Wamuyaya
Member
- Apr 4, 2021
- 72
- 68
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni!
Sikuamini machoni mwangu pale nilipowaona mafundi waliokuwa wakiendelea na ukarabati (kupiga plaster) nyumba ya jirani yangu maeneo ya Tabata, wakiambiwa na mtendaji wa mtaa kuwa hawaruhusiwi kuendelea na kazi ya ujenzi huo hadi pale boss wao atakapoenda kuomba na kulipia kibali cha kufanya ukarabati wa nyumba yake.
Cha kushangaza ni kwamba huyo jirani yangu alihamia Kwenye hiyo nyumba zaidi ya miaka 5 iliyopita, na alihamia kigumu bila kupiga plaster. Na alipokuwa anajenga wala hakuombwa kibali cha ujenzi, lkn leo hii amepata vihela ili afanye finishing ya nyumba yake anaambiwa lazima akalipie kwanza kibali. Hivi hii imekaaje...yaani Tanzania ya Mama Samia imefikia hapo?
Alipojaribu kufuatilia Ofisi ya jiji aliambiwa hilo ni agizo kutoka kwa mkurugenzi wa jiji la Ilala...Ni sheria! Wakidai kwamba kila aina ya ujenzi na ukarabati wowote unaotumia materials kama cement, nondo, mchanga nk bila kujali ukubwa na aina ya jengo, ni lazima mhusika aombe na kulipia kibali cha ujenzi kabla ya kuendelea na ujenzi/ukarabati.
Hatari sana....Juzi kati tumetoka kwenye ongezeko la tozo za miamala ya simu, leo tena zimekuja tozo za LUKU. Huku JIJI nao wanataka tozo za vibali vya kukarabati vibandavyetu. Hii nchi sasa naona kila mahali ni pa MOTO...hapashikiki! NIMECHOKA!