Huo ni upumbavu na umbumbu wa mawazo nafikra,kama mwanafunzi akiwa shuleni na walimu alishindwa ,mtihani,je akiwa peke yake kama mtahiniwa binafsi ndo ataweza?labda kama mnatka kuwapa mtihani kama wa form one,maana tumesh wazoea nyie kuharibu elimu ya watoto wetu kisa watoto wenu wasoma ulaya.Kwanini hizo pesa za kugharimia mtihani hamkuwapa walimu ili wawa fundishe watoto bila kinyongo? au ndiyo hako kamtindo kenu mliko gundua siku hizi kakuwachotea alama za bure watoto mmeona dili? darasa la saba mlishusha alama kutoka 100 hadi 70,kidato cha pili mliwaongezea watoto alama 12 kwa kila somo,hivi mnamdanganya nani? basi wapeni alama watoto wakiwa nyumbani kwao,mnasema waende shule kufanya nini kama baadae mnawapa alama za bure ili wafaulu?
Baadhi ya mawaziri waliopita walishauri vibaya serikali wakidai watoto wana soma masomo mengi ni mzigo kwao ndiyo maana wanafeli,jambo ambalo siyo kweli kutokana na ukweli kuwa:
1.Mwanafunzi aliyekuwa anasoma PCM,PCB,PGM,CBG alikuwa hasomi FINE ART,MUSIC,UCHAPAJI WALA COMMERCE,na aliyekuwa anasoma ushonaji,upishi alikuwa hasomi HGL,HGK NK.
2.Wanafunzi funzi siku hizi wanasoma masomo yanayo fanana ndiyo maana wanafeli,kwani mtoto mwenye kipaji cha kuchora,analazimika kusoma sayansi au masomo ya lugha jambo ambalo linamfanya ashindwe kumudu,kisha anaamua kuchora picha wakati swali lilitaka aeleze athari za vita ya majimaji kwa mfano. Sasa ule mchoro lingekuwa somo siangepata A huyo? sasa sifuri zingetoka wapi? na wale wanao andika nnyimbo za bongo flava,kama somo la mziki lingekuwepo siangefaulu huyo?
3,Watoto wanaosoma masomo yanayo fanana nchi nzima baadae mtakuja muwaajiri wapi?
Halafu waziri wa elimu anatudanganya eti wanafunzi wamefeli shule nyingi zinakosa maabara,ni kweli,lakini miaka iliyopita mbona walifaulu shule hizohizo je,makta,maabara,vitabu na hao walimu walikuwapo/zilikwapo? mbona mlifika kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri bungeni na mkawapa zawadi mkawasahau hata walimu japo hata kuwashika mkono tu.
Imekuwa ni tabia sasa kwa baadhi ya viongozi wa serikali kuwashauri/kuishauri serikali vibaya kwa maslahi yao binafsi,hata katika kipindi cha sensa waliamua kutumia kigezo cha mgomo wa walimu kuwanyima walimu sensa eti wataivuruga kumbe walitaka kuuza nafasi na kuwapa ndugu na jamaa zao.
4.Serikali yenyewe mwakajana ilifunga shule kwa muda mrefu kwa kisingizio cha sensa,ambapo walimu wachache tu walishiriki zoezi hilo,na wengine walikaa tu nyumbani,mlitegemea miujiza gani katika matokeo?
5.Ni waziri gani anaweza kufanya kazi kwa ufanisi huku akiwa anabubujikwa kwa na machozi kisa mshahara mdogo,na maslahi mengine anapunjwa?mlitegemea walimu wafanyaje kama wanachoomba hawapewi na kuambulia vitisho?
MAONI YANGU:
1.Kaeni meza moja na walimu mzungumze juu ya masilahi yao ili walimu warudishe moyo wa kazi
2.Rudisheni masomo ya biashara,uchoraji,kilimo,upishi,ushonaji na uchapaji ili watoto wawe na uwanja wa kuchagua masomo wanayoweza nayanayo weza kuwapa ajira.
3.Wizara ya elimu ni pana mno kiasi cha waziri mmoja hata akawa mahiri hawezi kuimudu,maoni yangu,kuanzia chekechea hadi darasa la saba iwe wizara moja,sekondari zimekuwa nyingi sasa,iwe wizara na vyuo vya ufundi,na ualimu iwe pia wizara yake na vyuo vikuu viwe na wizara yake na wizara ambazo hazina changamoto nyingi ka michezo,habari,nk zinaweza kuunganishwa pamoja.
4.Nchi nzima itumie kitabu cha aina moja kwa shule zote,kuliko ilivyo sasa kila mtunzi anapeleka kitabu kitumike shuleni.
5.Ikumbukwe kuna kipindi walimu wa shule za msingi walipata mafunzo ya ualimu kwa muda wa mwaka mmoja tu na huku ufaulu wao ukiwa chini,serikali imesahau kuwapa mafunzo kazini ili wajenge msingi mzuri kwa wanafunzi wa shule za msingi,hivyo wapate mafunzo kazini.
6.Waziri katika matatizo aliyoyataja,hakusema kama shule nyingi za kata wanafunzi hawapati,uji wala chakula cha mchana shuleni,serikali ifanye mpango watoto wale shuleni angalau hata uji tu.Haiwezekani mtoto aokea mbagala akasome bunju bila kula halafu mtoto huyo utegemee apate dision ONE.
7.Shule nyingi za kata hazina madarasa ya kutosha,msongamano madarasani ni mkubwa,wananchi siku hizi hawataki kuambiwa juu ya kujitolea ili kukamilisha madarasa katika shule zile.Sasa napendekeza mahabusu na wafungwa wakafanye kazi ya ktengeneza matofali,wajenge,wapaue na kufaya finishing ,huku serikali na wananchi wakichangia bati na saruji na mbao,kuliko kuwarundika tu magerezani bila kazi.
Maoni yangu kwa leo ni hayao,
FATHER OF HISTORY natoweka,byeeeeee!
H
Naibu Waziri wa Elimu Philipo Mulugo alipozungumza na gazeti la HabariLeo kuhusiana hatua zitakazochukuliwa na serikali kutokana na idadi kubwa ya watahiniwa wa kidato cha nne kupata sifuri, amedai kuwa serikali inafikiria warudie mtihani mwaka huu.
Amesema serikali inaangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi. Likipita hilo la kurudia mtihani, serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi.
Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za serikali.
Kuhusu idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu alisema, matokeo hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea. Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.
Source: Habari Leo
N.B: Kwa mahesabu ya haraka haraka kama serikali itaamua kuwalipia wanafunzi zaidi ya 240,000 waliofeli kurudia mitihani itagarimu sio chini ya Sh. 8,400,000,000.