Waliofeli Kidato cha Pili kuendelea na Masomo

Waliofeli Kidato cha Pili kuendelea na Masomo

Hakuna la kuhangaza hapa. Kama wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanachaguliwa kuingia sekondari unategemea nini? Hapa wanakwepa aibu ya kufaulisha wasiostshili ili wawe na takwimu kubwa. Wanchotafuta au kutaka wao ni takwimu kubwa na si ubora. Ni katika nchi ya ajabu kama Tanzania ndipo waziri anasimama hadharani na kutangaza kuwa wanafunzi zaidi ya 5200 wamefaulu kuingia kidato cha kwanza wakiwa hawahui kusoma. Sasa jiulize huko sekondari wanafanya nini? Hatua kama hii ni mwendelezo ule ule wa kufaulisha badala ya wanafunzi kufaulu wenyewe. Hawa si muda mrerefu utawakuta vyuo vikuu. Wamepitaje? Ni kwa njia hii kwakuwa viongozi wanacheza na idadi na si ubora. Mwakani wakati wa kampeni utawasikia wakitoa takwimu hizo za kuongezeka kwa ufaulu na idadi ya wanafunzi mashuleni na vyuoni. Na ndipo kwa mtindo huu tunawapata mawaziri kama Mulugo asiyejua hata historia ndogo ya nchi yake na kiongozi mkuu asiyejua kwanini nchi yake ni masikini licha ya kuwa na shahada ya uchumi! LONG LIVE "BIG RESULTS NOW!"
 
Haya ndo madhara ya kuingiza siasa ktk mambo ya kitaalamu,elimu yetu haina mwelekeo wanachofanya ni kuosha chombo nje wakati ndani kuna uchafu
 
Kadri uchaguzi mkuu 2015 unavyokaribia tutasikia mengi. Kuna rafiki yangu anasomesha shule ya kata kaniambia shule yao haijawahi kuwa na mwalimu wa maths tangu form one mpaka four tangu ilipoanzishwa mwaka 2000! Katika hali kama hii, tutegemee nini hasa mkizingatia kwamba kuna wanafunzi wanaochaguliwa kwenda sekondari wakiwa hawajui kusoma wala kuandika? Haya ni MAJANGA kwa kweli.
 
Serikali imeagiza wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2013 na kushindwa,waendelee na masomo yao yaani hawatakariri wapewe Muda maalum wa kunolewa [REMIDIAL CLASS].

Nini maana ya Dr.Shukuru kawambwa kama ataamua wanafunzi wote waendelee na masomo hata wale waliofeli?
Huku ni kuua elimu kabisa,kwani tone moja la udongo huchafua maji yote kwenye ndoo.Wale waliofeli watawaharibu hata hawa wenye juhudi na waliofaulu,naomba waziri huyu hatufai!Elimu sio,tu kwa malengo ya kisiasa,ni msingi imara kwa maisha ya vijana wetu ambao ndio uti wa mgongo wa Taifa hili,na Viongozi wa kesho katika ngazi zote za kitaifa.
 
Sasa wakiendelea kidato cha tatu ilihali cha pili walifeli, sijui itakuaje huko mbeleni...
 
Hii wizara kweli ina watu

kwa Tanzania tutabadili mno viongozi lakini elimu imefariki. Kuingia mchome kama katibu mkuu nikadhani mambo yatakuwa mswanu kwa kuwa ni prof tena wa sheria akisaidiana na waziri wa elimu dr wa vyuma( Sido) kawambwa div.5 ukawa mkwara wa mchome wa kuingilia, imeshindikaka sasa free pass form 2, haya bana mimi sio prof nisije onekana sina adabu kumchalenge prof wa Uds mchome, naka degree kangu kaku unga unga.Ni samehe prof mchome na Dr kawambwa.
 
OPERESHENI YA KICHWA BADALA YA MGUU NA MGUU BADALA YA KICHWA, those students are the future doctors,teachers,magistrates,ole wako upite anga zao,utafanyiwa miujiza,inabdi nijipange kusomesha my kid in the best schools na matibabu japo kenya au south africa than to risk

Mkuu, sikubaliani na nia ya serikali kuwaruhusu waliofeli kuendelea na masomo kidato cha tatu, ni kwa sababu imekwishaona madhara yake katika kipindi cha miaka 2 huko nyuma. Lakini pia nakupinga moja kwa moja kuwa kusolve tatizo hilo eti wewe utamsomesha mwanao katika shule nzuri, hiyo ni kuonyesha ulivyo mbinafsi maana hapa tunaongelea issue ya kitaifa. Pia mwanao hatasoma akawa na profession zote, atakuwa medical doctor sawa lakini atabobea mfano katika macho, atakusaidia sana ukiugua macho lakini ukiumwa moyo utapelekwa kwa doctor atakayekufanyia operesheni ya figo so unakuwa hujatatua tatizo.
Hoja yangu: Tulijadilo suala hili kitaifa na sio kifamilia.
 
Mkuu,hali ilipofikia ni kila mtu afe au apone kivyake
 
kwa Tanzania tutabadili mno viongozi lakini elimu imefariki. Kuingia mchome kama katibu mkuu nikadhani mambo yatakuwa mswanu kwa kuwa ni prof tena wa sheria akisaidiana na waziri wa elimu dr wa vyuma( Sido) kawambwa div.5 ukawa mkwara wa mchome wa kuingilia, imeshindikaka sasa free pass form 2, haya bana mimi sio prof nisije onekana sina adabu kumchalenge prof wa Uds mchome, naka degree kangu kaku unga unga.Ni samehe prof mchome na Dr kawambwa.
Mkuu tatizo la wizara limekaa kifamilia zaidi. Kawambwa na Mchome wameoa nyumba moja kwa hiyo maamuzi yanayogusa taifa yanafanyika nyumbani wakifika ofisini ni kutoa tu matamko yasiyo na maslahi kwa maendeleo ya nchi hii. Yaani hawa Kawambwa, Mchome na Kamishna Bhalalusesa hawana hata chembe ya uzalendo kwa taifa hili. Maamuzi yao yote tanalenga kuua Elimu. R.I.P Elimu ya Tanzania
 
Hivi serikali kwanini inachezea elimu kiasi hiki? Kwanin serikali inataka kufanya elimu iwe mtaji wa kisiasa? Yan mtu afeli halafu aendelee kusoma ili baadae awe nan? Mambo kama haya hayakubaliki hata kidogo. Hebu tuache utani na suala la elimu jamani watanzania. Sio lazima kila mtu asome mpaka kidato cha nne kama kafel kwenye elimu rasmi atafutiwe mbadala lakin sio kwa kuendelea kuleta siasa katika elimu.
 
Ama Kweli Wizara Ya Elimu Ni Kichwa Cha Mwendawazimu Kila Mtu Ananyoa Mfano Pengine Kuna Watoto Wa Baadhi Ya Viongozi Wakuu Wa Wizara Watoto Wao Wamefeli Haswa Huyu Kilaza Mulugo Kalandisha Hadi Mtoto Ukilaza Hatmae Ameshndwa Kupass Form 2,,,,, Ccm Oyeee!
 
Back
Top Bottom