JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
Wakizungumza na waandishi wa Habari leo, wafanyakazi hao wamesema kuwa suala la ulipwaji wa mishahara limekuwa changamoto kubwa, huku michango yao NSSF ikiwasilishwa kwa kusuasua.
“ Tangu nimeajiriwa hapa, tumekuwa tunalipwa kwa kusuasua sana, kwa mwaka wanaweza kutulipa miezi mitatu hadi minne, na miezi mingine tukabaki tunadai, sasa tangu mwaka huu umeanza shule hii haifanyi kazi,” Amesema Mary Mshana….
“ Wazazi ambao walikuwa na watoto hapa waliwaondoa, na wale ambao tulitarajia kuwasajili kidato cha kwanza mwaka huu, hakuna mtoto hata mmoja aliyekuja, mpaka sasa shule haina mwanafunzi hata mmoja,”
Wafanyakazi hao wanasema kuwa kutokana na hali hiyo, wamekuwa wakifuatilia hatma ya ajira yao kutokana na kukaa muda mrefu bila ya kazi lakini pia hata mshahara hawapati.
“Tumefuatilia barua ya ukomo wa kazi yetu hatupewi, tumekwenda NSSF lakini tumeambiwa kuna malimbiko mengi ya mshahara bado hayajapelekwa kwenye mfuko huo, tumewatafuta viongozi wa Chama bado hatujasaidiwa” Jackson Kangoma, Mwalimu.
Wafanyakazi hao wamemwangukia Rais Samia ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, kuwasaidia ili waweze kupata haki yao, kwani viongozi wengine wa chini yake wameshindwa kuwasaidia.
“ Tunamuomba mama yetu, kipenzi chetu, Rais wa wanyonge, atusaidie kwenye hili, sisi wastaafu na hawa wengine ambao bado wameajiriwa lakini shule haifanyi kazi, tunateseka sana, tunaomba aingilie hili, atusaidie,” amesema Jeremiha Magige.
=============
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Shemsa Mohamed, amesema anafahamu madai hayo na anafuatilia ili kuyafanyia kazi.
"Madai yao yamekuwa yakijadiliwa katika vikao vya jumuiya ya wazazi na sisi kama chama, tumekuwa tukifuatilia kwa karibu hivyo ninaomba niendelee kufuatilia ili nije na taarifa sahihi kuhusu madai hayo," amesema Shemsa.