Waliojenga nyumba hupenda kuwaogopesha wengine kuwa ujenzi ni gharama!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
 
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni kuplay god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
Acha kudanganya watu labda kama unajenga kibanda kijijini ila ujenzi ni gharama, take it from me.

Sent from my VFD 300 using JamiiForums mobile app
 
Kumbuka gharama za ujenzi ni sawa na unapoenda kununua nguo dukani, nguo ni bidhaa ambayo bei yake haijasimama kama bidhaa ya sukari au mchele.

Ndio gharama za ujenzi zilivyo mfano
Utofauti wa upatikanaji wa matirio hutofautiana bei eneo na eneo wengine matirio ya ujenzi wanapata kwa dili wengine kwa bei kubwa nk

Gharama za ujenzi kuna mafundi wana bei kubwa wengine bei ndogo

Ndio maana humu tunaona nyumba unambiwa inauzwa milioni 50 wakati ukiangalia ina thamani ya milioni 20 tu

Kwaiyo mtu anapolalamika ujenzi garama usimshangae pengine kweli ujui amejengaje pia wewe unayeona ujenzi si garama pengine kweli hatujui umejengaje

Mfano bei ya kiwanja maeneo mengine tz sawa na shagarama ya nyumba ya kisasa iliyokamilika hapa hapa tanzania

Mfano juzi juzi hapa nimeshuhudia mtu anauziwa kiwanja milioni nne tena anafurahi anaona bei rahisi kweli eneo ambalo wenyeji wanauziana kwa milioni mpaka laki tisa Kiwanja unaona hii kitu

Sababu aliyenunua kiwanja kwa milioni nne ni mgeni katoka eneo ambalo aridhi ina thamani watu wanauziana mpaka milioni 30 eneo la miguu 25 kwa ishirini
 
Acha kudanganya watu labda kama unajenga kibanda kijijin ila . Matofali jenz ni gharama .take it from me

Sent from my VFD 300 using JamiiForums mobile app

Acha kudanganya watu labda kama unajenga kibanda kijijin ila ujenz ni gharama .take it from me

Sent from my VFD 300 using JamiiForums mobile app
Ndio nyie tunaowazungumzia.
Nyumba ya mabati sabini kwa elfu kumi na tano bati moja ni milioni moja hiyo.
Mbao za milioni na nusu zinatosha kupaua.
Matofali elfu mbili na mia tano ni milioni tatu hiyo, cement ya kujengea mifuko mia ni sh milioni moja hiyo.. Fundi wa kujenga na kupaua, milioni nne hiyo.. Hizo gharama unazozungumza, unajenga shule?
 
Kwa uzoefu ua nashangaa watu wanaodai ukiwa na m20 nyumba ndo inakamilika!! Nyumba hata milioni 5 ipo sema unataka nyumba yenye nakshi zipi za gharama kiasi gani!! Kuna my class mate kamaliza kwa badget ya 16 milion but the quality of it unaeza sema ni 50 milion!! Lakini itategemea unajenga wapi
 
Acha kudanganya watu labda kama unajenga kibanda kijijin ila ujenz ni gharama .take it from me

Sent from my VFD 300 using JamiiForums mobile app
Acha mupigilia msumali wa mwisho, ujenzi ni gharama kulingana na sehemu unayojenga. Mfano unanunua malighafi na kusafilisha kwa umbali mrefu lazima uone gharama, lakin kama malighafi zimekuzunguka gharama itatoka wapi, chukulia mfano kwa wakazi wa Dar vifaa vya ujenzi gharama ipo chini sana sema viwanja ndio tatizo.
 
Kama umeshagundua ujenzi ni rahisi wewe jenga tu.... Hata Thread yako haitachangia kupunguza gharama... Ila gharama za ujenzi wa nyumba zinaongezeka kutokana na vifuatavyo... eneo la ujenzi(topography yake), ubora wa material ya ujenzi mfano mbao, bati, tiles, rangi n.k, ubora wa kazi (fundi mwenye kujua kazi yake vizuri na hela anaijua pia), urembo ktk nyumba (urembo wa ceiling, kuta, nguzo, bati, madirisha, milango, nk) upatikakanaji wa material za ardhini kama mchanga, mawe, udongo n.k)... Kutokana na haya na mengine mengi na kawaida kabisa kusikia ramani moja ila gharama zimezidi hata mara 3 au 4 zaidi... Usiandikie mate na wino upo anza ujenzi ndipo utagundua wanaosema ujenzi ni ghali ni majuha au wajanja
 
Jenga na wewe alafu ulete hizo gharama za chini ili uwatie moyo wengine!

Gharama za ujenzi zinategemea na eneo ulipo, nature ya kiwanja, materials unazotumia na aina ya wajenzi unaotumia na ukubwa na hadhi ya nyumba unayotaka jenga... Mtu akikutisha gharama wala zisikutikise, hamuwezi fanana!

Wengine wamejenga nyumba ya kawaida tu, sio ghorofa na millioni 150 TZS zimekatika na bado nyumba haina finishing nje!
 
Ndio nyie tunaowazungumzia.
Nyumba ya mabati sabini kwa elfu kumi na tano bati moja ni milioni moja hiyo.
Mbao za milioni na nusu zinatosha kupaua.
Matofali elfu mbili na mia tano ni milioni tatu hiyo, cement ya kujengea mifuko mia ni sh milioni moja hiyo.. Fundi wa kujenga na kupaua, milioni nne hiyo.. Hizo gharama unazozungumza, unajenga shule?
unanikumbusha kipindi mzee anajenga nyumba yake ya uzeeni, alifanya utafiti wake na kupanga bajeti kama unavyopanga hapo... Akafikia kwenye conclusion eti millioni 60 inatosha kabisa!!!!
Alivyoanza ujenzi mbona macho yalimtoka!!!
 
Ndio nyie tunaowazungumzia.
Nyumba ya mabati sabini kwa elfu kumi na tano bati moja ni milioni moja hiyo.
Mbao za milioni na nusu zinatosha kupaua.
Matofali elfu mbili na mia tano ni milioni tatu hiyo, cement ya kujengea mifuko mia ni sh milioni moja hiyo.. Fundi wa kujenga na kupaua, milioni nne hiyo.. Hizo gharama unazozungumza, unajenga shule?
Vipi kuhusu FINISHINGI mkuu. Masinki. Tiles. Rangi. Ripu. Madirisha. Milango. Umeme. Mabomba ya maji. Vyoo. Dari. Septic tanks. Sewerage systems.

Yaani kwa ufupi hayo uliyotaja ni robo ya gharama zote.
 
Nimejaribu kufuatilia kauli za waliojenga nyumba. Huwa wanapenda kuwaogopesha waliopanga kuwa ujenzi ni gharama.

Huwezi kutana na mtu akakutia moyo hata kidogo. Lengo la wengi waliojenga ni ku play god. Yani wanapenda waheshimike na kujionesha kuwa wana mawe marefu.

Mimi ninapopiga gharama za ujenzi, napata gharama za chini kama ambavyo Magufuli alifanya kwenye ujenzi wa hostel za UD. Tukienda kwa stail yake, mbona kila mtu atakuwa na ka mjengo!
Usiogope mkuu ujenzi ni mpango WA muda utakaoupangilia wewe (hapa hela za pembeni hazihusiki! Mm nimejenga nyumba for just 72.5m. Kwa miaka mitatu to! Ni mipango tu ya saraly yako Hakuna uchawi hapa! Jenga nyumba kwa percentage yako ya mshahara mm nilikuwa nikiweka 30%ya salary jenga kwa kiwango cha kipato chako! Si kujenga kwa kujifanananisha na Fulani, hata ukijenga miaka kumi Nani WA kukuuliza!
 
Vipi kuhusu FINISHINGI mkuu. Masinki. Tiles. Rangi. Ripu. Madirisha. Milango. Umeme. Mabimba ya maji. Vyoo. Dari. Septic tanks. Sewerage systems.

Yaani kwa ufupi hayo uliyotaja ni robo ya gharama zote.
Kwa vijana wa mjini wanaita kupanga matofali... Huko kwenye finishing ndio tunakoachana kwani mwingine tiles ya mchina box 20,000/tsh na mwingine box 65,000/=tsh... bati unaweka la 16,000/= mwingine anaweka la 40-80,000/=.... Ujenzi sio kupanga tofali na ndio maana nyumba haionekani size hadi imeisha vizuri. Bado hayo uliyotaja hapo... shikamoo ujenzi...
 
Vipi kuhusu FINISHINGI mkuu. Masinki. Tiles. Rangi. Ripu. Madirisha. Milango. Umeme. Mabimba ya maji. Vyoo. Dari. Septic tanks. Sewerage systems.

Yaani kwa ufupi hayo uliyotaja ni robo ya gharama zote.
Na huku ndo kwenye gharama sio kule kwenye kupanga tofali, mi nilinunua vifaa vya umeme 2m nikavibeba kwa bodaboda yaani vyepesiiii
 
Usiogope mkuu ujenzi ni mpango WA muda utakaoupangilia wewe (hapa hela za pembeni hazihusiki! Mm nimejenga nyumba for just 72.5m. Kwa miaka mitatu to! Ni mipango tu ya saraly yako Hakuna uchawi hapa! Jenga nyumba kwa percentage yako ya mshahara mm nilikuwa nikiweka 30%ya salary jenga kwa kiwango cha kipato chako! Si kujenga kwa kujifanananisha na Fulani, hata ukijenga miaka kumi Nani WA kukuuliza!

Nadhani sentensi yako ya mwisho ndo ushauri unaotufaa wote humu.

Wengi tunajenga kwa kuangalia Fulani kajenga vipi. Cha muhimu jipange mapema. Fanya utafiti wa kutosha. Omba ushauri wa kitaalam. NA tumia mali ghafi ambazo una uwezo nazo. Mwisho wa siku nyumba ni finishing. The quality of your finishing determines resources required.
 
Back
Top Bottom