Waliofeli Form Four kurudia mitihani bure mwaka huu?

Waliofeli Form Four kurudia mitihani bure mwaka huu?

Wakifeli tena?
Hii ni sawa na kuchota maji baharini na kuyamwagia kwa Mto.
Tatizo la kuferi sio suala la leo wala jana hawa watu hawana msingi toka form darasa la kwanza kwenye the so called shule za kata.
Nina wasi wasi next year NECTA watapewa target ya kuwa mkirudia matokeo kama ya mwaka jana wote mtajiuzuru
Maana ndo namna hii serikali inavyofanya kazi
 
Je waliofeli mwaka jana unakuwaje?
Hii inaonesha kushindwa kwa serikali
 
1/Je hili ndio suluhisho la kufeli kwa wanafunzi wengi AU mpango wa kuwafariji waliofeli?

2/Tatizo lililopelekea wanafunzi wengi kufeli ni maandalizi duni ya kielimu AU ni aina ya mtihani waliofanya?

3/Kuna uhusiano gani kati ya kufeli kwa kupata ziro na kurudia mtihani mwaka huu?

4/Je inapasa wanafunzi warudi shuleni kufundishwa upya AU warudie kufanya mtihani tu?

5/Lengo la serikali kutoa elimu ni ili watu waelimike AU wafaulu mtihani tu?

6/Lengo la mtihani ni Kupima uelewa wa wanafunzi AU ni daraja tu la kufaulisha wanafunzi?

7/Hitaji la wanafunzi waliofeli ni Pesa za kulipia mtihani AU elimu bora itakayowezesha wao kufaulu vizuri mitihani?
 
Hiyo bilioni 8.4 na ushee ambayo wanataka kutwanga maji kwenye kinu, wangewekeza kwa miaka mitano mfululizo iliyopita tusingekuwa tunazungumza machungu haya ya wadogo zetu.
 
ELIMU YA NAPE NNAUYE.

Mwaka 1993 alifeli darasa la saba. Wakati ule jina halali la Nape akiitwa Nahum Nnauye. Waliosoma nae wanakumbuka. Bt akafanyiwa mpango na kupewa jina la Nape Mkumbo Nyagicha mtoto masikini wa Kinyiramba, aliyefaulu lakini familia yake haikuwa na uwezo wa kumsomesha.

Mwaka 1994 Nahum Nnauye akajiunga na shule ya sekondari ya kutwa Ngudu wilayani Kwimba akiwa na jina jipya la Nape. Mwaka 1995 akahamishiwa shule ya Sekondari Nsumba kwa kutumia title ya baba yake Mzee Moses Nnauye.

Mwal 1997 akafeli form four kwa kupata division four ya point 29 akiwa na D 4, c 1 na F 5. Akareseat mara 2 bila mafanikio pale Butimc TTC ambacho ni kituo cha watahiniwa binafsi. Mwaka 1999 na mwaka 2000.

Akakata tamaa na hatimaye mwaka 2001 akaamua kwenda kusoma cheti cha Uhazili (cert of secretarial services) katika chuo cha Kivukoni. So kabla sijaendelea naomba ieleweke kuwa Nahum Moses Nnauye (Nape) hajawahi kusoma form 5 shule yoyote duniani. Kama anabisha aje hapa tumuulize maswali ya Geography 1 au Ecomics 2 uone atakavyochanganyikiwa. Kwanza hajui kama kuna paper 1 na 2 A.level, atasemaje amesoma A.level?

So akatumia cheti chake cha uhazili kuomba diploma pale chuo cha Diplomasia kurasini. akapata na akaanza kusoma. Mwaka mwaka 2002 akafeli kuendelea na 2nd year baada ya kupata suplimentary 4 ktk masomo 6 aliyokuwa akisoma. So kwa kifupi akadsco. Hivyo naomba ieleweke kuwa huyu jamaa anayejiita Nape hajawahi kutunukiwa diploma yoyote kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini. Kwanza asikidhalilishe chuo maana pale hakuna Diploma ya mwaka mmoja. kama anabisha aupoad picha yoyote hapa alipokuwa anatunukiwa hiyo diploma.

Mwaka 2004 akatumia cheti chake cha form four kuomba degree India kwa kusaidiwa na mwandishi mmoja mashuhuri nchini kwa kuwatafutia vyuo vya nje watu waliofeli.

Na akapata kwa masharti ya kusoma miaka minne. Ikumbukwe India ni nchi yenye vyuo vya hovyo sana duniani, na ni miongoni mwa nchi ambazo hata kama una zero unaweza kusoma Bachelor bila matatizo yoyote hadi ukahitimu. Reffer kesi ya Mr.Andekisye, Lecturer aliyefukuzwa kazi Arusha University kwa kusoma elimu feki India. Andekisye aliajiriwa kama mhadhiri wa Marketing na Business Mathematics akidai ana MBA kutoka India.

Bt ilipofuatiliwa ikagundulika ni kweli ana Masters ya MBA bt hajawahi kusoma Bachelor. Alichomoka na Diploma yake ya Ualimu (Mathematics & Physics) kutoka Monduli TTC akaaply Masters India akapata akaenda kujoin. Sasa imagine mtu anatoka Diploma anakwenda Masters sembuse Nape kusoma bachelor?

Nape akapata degree yake fake ya psychology ambayo ndiyo aliyoitumia kuomba masters mzumbe. Na mzumbe hakukabidhi cheti zaidi ya kile cha degree yake ya India.
Kama anabisha aweke vyeti vyake vya o.lel na a.level hapa.

Huyo ndiye Nahum Moses Nnauye anayejiita Nape. Katibu mwenzezi wa Chama cha Mapinduzi CCM na mgombe ubunge ubungo mwaka 2010, wakati ule akijaribu kushindana na Genious John Mnyika aliyepata A 9 O.Level yeye akiwa na D 4 tu.
 
Zaidi ya TZS 8.4 bilioni zitateketea. Hiyo pesa imetakata sana kwa uchaguzi wa srikali za mtaa mwaka ujao. CCM bwana kwa mikakati ya kifisadi ...!
 
Tatizo letu Tanzania kubwa ni kwamba ni wazito sana kubadilisha mfumo hata kama matunda yake ni mabaya. Ni wakati wa kujiuliza ni jinsi gani gani tunaweza kuongeza kiwango cha elimu lakini kuzingatia nchi yetu ni masikini. Ni lazima tufikirie tofauti kwenye jinsi ya kutumia pesa na rasilimali. Hivyo tuje na mawazo mapya badala ya kulaumu au kukazania System ambayo haiendi na wakati. Baadhi ya mawazo yangu ni haya hapa

Tanzania haitaweza kufanya yote haya niliyoyataja kwa Tanzania nzima kwani wananchi wa Tanzania wametapakaa sana nchini na si rahisi kujenga shule kila mahali zenye kila kitu. Sasa badala ya kupiga debe ya elimu bure ni lazima tujiulize je ungekuwa na budget hiyo ungefanya nini tofauti kufundisha watoto wote.

1. Wanafunzi wa vyuo vikuu wanao chukua mikopo na dhamana ya serikali ni lazima wafundishe miezi sita kabla ya kupewa vyeti vyao kama ilivyokuwa JKT. Hii itasaidia kupunguza gharama sana, kuongeza uzalendo na kuhakikisha jamii yote inasaidiwa.
2. Kwenye ujenzi wa shule za Primary na Sekondari wakijenga wahusishe wenyeji. Hii itasadia wenyeji kuona ni part ya maendeleo yao na hii tabia wanafanya sana wachagga badala ya kusubiri serikali ifanye kila kitu. Ukweli ni kwamba utamaduni huu umeifanya Kilimanjaro kuwa miongoni mwa sehemu zenye elimu kwa watoto wengi kuliko sehemu nyingine.
3. Boarding School- Serikali ianzishe Boarding school kwa wilaya ambazo zina watu wachache hii itasaidia badala ya kuwa na shule nyingi kila mahali ni bora uwe na shule moja kubwa sehemu moja na watoto wa Primary na sekondari waweze kwenda.
4. Serikali isiruhusu shule zinazofelisha zifungwe au wabadilishe uongozi. Kama tatizo ni utamaduni wa jamii kama shule nyingi za Zanzibar wapeleke watoto shule za boarding.
5. Shule binafsi-Serikali ipige mahesabu ya gharama kwa mwanafunzi mmoja na iruhusu watu binafsi kujenga shule za kisasa na kuwapa hizo pesa shule zikifunguliwa kwa mwanafunzi. Kama zinafelisha serikali inakata pesa maana hii itapunguza utaratibu wa serikali kujenga shule kila mahali.
 
Warudie wanafaunzi wote waliomaliza form four Mwaka jana siio fair kabisaaaa kuwatenga
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Labda aseme watakaporudia kusahihisha huo mtihani wa marudio watarahisisha alama za ufaulu, azawaizi sioni lojiki katika hili
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo alipozungumza na gazeti la HabariLeo kuhusiana hatua zitakazochukuliwa na serikali kutokana na idadi kubwa ya watahiniwa wa kidato cha nne kupata sifuri, amedai kuwa serikali inafikiria warudie mtihani mwaka huu.

Amesema serikali inaangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi. Likipita hilo la kurudia mtihani, serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi.

Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za serikali.

Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema, matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea. Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.


Source: Habari Leo

kweli ukistaajabu ya mussa.....
 
Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo alipozungumza na gazeti la HabariLeo kuhusiana hatua zitakazochukuliwa na serikali kutokana na idadi kubwa ya watahiniwa wa kidato cha nne kupata sifuri, amedai kuwa serikali inafikiria warudie mtihani mwaka
huu.

Amesema serikali inaangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi. Likipita hilo la kurudia mtihani, serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi.

Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za serikali.

Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema,matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea.

Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.

Source: Habari Leo
 
eti daraja la nne ndo wataenda vyuo vya ualimu...SMH
Kesho tena mje muwasingizie clouds fm na FB wamefelisha watoto wetu.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Ni jukumu la wazazi sasa kuwasaudia watoto wao kujiandaa upya.
Mzee Mwanakijiji, wanafunzi hao hawakushindwa kwa sababu mitihani ilikuwa migumu bali hawakuwa na maarifa (knowledge), kwa hiyo hata kama watarudia mtihani huo mara mia hawatafaulu.
 
ELIMU YA NAPE NNAUYE.

Acha kutumiwa kama mtaji wa kisiasa.

Tujadili elimu ya Nape au serikali kutaka kungia gharama ya Sh. 8,400,000,000 kuwalipia wanafunzi zaidi ya 240,000 waliofeli kurudia mitihani?
 
Ni kweli yatizo ni knowledge na yote imetokana na kuporomoka hali ya maisha na uchumi;ndipo hapo uchumi wa mwalimu unapokua duni ari ya kufundisha itatoka wapi?pia mzazi nyumbani maisha magumu kujikimu,vifaa vya mtoto shule;ada;michango;tuition;nauli za basi kwenda na kurudi shule ni mzigo kwa mzazi
 
eti daraja la nne ndo wataenda vyuo vya ualimu...SMH
Kesho tena mje muwasingizie clouds fm na FB wamefelisha watoto wetu.

Hata waliopata sifuri ndiko watakapoelekea.
 
Warudie wanafaunzi wote waliomaliza form four Mwaka jana siio fair kabisaaaa kuwatenga

Nilikuwa nafikiri hivyo hivyo. Kama ni kurudia na kulipiwa na serikali basi warudie wote.

Sioni justification ya waliopata sifuri walipiwe halafu waliopata four wasilipiwe.

Hata hivyo, the whole idea ya kuwalipia, I do't get it.
 
Back
Top Bottom