zitakuja tatu nane zimeshakuwepo. Hii ndio Tanzania tunayotaka kuijenga.
 
Hivi na huko USA na Ulaya ya Magharibi marais / PM or whatever the name of the head of state wanazindua majengo?
Walizinduaga zamani.
Kumbuka huo ni mji Mpya wa shughuli za kiserikali na zinduzi za namna hii ni platform muhimu kwa Mkuu wa nchi kazungumza na wananchi.
Huko Ulaya na kwingineko wao wanatumia tweeta.
 
Hivi na huko USA na Ulaya ya Magharibi marais / PM or whatever the name of the head of state wanazindua majengo?
Huyu baba anataka kututoa kwenye sherehe za uhuru tulioupata kupitia kwa mashujaa wa Kigamboni...

Wajanja tumeshtuka!
 
Uwepo wa vyama vya kisiasa unaonyesha mwelekeo wa uchaguzi ulivyoandaliwa.

Eti UDP, NCCR, TLP ..... What a joke!!
 
Hela ni kwenye majengo na miundombinu tu kwa miaka yote mitano!!

Hii sio sawa kabisa na ndio maana watumishi wanateseka na hata wakulima wa korosho nao wamesoteshwa kwa muda mrefu kulipwa hela zao.

Kwa kifupi,kumekuwa na athari nyingi sana kwa kuwa na vipaumbele vya aina moja tu kwa miaka yote mitano.
 
Back
Top Bottom