DOKEZO Walimu wa Shule ya Gisela (Ukonga) tuna hali mbaya, hatulipwi mishahara wala malipo ya NSSF

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mfanyakazi wa Shule ya Msingi Gisela N/P School (Private) iliyopo Kipunguni B Ukonga Ilala hapahapa Dar es Salaam, tunadai mishahara ya miezi 3 mfululizo, ya tangu mwezi wa 7 mpaka mwezi huu unaoenda wa kuwa wa 11, 2023.

Sambamba na hilo tuna malimbikizo ya mishahara yetu ya nyuma tangu Mwaka 2019 na ikiwemo ya kipindi cha Corona.

Vile tuna madai ya malimbikizo ya maingizo ya fedha zetu katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Tunaomba Mamlaka za Serikali ziingilie kati ili tupate mishahara yetu maana tuna hali mbaya sana.
 
Aisee poleni, si mnsaini mkakataba kuwa mtavumilia pale mshahara ukichelewa kutoka.
 
poleni sana kwa changamoto hiyo, tunaimani mamlaka zitalifanyia kazi swala hili
 
Ni kama vile uwe umeolewa alafu mume uliyenae anakupa mkong'oto , afu unalalamika jamani napigwa, polisi nisaidieni. Jisaidie kwanza wewe Kwa kuondoka hapo ndipo udai malimbikizo Yako.
 
Mimi ni Mfanyakazi wa Shule ya Msingi Gisela N/P School (Private) iliyopo Kipunguni B Ukonga Ilala hapahapa Dar es Salaam, tunadai mishahara ya miezi 3 mfululizo, ya tangu mwezi wa 7 mpaka mwezi huu unaoenda wa kuwa wa 11, 2023.

Sambamba na hilo tuna malimbikizo ya mishahara yetu ya nyuma tangu Mwaka 2019 na ikiwemo ya kipindi cha Corona.

Vile tuna madai ya malimbikizo ya maingizo ya fedha zetu katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Tunaomba Mamlaka za Serikali ziingilie kati ili tupate mishahara yetu maana tuna hali mbaya sana.
Hizi shule za private zimekuwa na shida sana ya kulipa mishahara wakati wanapokea pesa nyingi na access ya kukopa kuwalipa mishahara wafanyakazi wanayo.
 
Shule ina wanafunzi wangapi na ada ni kiasi gani?
 
mara nyingi matatizo haya huwa yanasababishwa na:
baba: mkurugenzi wa shule
mama: mkuu wa shule
mtoto: mhasibu mkuu

ukikuta shule iko hivyo, basi walimu MPAKA MSEME....
 
Hizi shule za private zimekuwa na shida sana ya kulipa mishahara wakati wanapokea pesa nyingi na access ya kukopa kuwalipa mishahara wafanyakazi wanayo.
Shangaa ndugu. Wanakusanya mabilioni lakini mishahara kwa walimu ni kiduchu sana. Hawa waundiwe mamlaka ya kuwadhibiti. Kwanza wanapandisha ada kila wanapojisikia, na wakati mwingine hulazimisha wazazi wachangie ujenzi wa majengo na fence ambavyo ni mali zao. Hii si sawa kabisa.
 
Hapo dawa ni kuhoji mapato na matumizi ya fedha za kampuni inayomiliki hiyo shule maana huenda nidhamu ya fedha hamna.
 
Back
Top Bottom