Waliofeli Kidato cha Pili kuendelea na Masomo

Waliofeli Kidato cha Pili kuendelea na Masomo

jamani tanzania yangu wengine waiweka mifukoni mwao et yao, wakilala na wakezao wanawashauri wafanye nini juu ya sisi na nchi yetu. eeh muumba shusha mikono yako.
 
Mkuu,

Sijui kama wengi wanakuelewa hapa. Athari iliyopo ni cream ya watu wa dini moja kusonga mbele alafu upande wa dini nyingine kulalamika. Watataka utawala kuzingatia udini badala ya uwezo wa mtu kishule.
Mthian wa form two aliutoa jk, wameona athari zake baada ya miaka 2 wakaulejesha, kumbe wamerudisha kiini macho tu!

Tatizo hapa sio watu wa dini moja kuwa mbele. Tatizo ni level ya mafisadi. Sijawahi kusikia eti kanisa Fulani limekataa mchango wa fisadi Fulani....
Watakataa vipi na hali wamewalea na kuwasomesha??
 
Serikali imeagiza wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2013 na kushindwa,waendelee na masomo yao yaani hawatakariri wapewe Muda maalum wa kunolewa[REMIDIAL CLASS].

Mwaka huu 2014, ni mwaka wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kama sijakosea! Kwa hiyo Serikali ya Magamba inaogopa kupoteza viti vya Uongozi! Its more politically!
 
Nchi iliyokosa direction tunaenda kama minguruwe inavyokwenda kwahyo ni kwanin walirudisha hii mitihani. Hawajui ndo janga ambalo serikali itakuja kuwaumiza wenyewe baadae bora wafanye screening huku Form II kuliko kumdanganya mtu afike form 4 kichwani hajui objective hata la somo moja kwenye hayo 9.
 
Hawaoni tatizo, ababu wao wenyewe wameferi kuendesha nchi, na wengi wao hawajaenda shule, waghushi vyeti, unakuta mtu anajiita Doctor, mambo anayofanya hayaendani na elimu yake, hili balaa, wananchi tuache kumung'unya maneno, kwa sasa mkombozi wetu ni CHADEMA, tuiunge mkono kwa kuondoa mauchafu haya, taifa linayumba.
 
Serikali imeagiza wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kidato cha Pili mwaka 2013 na kushindwa,waendelee na masomo yao yaani hawatakariri wapewe Muda maalum wa kunolewa[REMIDIAL CLASS].

Hii kama imekaa kisiasa zaidi!!! Na kwanini mwaka jana na juzi hawakufanya hivi? Tunapoelekea 2015 tutaona mengi sana..
 
Suala la form two kufeli ni muendelezo wa tatizo la mfumo mzima wa elimu Tanzania. Kama wanafunzi hawana msingi mzuri tangu primary unategemea nini? Hata kama watabebwa mpaka form four tatizo litabaki pale pale. Hakuna miujiza itakayowafanya wafaulu. Kimsingi tukubaliane kuwa kuna baadhi yetu wamekuwa ni wahanga wakubwa wa mfumo huu mbovu wa elimu na Serikali bado inatatizwa na namna ya kuweza kulisaidia kundi hili. Hata hivyo jambo la msingi ambalo Serikali inapaswa kufanya ni kuimarisha msingi wa elimu kwa maana mfumo mzima wa elimu badala ya kushughulika na matokeo (results) miaka nenda miaka rudi.
 
jamani ndio nini hii? .........Okay! tunaomba chanzo.
 
Tusisahau kuwa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa hii wizara anatumia jina lisilo lake baada ya kufanya vibaya shuleni kipindi hicho!

Mwananchi wanasema wameona barua inayotoka wizarani kwenda kwa maafisa elimu ikielekeza kutowarudisha wanafunzi waliopata alama 20-29.Badala yake waendelee huku wakifanya the so called "remidial classes".

Hii ni tofauti na msimamo wa serikali hiyohiyo wa mwishoni mwa 2012 kwamba watakaopata chini ya alama 30 watakariri darasa kwa mara ya kwanza na kurudishwa nyumbani kwa mara ya pili!

Sijui elimu yetu nani ataiokoa.Sijui kipi kigumu kutekeleza msimamo wa awali mpaka wameufanyia "harmonization"!

Tusipoangalia na kuendelea kutenda kwa namna ya sasa basi tutakuwa taifa la ajabu sana duniani.Taifa lisiloweza kutekeleza mipango yake yenyewe kwa kuhofia kuwaacha wengine nje ya utaratibu rasmi hata kama hawaonewi!

Hii serikali kwa muendelezo wa mambo kama haya no wonder wengine wakailebo "impotent".

Pia nina wasiwasi hata hizo 31% za wanaoitwa wamefeli huo mtihani ni baada ya hiyo "harmonization" ya kushusha kutoka 0-30 mpaka 0-20.

Sekta ya elimu inaenda kama gari bovu.Walisema wamebadili madaraja ya K4 na K6 badae wakakana na kusema utaratibu wa zamani utaendelea.Barua ya katibu mkuu ikakanushwa kirahisi tu na yule jamaa mwenye jina la watu bungeni!
 
Wakati watanzania wakisubiri kwa shauku matokeo ya kidato cha pili mwaka 2013, imebainika kuwa serikali imetoa AGIZO wanafunzi wote waliofeli mtihani huo kuendelea na masomo ya kidato cha tatu, huku wakisoma MAFUNZO ya kurudia mtihani wa kidato cha pili.

Source: Mwananchi

MY TAKE:
This kind of insanity can only happen in Tanzania, a country where even a corpse can head the country without any complaints from the citizens!
 
Sasa hiyo taarifa inaonesha jinsi viongozi wote kwenye Wizara ya Elimu walivyo MAJANGA KWA TAIFA LETU
 
Siyo kitu kigeni kwani hata waliofanya mtihani mwaka 1993 form two walipita wote.
 
Kama iliwezekana kufuta matokeo ya Kidato cha Nne na kuyatangaza upya, hivi ni nini kitakachoshindikana kwenye elimu?
 
Back
Top Bottom