Waliobanwa katika ajali wafariki

watawala wajue NO LONGER AT EASE!Hii ni dharau iliyopitiliza,RC BENDERA itakua alipewa taarifa akadharau au kamtupia mtu mzigo.imekua ni kawaida yake
 

Hapo akwenye blue,
Tuchukue hatua gani ??
Tununue crane kubwa ili zikae standby ??
Maana katika tukio lile, ilihitajika crane ya kunyanyua magari mazito ili kunusuru maisha ya watu wale.
Crane iliyohitajika ni kama hii hapa kwenye picha...
 
kama walikua wamebaniwa kwenye cabin ,si kwamba kilitakiwa kifaa cha kukatia vyuma ili kuwanasua na si crane?.

Kama wangekua wameangukiwa na cabin au bodi ndo nadhani ingetakiwa crane.
Mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa husika waachie ngazi haraka sana kwa ujinga huu.
 

Kabla hujatoa maoni yako, hebu tembelea video ya tukio ili uone picha kamili ya tukio.
Tembvelea hapa.....
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili wamebanwa na lori lililosheheni viazi. - YouTube

Ukishaona tukio lilivyo, rudi hapa uombe radhi kwa kejeli zako ulizotoa.

Kwa kukusaidia tu, tukio husika lilihitaji uwepo wa 'heavy duty crane' ya kuwezesha kunyanyua vitu vilivyowabana watu wale.
Pia kulihitajika vifaa vya kukatia vyuma ili kuwanasua watu wale.
Sasa, hebu sema kama serikali isingeweza kuleta vyombo hivyo haraka katika eneo la tukio.
Sipati picha kama ingekuwa ni ndugu yako amebanwa pale kwenye ajali !!
Sipati picha kama ingekuwa ni waziri, mbunge, au mtoto wa Kikwete angekuwa amebanwa pale kwenye ajali !!
 
Mkuu Elungata heshima mbele,Ufisadi nyuma. Nashukuru sana kwa kumjibu Huyo mdau.
Hao Marehemu walibanwa kwenye cabin...Kama kungekuwa na kifaa cha kukatia (Hydraulic Rescue Cutter) ingeweza kana kuokoa maisha ya hawa ndugu zetu. Kuna wadau Kama Huyo bwana huwa wananichosha kwa kuja na majibu mepesi kwenye masuala mazito. Crane haikuhitajika kwenye kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu hapo Juzi.
 
Mbona siwaoni akina Ritz & co kwenye huu uzi? Nawapa pole sana familia za wafiwa na watanzania kwa ujumla

kuchangia threads kama hizi haipo kwenye mkataba wao wa lumumba ...watakatwa hela wakithubutu, labda uzi ungeanza na neno wachaga
 
Majibu ya kesho yatakuwa ni kama ifuatavyo:
Ndugu wananchi serikali ingependa kutoa tamko kuhusu ajali mbaya ya magari ya mzigo ambapo watu watatu walifariki, baada ya serikali kupata taarifa hizo utaratibu wa kuwakwamua majeruhi ulianza kufanyika mara moja. Serikali kupitia kitengo cha maafa chini ya ofisi ya waziri mkuu iliwasiliana na mkuu wa mkoa wa Pwani wakawa eneo la tukio muda wote wakijaribu kuwanasua majeruhi. Ndugu wananchi wakati mipango ya kuwanasua ikiendelea kufanyika mitambo mikubwa ilibainika kutakiwa kuwepo kutokana na ukubwa wa tatizo lenyewe, tuliwasiliana na makampuni makubwa ya ujenzi jijini Dar es Salaam ambao kulingana na taratibu zao mitambo hiyo lazima ipate vibali ili kuruhusiwa kutoka eneo la kazi, wakati huo ni takribani saa kumi na moja zilikuwa zimepita tangu tuanze kufanya harakati kuwa nasua majeruhi. Safari ya kwenda ilanza ambapo kutokana na ukubwa wa mitambo uharaka wa kuwasili eneo latukio iliweza kuchelewa na kuweza kusababisha vifo hivyo.

Hii ndiyo itakuwa ni maneno yako kujinasua na kadhia hii ya serikali yetu kujali watu wake kulingana na NAFASI ZAO. SERIKALI INAYOBAGUA WANANCHI WAKE NI SAWA NA NYUMBA ILIYOGAWANYIKA YENYEWE KWA YENYEWE NA HAIWEZI KUSIMAMA KAMWE.
 
NDIYO TANZANIA hiyo. MTALALAMIKA WEEE LAKINI UCHAGUZI UKIFIKA, CCM OYEEE.
TUNAWAFAHAMU SANA NINYI NDUMILA KUWILI ZERO BRAIN. ENDELEENI KUSINZIA SINZIA NA KUWA WAOGA. UNAFIKI NA UOGA SIO MZURI WATANZANIA WENZANGU.
 
mwisho SERIKALI IMEJIPANGA TUKIO KAMA HILI HALITATOKEA TENA!
 
inauma sana kaka! Utaskia imesababishwa na chadema,ngoja tusubiri.
na bado watanganyika nagombania mipaka, mnataka watu zaidi mpate kuwatesa. Leo malawi kesho zanzibar halafu mlima kilimanjaro ili mradi shida tu
 
Idara ya Zimamoto na na Uokoaji iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu wake wawajibike kisiasa kwanza kabla ya watendaji wengine wa serikali kufuata. Ilishawahi kutokea huko nyuma kwa Waziri wa Wizara hii kuwajibika. Hii ni kama kweli wanaona maisha ya watu yana thamani stahili..
 
Nmeichoka tz, hapa sio mahali salama pa kuishi. Siwezi kuifanyia chochote tz wakat serikali yake hainihitaji kwa namna yoyote ile. RIP my fellow poor
 

Mkuu mbona niliwahi kusikia kuna ketengo maalumu kilihanziswa kwa ajili ya kushughulikia majanga - huokohaji ukiwa ndio ungepewa kipa umbele zaidi, hiyo ilishia wapi TENA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…