Waliofeli Form Four kurudia mitihani bure mwaka huu?

Waliofeli Form Four kurudia mitihani bure mwaka huu?

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,347
Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo alipozungumza na gazeti la HabariLeo kuhusiana hatua zitakazochukuliwa na serikali kutokana na idadi kubwa ya watahiniwa wa kidato cha nne kupata sifuri, amedai kuwa serikali inafikiria warudie mtihani mwaka huu.

Amesema serikali inaangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi. Likipita hilo la kurudia mtihani, serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi.

Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za serikali.

Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema, matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea. Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.

Source: Habari Leo

N.B: Kwa mahesabu ya haraka haraka kama serikali itaamua kuwalipia wanafunzi zaidi ya 240,000 waliofeli kurudia mitihani itagarimu sio chini ya Sh. 8,400,000,000.

============ Updates ===========

Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo alipozungumza na gazeti la HabariLeo kuhusiana hatua zitakazochukuliwa na serikali kutokana na idadi kubwa ya watahiniwa wa kidato cha nne kupata sifuri, amedai kuwa serikali inafikiria warudie mtihani mwaka
huu.

Amesema serikali inaangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi. Likipita hilo la kurudia mtihani, serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi.

Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za serikali.

Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema,matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea.

Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.

Source: Habari Leo
 
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alipozungumza na gazeti la HabariLeo jana kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali kutokana na idadi kubwa (asilimia 60.6) na kama watajiuzulu alisema:

"Si sahihi kulizungumza hilo la kujiuzulu, kwa kuwa liko nje ya mipaka yangu ya kazi, si suala la Wizara ya Elimu pekee...lakini kuhusu hatua zitakazochukuliwa kwa waliopata sifuri, Serikali inafikiria warudie mtihani mwaka huu. Katika kuchambua hilo, tumeangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi, likipita hilo la kurudia mtihani, Serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi." alijibu waziri Mulugo.

Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za Serikali.
 
hizo hela wangepeleka kuboresha maabara na kununua vitabu!
 
Ngoja na mimi niliyefeli enzi ya nyerere nikarudie nije niokoe taifa hili
 
Gharama hizo ni kubwa sana ni lazima Waziri wa Elimu awajibike. Hatuwezi kuwalipia watoto hawa mara ya pili kwasababu ya usingizi wa mtu tuliyempa mamlaka awaelimishe vijana wetu.
 
Kwanini inakuwa ni rahisi kuingia hasara kwa kulipia marudio ya mtihani lakini inakuwa ni ngumu wao kujiuzulu,au kwasababu hizo hela hazitoki mfukoni kwao? waache mchezo wa kuigiza.......hembu watuambie hao wanafunzi wakifeli tena baada ya kurudia mtihani nini kitafuata......Serikali imejaa wasanii kila kona na wananchi ni kama tumezoea kuongozwa kisanii, Mungu asaidie hili TAIFA.
 
Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema, matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea. Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.

Hapo kwenye red ndo tatizo linapoanzia, Nchi moja, Wizara moja sera tofauti- Vyuo vikuu, wanaopata 1st class ndiwo mara nyingi wanaopata nafasi ya kuwa ma-TA, Sekondari wanaofeli ndo wanaenda kuwafundisha wenzao; kwanini wasifeli watakaofundishwa. Ukweli ni kwamba mtoto wa Form Four anaepata Division 4, huyu aidha hajafundishwa au hana uwezo, hivyo hawezi kufundisha watu-Huu ni ujinga toka kwa NW, hwcome aje statement ya ajabu namna hii. Wekeni utaratibu huu, kwa sasa hakuna homa ya walimu saaaana kama kipindi hicho, japo hawatoshi so pigeni marufuku form four kusomea ualimu, only form Six leavers wasomee diploma ya ualimu wawe walimu wa Primary!

Only University graduates wawe walimu wa Sekondary. All form four wa point hizo waende vocational training tu kama hawataki ku-resit. Fanyeni rationalization ya mishahara ya Walimu na affordable accomodation allowances; Fikisheni Umeme katika shule zote Tanzania; Imarisheni miundombinu ya Maji, rudisheni kitengo cha ukaguzi wa waalimu/ au kiwe active kama bado kipo, pigeni marufuku waalimu kuuza karanga na mihogo, Acheni ujinga wa kununua ma-VX V8 ili fedha mu-invest katika elimu, Hivi nyie mawazir huwa hamuaoni haya mnapoenda nje ya Nchi?

Pia ni ujinga na kumuumiza mtoto kumfundisha katika lugha mbili katika miaka 12, Just fundisheni Kiingereza katika Level zote ili iwe lugha anayoanza nayo-Fanyeni haya then muone kama kutakuwa na Zero hizi. Acheni Blahblah jamani tunazidi kutengwa na Dunia. Mtapeleka wapi vijana wenye D ya kiswahili?

Inauma sana, tena sana!
 
Gharama hizo ni kubwa sana ni lazima Waziri wa Elimu awajibike. Hatuwezi kuwalipia watoto hawa mara ya pili kwasababu ya usingizi wa mtu tuliyempa mamlaka awaelimishe vijana wetu.
Maneno yako murua kabisa ila ukiwaambia hivyo wanachukiiiiia........siku na zipite hawa watu waondoke.
 
:crying:
Gharama hizo ni kubwa sana ni lazima Waziri wa Elimu awajibike. Hatuwezi kuwalipia watoto hawa mara ya pili kwasababu ya usingizi wa mtu tuliyempa mamlaka awaelimishe vijana wetu.

Ni kweli na ni dhahiri hawa watu hawakua serious katika marking maana nimesikia mwanafunzi wa Green Acres ambaye hakufanya mtihani kaandikiwa kafanya lichaya ya hivyo pia kajaziwa grade nzuri tuu. Je hizo grade mezipatia wapi??? pia solution sio baraza LA MAWAZIRI kujiuzuli maana hata wakijiuzuli bado taifa limeshaangamia.
 
Wakirudia Mtihani ndiyo watapa One?Mulugo mawazo Mgando hayo, tibuni tatizo kwanza.
 
Mkuu Zinedine umemaliza kila kitu hapa.
Huo ndio ukweli tena mchungu lakini ndio dawa.
Blah blah za Mkwele, Kawambwa na Mulugo hatuzitaki tena, tuna taka hatua madhubuti.
 
Huwa wanasolve tawi la tatizo badala ya mzizi wa tatizo.
 
.
Kuna kitu hapa Serikali & Watanzania kwa ujumla hamtaki kukubali ukweli ...

Hao wanafunzi hata wakirudia mitihani yao WATAFELI tena! ...

Asilimia kubwa ni mbumbumbu na hawajaelimika & hata IQ zao zipo chini, hata ufahamu tu wa general knowledge nao upo chini

Tatizo ni kubwa kuliko mnavyofikiria

=====
Hebu - Download hii Report alafu muangalie wenyewe jinsi wanafunzi wetu wa Tanzania wanavyojibu mitihani alafu toa pendekezo mwenyewe je? wakirudia mitihani watafaulu?

Pimeni wenyewe hii ndio hali halisi ya Elimu ya Tanzania

https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=84127&d=1361514648

=====
EMT . Mzee Mwanakijiji .
.
===
 
:crying:

Ni kweli na ni dhahiri hawa watu hawakua serious katika marking maana nimesikia mwanafunzi wa Green Acres ambaye hakufanya mtihani kaandikiwa kafanya lichaya ya hivyo pia kajaziwa grade nzuri tuu. Je hizo grade mezipatia wapi??? pia solution sio baraza LA MAWAZIRI kujiuzuli maana hata wakijiuzuli bado taifa limeshaangamia.
Mkuu emilwayne wewe bado upo usingizini?
Hiyo issue ya wanafunzi wa Green Acres ameshatolewa ufafanuzi tena humu humu na kuna kuna topic yake humu JF.
Kifupi ni kwamba hakuna mtu aliyeonewa mpaka sasa na Necta na kama kuna anayehisi kaonewa anaweza kukata rufaa NECTA ili mtihani wake usahihishwe upya. Matokeo yaliyopo humu mtandaoni yako sawasawa tofauti na huyo mkuu wa shule alivyopotosha.

Huyo mkuu wa shule ya Green Acres alikurupuka ili kujitetea kukwepa mzigo wa lawama kutoka kwa wazazi waliotaka kumjia juu kwa matokeo mabaya ya shule yake.

Kwa suala la kujiuzuru mawaziri haliepukiki hata kidogo, tunapima utendaji wao kwa mwenendo wa elimu yetu hususani matokeo ya mitihani.

NECTA kazi yao ni kutunga, kusimamia, kusahihisha mitihani na kutoa matokeo.
Kwa matokeo yaliyotoka mpaka sasa sioni wapi NECTA unaweza ukaihusisha na uzembe mpaka wanafunzi wengi wamepata sifuri.
 
Last edited by a moderator:
Mulugo hapo ndipo anapokuja kujichanganya na kuifanya hiyo Wizara kuwa Hovyo kabisa.
Yaani ukiweka Kwambwa na Mulugo ndio unapopata 60% wanafeli
Kuna watoto wangapi wmeandika madudu, wangapi hawakuingia chumba cgha Mtihani Wangapi wanaishi mbani na walikuwa katika mabweni leo uwaambie warudi waanze maandalizi ya Mtihani Du ni NDOTO
 
Kwahiyo sababu ya kufeli ni kwamba watoto wetu hawakujiandaa au hawakuandaliwa? Na sababu ya kurudia mtihani tena ni kutoa fursa kwa watoto wetu kujiandaa, kuandaliwa, au kujaribu tena bahati zao? Nina wasiwasi mkubwa kwamba vyombo husika vinaweza kuligeuza suala hili likae kisiasa zaidi na watoto wetu wakirudia mitihani, wengi watapasishwa hata kama hawana uwezo ili mradi tu takwimu husika ziwe mtaji wa kisiasa/political asset, na kuondokana na hali ya sasa ambapo matokeo husika ni a political liability;

Hivi Tutafika kweli?
 
Back
Top Bottom